don-oba
JF-Expert Member
- Dec 8, 2011
- 1,387
- 677
Ikiwa tayari wanafunzi wengi wamemaliza UE na wengineo kukaribia maliza hivi karibuni, tayari idadi kubwa ya wanafunzi wameacha chuo kutokana na ukata mkubwa uliosababisha kufukuzwa kwenye nyumba walizokuwa wakiishi. Akiongea kwa masikitiko huku machozi yakimtiririka km mtoto mchanga mmoja wa wahanga hao ajulikanae kwa jina moja la HAPPY amemtupia lawama 'MUSSA' ambaye ndiye anashughulikia mikopo ya wanafunzi.. "tangu mwezi wa 11 naenda ananiambia jina langu liko allocated akaniomba a/c yangu kwamba pesa itaingia hadi leo sijapata hela" alisikika binti huyo akiongea kwa machungu huku akiwa amekalia mizigo yake iliyokuwa imetolewa nje na mwenye nyumba kutokana na kudaiwa pesa ya pango. Hadi sasa wanafunzi 215 tangu mwezi Sept mwaka jana hawajapata pesa zao za kujikimu, sababu kuu inadaiwa ni uzembe unaofanywa na serikali ya wanafunzi SAUTSO kushindwa kufuatilia suala hilo kwa ukaribu huku pia wakidai MUSSA amekuwa akitoa majibu ya ovyo kila wanapomfuata. Wanadai kwamba ni MUSSA huyohuyo ndiye aliyechelewa kupeleka matokeo yao kwa wakati kiasi cha kupelekea kukosa pesa zao kwa wakati. Hadi sasa semister imeisha haijulikani ni lini wanafunzi hao watapewa pesa zao. Tayari kuna baadhi ya wanafunzi wa kike wamejiingiza kwenye ukahaba. Inasemekana wanauza miili yao katika uwanja maarufu wa 'ODINGA' pia maeneo ya ATM nyakati za usiku ukipita na gari wanakusimamisha kuomba lift na akishapanda atakuelezea shida yako. Wanafunzi hao ni miongoni mwa wale waliokosa pesa yao ya kujikimu. Vyombo vya habari jijini Mwanza tayari vimeisharipoti jambo hili. Watu wengi wametoa maoni yao wakiushutumu uongozi wa juu wa chuo hiki unaoongozwa na mapadre wengi kwamba umeshindwa kumfukuza kazi Mussa. Pia wamelaumu uongozi wa serikali ya wanafunzi SAUTSO ambao uliingia madarakani kwa kujipambanua kwamba ni makamanda chini ya Malisa umewatelekeza wanafunzi wao.