SAUT Mwanza yasimamisha wanafunzi 8!

Yani kwa kifupi,wamefukuzwa chuo,naona mnauma maneno. Tena mmojawapo ni clasmet wangu,procurement 2. Jamaa alikuwa analiweza sana hilo somo alilokamatwa kaandika mkononi majibu,Cost Acc. Alianzia cheti,hakuwahi kupata B plus,ni A tu kwnye cost. Sasa,tunajitahdi apunguziwe adhabu,arudie mwaka. Tulitegemea aende akamuone VC,Tumeckia VC nae kajiuzuru. Mkosi 2
 

Mkuu sijawahi ona watu wenye roho ngumu Kama warumi!!!
Kama unadaiwa 500 tu wanakunyima exam no leo ndo watamrudisha chuo?? Hawana huruma hawa jamaa kozi hawana watoto!!!
Ulishawahi ona wapi mtu unamwekea deadline ya kulipa Ada?? Baada ya hapo unalipa with penalty ya laki? TCU mulikeni hiki chuo!!
Maana nimetoka kumlipia mdogo wangu,yamenikuta!!
 

Katika kila kitu kinachofanyika,wanachakachua tu. Katika Tanzania yetu wachakachuaji ndio wanaofanikiwa! Wanaofuata haki ndo the losers kwa asilillimia kubwa. ref bunge la katiba.
 

ni kweli hawana huruma hata kidogo
 
Kuibia mtihan nikosa la jinai na adhabu yake ni kufukuzwa chuo na kufungiwa masomo miaka 5. Achen siasa kile chuo kizur sana kinatenda ipasavyo hata kama ungekuwa ifm au udsm hata chuo chochote wangefukuzwa tu ndo sheria nyie mnataka ubabaishaji. Afu suala la ada nan alokwambia chuon kuna bagain ya ada hamna shukuran kunachuogan cha private kinalipa ada ndogo kama saut au mnaongea t.mnajua ada ya arusha university ilivyokubwa na michango mingne ya ziada na maxngra magum ya kusomea. Na hakunachuo kinachoruhusu kudanya mtihan kama hujamaliza ada hata 100 labda vya serikali.achen kuingia na vbut serious in studying.
 
Nina uzoefu wa vyuo vikuu saba (vingine nikiwa nasoma, na vingine nikiwa nafundisha). Vyote hivyo adhabu ya kuchakachua kwenye mtihani ni kukatishwa masomo.

Shukuruni kuwa na chuo kizuri kama SAUT. Huyo anayesema hawana huruma "kwa sababu hawana watoto" nimwambie tu kwamba "shukrani ya punda ni mateke".

Forgive them, for they know not what they say.
 

Elimu yetu ni majanga - hivi mwanafunzi wa elimu ya juu unaibia hii ina maana gani kwa mustakabali wa jamii yetu?
 
huyo jamaa yenu ni cheater mzoefu,Hizo A A zote anazipataga kwa njia hiyo.za mwizi 40.so atimae amedakwa na atakiwi onewa huruma.Seminary nilosoma mimi,Maua ukiwa form one kulikuwa na mwalimu specialiast wa kukamata watazamiaji au wenye kuingia na majibu kwenye test/mitihani ukikamatwa unafukuzwa shule akuna mjadala.Huyu jamaa awezi kuwa na akili alafu akamatwe na vijikaratasi vya majibu....huyo ni mburura kilaza a.k,a Kihiyo
 

hamsomi sheria za chuo ndugu zangu? hakuna chuo kitakachokulea kama utakamatwa na ushaid umeibia kwenye UE, hiyo ni sheria na waondoke kwa amani kabisa. ikumbukwe kwamba, warumi na waarabu siyo waliotunga sheria hiyo, tuache kuzunguka, tuangalie sheria zinasemaje.
kutegemea wizi ndo kunaendelea kuzalisha wataalamu wabovu nchini na nadhan hata hawa CCM wanaoiba kura walianza kuiba majibu ya mitihani.

NB: Neno lako la warumi limekaa kidini zaidi, tuache udini, hautatujenga, unapoona chuo hukiwezi, basi usisome hapo, nchi yetu ina vyuo vingi. by the way, watu mnaosema SAUT ni ngumu, tafuten mashahidi waliomaliza SUA miaka ya 2008 enzi za Prof MLAMBITI na yellow book yake ndo mtajua maana ya ugumu wa chuo.
ACHENI UVIVU, VINGINEVYO MTAINGIA NA NONDO NA MTAFUKUZWA TU.
Mungu ibariki TANGANYIKA.
 

