Saut: Musa na sautso waichafua, wanafunzi wengi waacha chuo, ukahaba nje nje.

don-oba

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Posts
1,387
Reaction score
677
Ikiwa tayari wanafunzi wengi wamemaliza UE na wengineo kukaribia maliza hivi karibuni, tayari idadi kubwa ya wanafunzi wameacha chuo kutokana na ukata mkubwa uliosababisha kufukuzwa kwenye nyumba walizokuwa wakiishi. Akiongea kwa masikitiko huku machozi yakimtiririka km mtoto mchanga mmoja wa wahanga hao ajulikanae kwa jina moja la HAPPY amemtupia lawama 'MUSSA' ambaye ndiye anashughulikia mikopo ya wanafunzi.. "tangu mwezi wa 11 naenda ananiambia jina langu liko allocated akaniomba a/c yangu kwamba pesa itaingia hadi leo sijapata hela" alisikika binti huyo akiongea kwa machungu huku akiwa amekalia mizigo yake iliyokuwa imetolewa nje na mwenye nyumba kutokana na kudaiwa pesa ya pango. Hadi sasa wanafunzi 215 tangu mwezi Sept mwaka jana hawajapata pesa zao za kujikimu, sababu kuu inadaiwa ni uzembe unaofanywa na serikali ya wanafunzi SAUTSO kushindwa kufuatilia suala hilo kwa ukaribu huku pia wakidai MUSSA amekuwa akitoa majibu ya ovyo kila wanapomfuata. Wanadai kwamba ni MUSSA huyohuyo ndiye aliyechelewa kupeleka matokeo yao kwa wakati kiasi cha kupelekea kukosa pesa zao kwa wakati. Hadi sasa semister imeisha haijulikani ni lini wanafunzi hao watapewa pesa zao. Tayari kuna baadhi ya wanafunzi wa kike wamejiingiza kwenye ukahaba. Inasemekana wanauza miili yao katika uwanja maarufu wa 'ODINGA' pia maeneo ya ATM nyakati za usiku ukipita na gari wanakusimamisha kuomba lift na akishapanda atakuelezea shida yako. Wanafunzi hao ni miongoni mwa wale waliokosa pesa yao ya kujikimu. Vyombo vya habari jijini Mwanza tayari vimeisharipoti jambo hili. Watu wengi wametoa maoni yao wakiushutumu uongozi wa juu wa chuo hiki unaoongozwa na mapadre wengi kwamba umeshindwa kumfukuza kazi Mussa. Pia wamelaumu uongozi wa serikali ya wanafunzi SAUTSO ambao uliingia madarakani kwa kujipambanua kwamba ni makamanda chini ya Malisa umewatelekeza wanafunzi wao.
 
jamani mkienda ivo mnapotea!!! hii nchi inasikiaga lugha moja tu!! MGOMO!!!!
 
Polen sana jamani! Mi nilipitisha mwaka mzima pesa ya mkopo haieleweki,nusura niache chuo kila ukienda kwa viongozi hakua kinachoeleweka, na mwisho hao kina Mussa na waziri wa mikopo huishia kuomba rushwa.Mi hapo nshatoka hivyo mazingira magumu ya main campus nayajua vema. Lawama kubwa ni kwa viongozi,kwani nakumbuka tution fee yangu ya mwaka mmoja mzima haikuja na kunifanya niishi katika hli mbaya. Binafsi namshukuru Mungu kwakuwa nimemeliza salama japo kwa misukosuko kama hiyo. Kuhusu hao dada zetu kuwa katika hali hiyo mi nathubutu kusema uongozi pamoja na kukusanya mabilioni ya fedha wameshindwa kulitafutia tatizo la malazi kwa dada zetu. Pia wanashindwa kufuatilia mikopo ya wanafunzi huku wakijua wazi kuwa 90% ya wanafunzi ni toka familia maskini.Chuo kinajinasibu kuwa cha kidini lakini hakina huruma. Nimewakumbuka rafiki zangu walio nyimwa vitambulisho vya kufanyia UE eti kisa hawjamaliza madeni. Tafadhali uongozi umwondoe Mussa kwakuwa amelewa madaraka na anadharau kwa wateja pia na kauli chafu nyakati zingine. Poleni wanaSAUT main campus!
 
