Sauna

Sauna

ablood8

Senior Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
181
Reaction score
90
Wana JF,

naomba kujua faida au madhara ya hii kitu inaitwa sauna
 
Faida zake zipo nyingi baadhi ni kama kutoa sumu aina ya heavy metals mwilini, kushusha blood pressure, kupendezesha ngozi, kuufanya mwili u relax na hivyo kuondoa stress, uchovu na kusababisha upate usingizi vizuri, husaidia hata kupunguza uzito (ingawa uzito utarejea mara utakapokunywa maji). Ila ni hatari kwa watu wenye low blood pressure kwani sauna hushusha sana pressure. Sauna pia zipo za aina nyingi, faida zake hutofautiana kidogo hivyo ni lazima ujue aina ya sauna unayotaka kutumia. Google benefits of sauna ujifunze zaidi
 
Stwita nashukuru sana kwa maelezo yako kidogo nimepata mwanga na pia nita Google kupata maelezo zaidi
 
Is there place like this in Tanzania
 
Kwa Dar es salaam wapi Sauna affordable naweza kupata ❓
 
Kuna Local Sauna ipo huku pande zetu. Napenda sana kuitumia huyeyusha fatty zilizoko mwilini. Hufanya blood circulation iwe sawa. Pia hufungua vinyweleo vya mwili.
Kwa wale wasiokua na mazoezi ya mwili ni nzuri pia kuufanya mwili uwe aktive.
 
Bongo kuna sauna asilia
unachemsha maji yanakuwa ya moto hafu unajifusha uku ukiwa umejifunika na shuka
utatoka jasho la kutosha ila cha moto utakiona
 
Jaman hiyo sauna ndy nn wengine hatujui , naomba kujuzwa kwa niaba ya wengine cc ablood8 stwita falcon mombasa

Sauna ni chumba fulani ambacho kina joto la hali ya juu. watu hukaa humo kwa muda fulani ili miili yao ipate joto na kutokwa na jasho. Joto hili linaweza kutengenezwa kwa umeme ama kwa njia ya asili.
Njia ya asili ni kuweka kitu kama jiko kubwa la kuni halafu kupitisha mtungi wa joto (chimney) kutoka kwenye hilo jiko mpaka kwenye hicho kichumba mara nyingi kinakua cheusi ili joto lisharabu.
 
Back
Top Bottom