Saudi Arabia inasema imewanyonga Wairani 6 kwa ulanguzi wa dawa za kulevya huku Iran ikilaani vikali.
Saudi Arabia ilisema Jumatano kwamba ufalme huo umewanyonga wanaume sita wa Iran kwa ulanguzi wa dawa za kulevya, jambo lililozua pingamizi kali kutoka Iran wakati nchi hizo mbili zikijaribu kurekebisha uhusiano.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia ilisema watu hao sita walikamatwa wakiingiza hashish katika ufalme huo na waliuawa baada ya rufaa kukataliwa na Mahakama ya Juu ya nchi hiyo. Haikusema ni lini hii ilitokea.
Adhabu hiyo iliambatana na sheria za Kiislamu maarufu kama (Islamic Sharia Law) na ililenga kuwalinda raia na wakaazi wa Saudi Arabia" kutokana na janga la dawa za kulevya," wizara hiyo ilisema.
Itakumbukwa kwamba Saudi Arabia na Iran ndio mataifa yanayoongoza duniani kwa kutekeleza adhabu ya kifo kwa kunyonga watu chini ya sheria zao za kiislam.:
Saudi Arabia says it executes 6 Iranians for drug smuggling