500,000 acres, the kind of land said to be owned by just one, Kenyatta family in neighbouring Kenya.
Hivi kama kuna mtu ametazama the vast underutilised land from the air, say flying from kigoma to dar or from mtwara to dar. Kuna tatizo gani hasa kwa "kuwakodisha", ambapo serikali bado itakua na uwezo wa kunyanganya ikiona mambo sivyo ndivyo. Maana kama ingekua kama kwa wenzetu Kenya ambapo the Kenyatta's "wanaimiliki" hiyo acre 500,000 for good, ningeona tatizo.
Cha msingi ni kuhakikisha mutual benefit, kwa mfano, wasaudi wanaweza kukodishwa say acre 100,000 halafu wakapewa condition ya kuziendeleza na kuwa soko la acre 400,000 za satellite farms za watanzania wenyeji wa maeneo husika(sio vigogo pekee). As hakuna free lunch duniani, hakuna mtu wa kuja kuwekeza mabilioni, kwa faida yetu sisi tu.
Isije ikawa tunawapigia kelele wasaudia, then sharp minded crook mtanzania mwenzetu, tena mweusi tiii, akachukua yeye hiyo ardhi ya acre 500,000, akaingia deal na wasaudi ya kusupply chakula Saudi Arabia kwa benefit yake na familia yake....tukabaki tunang'aa macho. Mi nafikiri kuna umuhimu wa kuitazama hii proposal kwa mapana zaidi, badala ya kuwa paranoid kwa taifa flani, halafu tukawa blind mweusi mwenzetu akifanya.
Cha msingi, ni kama baadhi walivyosema, huo mkataba uwe na mutual benefit, kwa wawekezaji na watanzania, ikiwemo training on modern agricultural practices kwa watanzania wa satellite farms. Kwa dunia ya sasa, hatuwezi kuchomoka tulipo, kama tukigoma kushirikiana na waliotutangulia. Miaka ile ya Mwalimu, ambapo tofauti ya dunia ilikuwepo si kubwa ya kutisha, labda. Miaka ya '70s daktari bingwa wa muhimbili alikua anaweza kwenda London na kuanza kutibu shortly. Leo hii hataweza, sababu wametupita mbali mno ki vifaa, mbinu na technolojia, kiasi kwamba atabaki anang'aa macho. Hivyo hivyo unaweza kusema kwa mtaalam wa kilimo, Laboratory technologist, electronic engineer etc. Wenzetu wanakimbia at full flight. Tutazame the big picture, moving forward.