Mimi niko SAUT pia, nina mkopo na nyumbani kwetu pia hawana uwezo kama ambavyo wewe unavyojieleza. Lakini kwa fedha hiyo hiyo ya mkopo, nimelipa chumba, nimelipa ada yote ya muhula wa kwanza, na ninakula vizuri tu na nitafanya mitihani.
Tatizo la wengi wanaopata mkopo ni Personal Financial Management ni mbaya.
SAUT ninayoijua ni SAUT ya leo, na sioni tatizo na hayo mambo. Suala la ulipaji wa ada wanapaswa kukazia hivyo hivyo, vinginevyo watashindwa kulipa walimu, watashindwa kulipa umeme, na baadaye wewe huyo huyo utarudi hapa na kufurahia hali hiyo.
Uongozi wa SAUT uko sawa kubana watu walipe, wenye matatizo inabaki ni "exceptional cases" ambazo zinapaswa kuwa handled in an exceptional way. Na wengi waliopeleka hizo "exceptional cases" wamefanyiwa exception na kupewa kadi za kufanya mtihani.
Inawezekana kweli una shida, lakini naona mada hii umeileta ukiwa na lako jambo. Kichwa chako cha habari kinaweka wazi kuwa una kampeni ya majitaka dhidi ya SAUT, vyuo na shule za kanisa!
I am proud to be a SAUT student.
Mkuu wewe unasoma kozi gani?