Sina Pingamizi Na Hatua Hiyo Kwani Nina Heshima Kubwa Sana Ya Chuo Kikuu Hicho na Kwa Nijuavyo tu Ni Kwamba Hao Waliofukuzwa Hawajaonewa na Isitoshe Wanastahili Kufukuzwa Kwani SAUT Siyo Chuo cha Wanafunzi Wazembe na Goigoi. Mafanikio Yangu Ya Leo Ni Ubora na Uimara Wa Chuo Kikuu Changu Kipenzi Cha Mtakatifu Augustino Kipindi Hicho Kikiwa Chini Ya Father Charles Kitima ( CK ). Najivunia Sana Kuwa Mwana SAUT ( BA ) 2006 - 2009 na Najivunia Tena Kuwa Mwana SAUT 2013 - 2015 ( MA ) na Mwenyezi Mungu Akipenda Natarajia tena Kuwa Mwana SAUT 2020 - 2024 ( PHD ). Nawapongeza SAUT Kwa Kuondoa Hizo TAKATAKA Nane ( 8 ), Hata Mimi Wameniudhi na Kunikera Sana. Big Up Sana Vice Chancellor Mpya Uliyemrithi Dkt. Kitima.
 
ni kweli hawana huruma hata kidogo

Kama Mtu Mzima Kama Wewe Leo Unataka Tasnia Ya Elimu Iwe na Huruma Kwa Wanafunzi Wenye Utovu wa Nidhamu tena wa Kuibia ktk Mitihani basi Sina Shaka Kuwa Hakika Sasa Elimu Ya Tanzania Ipo ktk Shimo La TEWA. Nimekudharau Sana Mwana JF Mwenzangu Na Nina Mashaka Sana Na Uwezo Wako wa Kufikiri na Hata Kama Utakuwa Umesoma basi Kwa Upuuzi Uliouandika Nina Uhakika Ulikuwa UNA DESA Sana. Hivi ktk Elimu Huwa Kuna Huruma????? Kwahiyo Una Maanisha Kwamba Mwanafunzi Akikutwa na Nyenzo Asamehewe Akienda Kinyume Na Taratibu Za Chuo Pia Asamehewe???? Hivi Wewe Una Akili Sawa Sawa????? Huruma ktk Elimu Kwa Ujinga Wa Wanafunzi Wenyewe???? Yaani Umenipandisha Hasira Zangu Za Kizanaki na Nimechukia Kupita Kiasi na Na Log Out Kabisaaaaa.........:shocked:
 

Mkuu naomba uwe unasoma vizuri post za watu!!
Nimesema hawana huruma kwenye suala la ADA ya chuo hata kama uwe unadaiwa Tshs 500 wanakunyima exam no!!
Suala la hawa madesa wanaozama na vijikaratasi kwenye paper acha wapewe adhabu tu!!
Pia mimi nimesoma Saut Ada 2005-2008!! Naijua vizuri Saut!!
 

Unaposema neno warumi limekaa kidini zaidi unamanisha nini??
Maana mimi mwenyewe mkotoliki, nimeanza kuwajua hawa jamaa pindi natumikia church!!
Nazani hujaelewa,nasema iweje watu wapele deadline ya kulipa Ada ya chuo?? Wakati wanajua kabisa wanatoa msaada?? Maana wanachaji gharama za chini sana!!
Na wanajua kabisa maisha ya waamini wao kwamba tunajikamua hadi zaka tunashindwa kutoa ili watoto wakasome,na wanajua kabisa tunaunganga kupata pesa! Hao waliofukuzwa ni halali yao!!!!
 

Prof MLAMBITI? umenikumbusha kitu. hii prof iko safi kichwani aisee, naikubali,haina ubabaishaji
 

Usipende kukalili kua kila uonapo kichaka ...............!!!
Ni kweli wanatoa degree kwa Ada ya chini sana!!
Kwa mfano Advanced Diploma kwa wakati nasoma mimi tulikua tunalipa Tshs 650,000÷2= 325,00/= administration cost Tsh 254,000÷2= 125,000/= hapa nilitakiwa nilipe Tshs 450,000/= hadi siku ya kuanza UE bila ya kupewa deadline!! Tulikua tunaanza masomo mwezi October !! Nilikua nalipa Ada kwa mafungu!! Sasa iweje leo waanze kusema mwisho wa kulipa Ada ni mwezi march 30 wakati second semester inaenda hadi mwezi June?? Huoni kuweka deadline ya kulipa Ada wanataka pesa za lazima toka kwa wazazi?? Mbona wanaolipiwa na HESLB hawajawapa deadline pia?? Wanaofukuzwa chuo kozi ya paper ache wapewe adhabu yao!!!!
 

Kamanda Saut uliingia lini na ulitoka lini? Kuna mtu alikamatwa anacheat kwenye paper,aliichukua ile karatasi na kuitafuna! Hadi msimamizi akamwambia toa basi walau pini,maana ingemchoma!! Hakufukuzwa chuo na leo anafanya kazi UN!!
 
Saut inasemekana now kuna uhaba wa pesa (tetesi) hata penalty za vitu kama mavazi na utovu mwingine wa nidhamu zipo nje nje. Wana miradi, wana walimu, walinzi, wafagiaji, mafundi na masista. Kiufupi hivyo vitu haviwezi jiendesha ndo maana linatokea hili. Usishangae sana bwana Mawazo. Ni taratibu na ushauri walioupata katika ngazi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…