Huyu mgombea wa chama cha sauti ya umma SAU ukitafakari kwa undani Sera yake ni muhimu sana coz lishe ndio iliyotusaidia kwy janga la coronaChama cha Sauti ya Umma (SAU) kimesema kina sera ya kuboresha maisha ya Mtanzania kwa kuhakikisha Mtanzania anakula lishe bora, ili mtu aweze kula kuku mzima na kama anakunywa chai basi aweze kuwa na siagi, matunda, mayai na mboga.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Moshi Mjini kupitia SAU amesema wanaonelea jambo la lishe bora kuwa sera nzuri kwa kuwa Watanzania wana afya mbaya kutokana na kula vipande vipande. Amesema unapokula kuku unapaswa kula kuku wote sio vipande.
Aidha kwa sera zake juu ya jimbo analogombea amesema atapanda miti ya matunda jimbo zima ili watu waweze kula matunda bure na wameshapanda matunda katika barabara ya New Street ambayo watu wanaendele kuyatumia matunda hayo.
Amesema zoezi hilo limesaidia kuleta kivuli aidha hadi sasa ameshafanikiwa kushusha jotoridi la Moshi kutoka Nyuzi Joto 40 na sasa zimefikia nyuzi joto 18.
Ila ukiangalia kwa kufikiria kuku tu utakuwa bado huja muelewa
Hongera kwake