Peleka habari yako Chuoni au kwa Ofisi zinazohusika na mikopo.kijana naona unapenda sana kutangaza shida
 
jamani mkienda ivo mnapotea!!! hii nchi inasikiaga lugha moja tu!! MGOMO!!!!

mkuu LORDVILLE umenifurahisha sana, ila hii kitu inaitwa 'MGOMO' huwa haipo SAUT. Na ichi ndio kinachowaponza!
 
Ni kweli mataizo yapo lakini ndio Msomi abadilishe utu kwa pesa!!?? Sijui wasomi hawa wanajenga taswira gani kwa jamii!!?? Ni aibu kubwa kwa wanawake na kwa taifa.
 
Nasikia ukahaba unasababishwa na bodi ya mikopo hivi ni kweli?
 
Peleka habari yako Chuoni au kwa Ofisi zinazohusika na mikopo.kijana naona unapenda sana kutangaza shida

mimi sina shida mkuu, nimejitosheleza kabisa. Ninachofanya ni kuwapigania hawa wadogo zangu kupitia jukwaa hili, wahusika wanaweza kupita.
 
Sitaki hata kumsikian huyu musa, kijana mwenye majivuno, majibu ya kunya, uongo hata mbele ya mapadri anaongopa hana utu, ninasema maana namfahamu vilivyo na tulikwaluzana sana kabla sijaondoka hapo na kama wewe akili haipo kwa kichwa atakukomesha.

Ushauri wangu, watu wengi SAUT ni waoga kusimamia ukweli, kama mtu unauhakika pesa yako imekuja, kwa nini akuzungushe, binafsi tulizungushana hadi kwa boss wake, mtu mwenyewe na Baed ya Geography anamalingo kama ndo kamaliza kila kitu, kunawafanyakazi SAUT wanakiburi kwa sababu tu wanauhakika wanafunzi hawawezi goma na wakiwa aggressive chuo kitawatimua!
 
natafuta bunduki nimpige jamaa au nimpige shoti ya umeme au kumwagia tindikali kwani amenifanyia kitu kibaya,hajapereka matokeo yangu bodi adi sasa
 
jamani mtu kama huyo mbona ni kazi ndogo?? sasa mkijidai wema eti kisa mnasoma chuo cha dini itakula kwenu....mi nashauri wanafunzi kama wanafunzi mkae na mjadili na wakuu wa chuo kuhusu matatizo yawakumbayo...na kama ikiwezekana wekeni MGOMO yes namaanisha mgomo jamaa aondoke,bila hivyo mtalalama tu na hamna litakalotokea......dah ila poleni sana hasa hao dada zetu!!!!
 
Peleka habari yako Chuoni au kwa Ofisi zinazohusika na mikopo.kijana naona unapenda sana kutangaza shida

yani wewe ni mse*** namba moja mpaka jamaa unamuona kauleta huu uzi hapa inamaana atakuwa meenda kunapohusika au wewe ndiyo musa watu wanalia njaa wewe unajibu shombo puumbafu maa fanta wewe poleni wadogo zetu mungu atawasaidia tu msikate tamaa.
 
miye nawashangaa sana nyie wanafunzi mnaogopa fukuzwa chuo kisa mnadai haki yako kipi bora sasa ufukuzwe chuo kisa mmeenda kundi kuchoma moto nyumba ya huyo musa, kisa unadai haki yako anajibu ovyo? Au ubebe mabegi ujifukuze chuo kisa ada, kodi, pesa ya pango imekushinda unamua jifukuzisha chuo mwenyewe kwa kurudi nyumbani kisa musa mnayemsema na mwenzake wachache wanachezea maisha yenu sikieni nyie jikusanyeni bebeni lita tano ya petrol mpaka anapokaa huyo musa funjeni milango mwageni mafuta washeni moto maana hii nchi pasipo action tunachezeana sana akili zetu hichi ndiyo dawa ya mnyonge kwa sasa over.
 
Wanafunzi wa siku hizi ni zaidi ya ajabu kabisa. Kipi bora uondoke peke yako au ufukuzwe kwa kufanya mgomo ili ujumbe uwafikie!
 
Kufukuzwa kazi si suluhisho!!!! Kwa nini tusiseme mfumo uangaliwe upya na kurekebishwa???
 
ndo taabu ya kusoma chuo cha dini hata kudai haki mnaogopa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…