dawa yenu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 2,825
- 3,675
Naufananisha muziki na bahari kubwa, wavuvi wapo wengi na sokoni kuna samaki wa kila aina kuna samaki wana virutubisho vingi na ni watamu kweli ila hawana soko au labda wanachukuliwa poa na walaji kwa kuwa uuzaji wa samaki hao huwa hauambatani na vioja (kiki) ambavyo kuna wakati vinaweza kuuvua utu wa mvuvi.
Naam, yule mvuvi bora kati ya wavuvi bora tuliojaaliwa Tanzania katuletea samaki wa aina yake mwenye virutubisho vya aina. Anaitwa NASHI MC mimi namuita fundi wa kinasa (kiswahili na sanaa) katuletea mdundo wa maana, mdundo uliotulia, mdundo wa mahadhi ya hip hop.
Wale wazee wa muziki na elimu hapa ndio mahali pake. Tutoe support kwa hawa wasanii wa hip hop asilia maana kazi wanayofanya na wanachokipata hakika havifanani.
Sauti ni wimbo mkali ambao napendekeza tuusikilize wanajf.... Ukihitaji nifuate PM maana hata yeye kasisitiza turushiane ili sote tuupate ujumbe uliokusudiwa.
Hip hop sasa, siku zote na milele.
Amina