hamsomi sheria za chuo ndugu zangu? hakuna chuo kitakachokulea kama utakamatwa na ushaid umeibia kwenye UE, hiyo ni sheria na waondoke kwa amani kabisa. ikumbukwe kwamba, warumi na waarabu siyo waliotunga sheria hiyo, tuache kuzunguka, tuangalie sheria zinasemaje.
kutegemea wizi ndo kunaendelea kuzalisha wataalamu wabovu nchini na nadhan hata hawa CCM wanaoiba kura walianza kuiba majibu ya mitihani.
NB: Neno lako la warumi limekaa kidini zaidi, tuache udini, hautatujenga, unapoona chuo hukiwezi, basi usisome hapo, nchi yetu ina vyuo vingi. by the way, watu mnaosema SAUT ni ngumu, tafuten mashahidi waliomaliza SUA miaka ya 2008 enzi za Prof MLAMBITI na yellow book yake ndo mtajua maana ya ugumu wa chuo.
ACHENI UVIVU, VINGINEVYO MTAINGIA NA NONDO NA MTAFUKUZWA TU.
Mungu ibariki TANGANYIKA.