Bando la wiki
JF-Expert Member
- May 23, 2023
- 911
- 3,017
Ki ukweli sauti ya Mkandara Lufufu ilikuwa na upekee fulani hivi ambao haupati kwa watu wengi.
Ila hivi juzi nimeona tangazo la ngumi kati ya Karim Mandonga na Mada Maugo huku kuna jamaa kaingiza sauti kama ya Lufufu akisimulia namna mabondia hao wanavyotafutana msituni.
Sasa mimi nilikuwa naona ili kumuenzi shujaa Mkandara Lufufu (ni shujaa kwa sababu ndie mwanzilishi wa utaratibu wa kuingiza sauti na kutafsiri movies kutoka kwenye lugha za kigeni kuja kwenye kiswahili)
Huyo kijana apewe kuingiza sauti ya Lufufu kwenye movie itakayokuwa imeigizwa kuzingatia maudhui ya kitanzania hasa ikiwa ya kilugha kama kichaga, kihehe, au kisukuma ikionesha harakati za mashujaa wa kitanzania enzi za ukoloni walivyo jaribu kupambana na ukoloni.
Hapa movie inaweza kumhusu Shujaa kama Mangi Meri, Chief Mkwawa, au Mirambo n.k Movie ikiwa kwa mfano ya chief mkwawa kwa lugha ya kihehe na kibena, kijana huyo (Lufufu) itasikika sauti yake kwa kiswahili huku subtitles zikiwa kwa kiingereza.
Au movies nyingine inaweza kuwa pure action huku sauti ya Lufufu (kijana huyo) ikipita kwa maelezo.
Nadhani kwa kufanya hivi tutakuwa tumemuenzi sana Lufufu huku familia yake nayo ikifurahia matunda ya kazi ya baba yao.