Nachotaka kusema ni kwamba nchi zote maskini ni nyasi ambazo fahari wawili hupigana..
Kwa wananchi hakuna mtu wa maana kati yao, sii huyo rais mzalendo Mtawala wala huyo mgeni fahari anayetaka kumiliki zizi..Wote hawa ni wezi wa mali zetu kina Mugabe, Chiluba, Mkapa upande mmoja.
Upande wa Pili pia unakuta madume haya yenye mbegu za kupandikiza kina US, UK, CHINA na kadhalika wote pia nia yao ni kuwa wao madume wa kumiliki chumi zetu.. Hakuna kati yao anaye care kweli maisha ya wananchi sipokuwa wanatumia siasa kututenganisha wananchi wapate kutawala vizuri uchumi wetu.
Vongozi wa nchi zetu maskini wote ni Mafisadi hawatupendi sisi ila umilikaji wa hizo maliasili na hawa wanaokuja na misaada pia hawatupendi macho yao ni hizo hizo mali asili na nishati zetu.... So who you gonna call!..