SoC03 Sauti kutoka ng'ambo

SoC03 Sauti kutoka ng'ambo

Stories of Change - 2023 Competition

Leetheboss

New Member
Joined
Jun 6, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoendelea kukua kiuchumi duniani na afrika kwa ujumla.Aidha nchi mbalimbali kama vile Nigeria,Afrika kusini,Ethiopia na Kenya ni nchi zenye uchumi mkubwa kusini mwa jangwa la sahara hii ni kutokana na miundombinu bora waliyonayo.tuchunguze baadhi ya miundombinu hiii.

Barabara ni moja ya miundombinu ambayo inasaidia mzunguko wa watu kutoka sehem moja hadi nyingine na usafirishaji wa bidhaa kutoka sehem moja hadi nyingine. Katika nchi yetu ya Tanzania miundombinu ya barabara katika sehemu nyingi ni mibovu hasahasa sehemu za vijijini na hii imesababisha baadhi ya bidhaa kuchelewa kufika kwa wakati.

Elimu ni mojawapo kati ya miundombinu muhimu uwepo wa shule,walimu wenye ustadi,vyuo na usafiri wa wanafunzi ni jambo muhimu katika ukuaji wa nchi kiuchumi aidha nchini Tanzania elimu imekuwa chamgamoto kutokana na uhaba wa shule na madarasa,ukosefu wa walimu ambapo baadhi ya shule zina walimu wachache ukosefu wa madawati na vifaa vya kufundishia ambapo idadi kubwa ya wanafunzi wameishia njiani na kuingia kwenye makundi kama vile wizi na utumiaji wa dawa za kulevya na hivyo taifa kupoteza vijana ambao wangekuwa nguvu kazi kwa taifa.

Nishati na umeme pia ni mojawapo ya miundombinu muhimu katika ukuaji wa nchi kiuchumi.umeme husaidia katika viwanda ambapo mashine nyingi hutegemea umeme ili kufanya kazi.Nchi yetu ni moja kati ya nchi zenye tatizo kubwa la umeme. Umeme uliopo hautoshi katika viwanda vikubwa aidha katika maeneo mengi umeme umekuwa chamgamoto kubwa na hivyo kuchelewesha shughuli za utoaji bidhaa na uzalishaji wa bidhaa nchini.

Viwanja vya ndege na bandali ni mojawapo kati ya miundombinu muhimu inayosaidia katika usafirishaji wa mizigo kutoka nchi tofauti kama Marekani na china baadhi ya viwanja vya ndege katika nchi yetu ya Tanzania ni midogo na hivyo ndege kubwa haziwezi kutua na hii imesababisha mikoa hiii isikue kimaendeleo na kuendelea kuwa uchumi mdogo.

Aidha vituo vya afya kama vile hospitali na zahanati,uwepo wa madaktari bingwa na madawa ya kutosha ni moja ya miundombinu katika ukuaji wa nchi kiuchumi kwa kusikitisha bado nchini Tanzania hamna madaktari bingwa wanaoweza kufanya upasuaji wa magonjwa makubwa kama moyo na ubongo na hivyo kufanya baadhi ya wagonjwa kutibiwa katika nchi nyingine kama Afrika kusini na India,pia upatikanaji wa vifaa vya matibabu umekuwa chamgamoto kubwa.


Faida za kuwa na miundombinu bora ni kama zifuatazo.

Miundombinu kama barabara na reli inasaidia kusambaza huduma kama vile huduma za maji hasahasa katika maeneo ya vijijini na hivyo kusaidia kupunguza kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu aidha Tanzania bado ina chamgamoto ya utoaji wa maji safi kwa wanachi na hivyo wananchi kutumia maji kutoka kwenye visima na mabwawa pamojana mito na chemichemi ambayo si safi na kuzua magonjwa na hivyo serikali kutumia fedha kwa ajili ya madawa badala ya kwekeza kwenye ukuaji wa nchi kiuchumi.

Inasaidia usafirishaji wa bidhaa kutoka sehem moja hadi nyingine mfano dawa za hospitalini,vifaa vya elimu na kukuza uchumi wa nchi kwa haraka.

Umeme pia husaidia uzalishaji wa bidhaa viwandani na hivyo kutengeneza bidhaa nyingi nchini ambazo zinawezwa kuuzwa nje ya nchi na kutengeneza pato la taifa.

Husaidia kukuza pato la nchi ambapo bidhaa nyingi na huduma zitazalishwa na watu wataweza kuuza na kununua.

Nini wajibu wa serikali ili kuweza kukuza uchumi kupitia sekta ya miundombinu.

Serikali ina wajibu wa kuhakikisha kwamba miundombinu kama barabara inajengwa kwa wakati na kuwasimamia wakandalasi ili wasile pesa bila kufanya kazi.mfano barabara ya kigoma hadi Nyakanazi imekuchukua zaidi ya miaka mitano(5)kutengenezwa hii ni kutokana na kutowajibika kwa wakandalasi na serikali na hivyo watu wanashindwa kusafirisha bidhaa kutoka bukoba hadi kigoma na hivyo kufanya mkoa huu kuwa duni kimaendeleo na kudhoofisha pato la nchi.

Aidha serikali ina wajibu wa kuhakikisha kwamba wana boresha sekta ya elimu kwa kutoa walimu wenye ustadi na vifaa vya kufundishia ili wanafunzi waweze kujifunza kwa vitendo.

Pia,serikali ina wajibu wa kuhakikisha kwamba wanaongeza na kupanua viwanja vya ndege na bandali ili kuweza kupokea bidhaa nyingi kutoka sehemu mbalimbali na kusafirisha bidhaa kutoka nchini kwenda mataifa tofauti na kukuza pato la nchi.

Serikali ina wajibu wa kuhakikisha kwamba inanunua vifaa bora vya matibabu ili baadhi ya matibabu makubwa yaweze kufanyika ndani ya nchi yetu na kutoa elimu ya juu kwa wanafunzi hasahasa madaktari ili waweze kutokeza madaktari bingwa ndani ya nchi yetu badala ya kwenda nchi jirani kufuata matibabu.

Mwisho,serikali ina wajibu wa kuhakikisha kuwa inatengeneza na kuboresha miundombinu nchini ili kuweza kukuza uchumi wa nchi na pia kuboresha maisha ya wananchi wa Tanzania aidha ina wajibu wa kusimamia kwa umakini utekelezaji wa miundombinu hiyo ili kuweza kukamilisha kazi kwa wakati na kwa kufanya hivyo nchi yetu itakuwa yenye uchumi mkubwa afrika na duniani kwa ujumla.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom