Saudi Arabia kuendelea kutumia dola katika biashara ya mafuta

Saudi Arabia kuendelea kutumia dola katika biashara ya mafuta

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
14,885
Reaction score
18,083
Saudi Arabia itaendelea kutumia dola ya Kimarekani katika biashara ya mafuta baada ya kuona kwamba kuachana na sarafu hiyo yenye nguvu duniani itaiathiri uchumi wake.

Saudi Arabia bado haijathibitisha ikiwa inataka kujiunga na muungano wa BRICS na imesimamisha uamuzi huo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

BRICS iliialika Saudi Arabia kujiunga na umoja huo wakati wa mkutano wa kilele wa 2023 na Ufalme huo bado haujakubali mwaliko huo na kutoa jibu. Baada ya kuamua kuhusu BRICS, kampuni kubwa ya mafuta ya Saudi Arabia Aramco imeanza kutoa bondi za dola za Marekani.

After Pausing BRICS, Saudi Arabia Starts Issuing US Dollar Bonds
 
kuna haja ya watu kufahamu zaidi mkataba wa Petrodollar upoje ili kuondoa mkanganyiko uliopo.
 
dogo kwani akiuza kwa dollars au kwa euro tofauti yake nini? Si zinaenda kwenye bank yake au zinaenda US 😄
 
Suala ni kwamba atauza mafuta yake kwa dollar pekee au atapokea pesa zingine kama Euro, Sterling, Renminbi nk nk.
 
Saudi Arabia itaendelea kutumia dola ya Kimarekani katika biashara ya mafuta baada ya kuona kwamba kuachana na sarafu hiyo yenye nguvu duniani itaiathiri uchumi wake.

Saudi Arabia bado haijathibitisha ikiwa inataka kujiunga na muungano wa BRICS na imesimamisha uamuzi huo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

BRICS iliialika Saudi Arabia kujiunga na umoja huo wakati wa mkutano wa kilele wa 2023 na Ufalme huo bado haujakubali mwaliko huo na kutoa jibu. Baada ya kuamua kuhusu BRICS, kampuni kubwa ya mafuta ya Saudi Arabia Aramco imeanza kutoa bondi za dola za Marekani.

After Pausing BRICS, Saudi Arabia Starts Issuing US Dollar Bonds
Ni jambo jema sana
 
Machawa wa marekani mnatuletea ushuzi mwingi sana humu jamvini. Hiyo dollar yenyewe imeshasusiwa na mataifa kibao tena yenye uchumi mkubwa tu.
 
Zitaje hizo nchi ambazo hazipokei pesa ya marekani? Achana na mrusi ambaye haruhusiwi kupokea Wala kutuma pesa kwa mfumo wa Money Swift.
Sasa niachane na urusi kwani urusi siyo nchi? Nyie machawa wa US vipii
 
Sasa mchina kutransact na mataifa hayo haimanishi hapokei dollar wakileta uwe unaelewa. Tanzania tunafanya biashara na Kenya na tunapokea Ksh je dollar haturuhusu kupokea ukiwa wafanya biashara wa Kenya watakuja na USD?
Wewe ndio huelewi ile transaction flow inapungua kwahiyo lazima iwe na athari kwa dola
 
Back
Top Bottom