Sauti ya nashi mc

dawa yenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
2,825
Reaction score
3,675
Naufananisha muziki na bahari kubwa, wavuvi wapo wengi na sokoni kuna samaki wa kila aina kuna samaki wana virutubisho vingi na ni watamu kweli ila hawana soko au labda wanachukuliwa poa na walaji kwa kuwa uuzaji wa samaki hao huwa hauambatani na vioja (kiki) ambavyo kuna wakati vinaweza kuuvua utu wa mvuvi.

Naam, yule mvuvi bora kati ya wavuvi bora tuliojaaliwa Tanzania katuletea samaki wa aina yake mwenye virutubisho vya aina. Anaitwa NASHI MC mimi namuita fundi wa kinasa (kiswahili na sanaa) katuletea mdundo wa maana, mdundo uliotulia, mdundo wa mahadhi ya hip hop.

Wale wazee wa muziki na elimu hapa ndio mahali pake. Tutoe support kwa hawa wasanii wa hip hop asilia maana kazi wanayofanya na wanachokipata hakika havifanani.

Sauti ni wimbo mkali ambao napendekeza tuusikilize wanajf.... Ukihitaji nifuate PM maana hata yeye kasisitiza turushiane ili sote tuupate ujumbe uliokusudiwa.

Hip hop sasa, siku zote na milele.
Amina
 
Irushe hapa hapa, moja kati ya maandishi yake ninayoyakubali no ile ya "maneno"
 
Nash MC Zuzu .
Muhaya jeuri aliyemdindia ruge na radio yake ya mashoga.
 
Maalim Nash a.k.a Uchebe chaka!

-Kaveli-
 
Hamna kitu huyo boya, na miguu yake kama banio! Alafu anajifanyaga anajua sana, kumbe kichwani empty . kuna siku mona nilikaa naye kuzungumza mawili matatu, ndipo nilipoona hamna kitu huyo jamaa!
 
Hamna kitu huyo boya, na miguu yake kama banio! Alafu anajifanyaga anajua sana, kumbe kichwani empty . kuna siku mona nilikaa naye kuzungumza mawili matatu, ndipo nilipoona hamna kitu huyo jamaa!
chuki haipandikizwi wewe boya wewe unaleta stor zako za kimama apa
 
chuki haipandikizwi wewe boya wewe unaleta stor zako za kimama apa
Punguza jazba maalim! Ukitaka kuamini nachokuambia nenda kwenye show zake anazofanya bure uone kama kuna watu, huwa anaimbia viti vitupu!
 
Punguza jazba maalim! Ukitaka kuamini nachokuambia nenda kwenye show zake anazofanya bure uone kama kuna watu, huwa anaimbia viti vitupu!
eti viti vitupu ata ukimuambia mtoto mdogo atahisi una mtindio maana ni kitu kisichowezekana
 
Unajivua nguo bro, Hayo matusi ya nini sasa?
Hamna kitu huyo boya, na miguu yake kama banio! Alafu anajifanyaga anajua sana, kumbe kichwani empty . kuna siku mona nilikaa naye kuzungumza mawili matatu, ndipo nilipoona hamna kitu huyo jamaa!
 
huwa anaimbia viti vitupu!
Hizi ni chuki za wazi, tujifunze ku-appreciate kile kidogo mtu anafanya na kuwatia moyo, kwa maoni yangu pamoja na madhaifu mengine ya kibinadamu ila jamaa anajitahidi sana kusongesha harakati zake, ningeshauri ujaribu kufuatilia hata page zake uone harakati zake.
 
Nashi kama binaadamu wengine tu, mapungufu hayakosekani ila katika harakati za kuuweka utamaduni huu sehemu inayostahili Nashi anafanya mengi makubwa kuliko wakubwa waliopo kwenye mainstream
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…