Sauti ya umma tumaini iringa.

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
62,197
Reaction score
128,160
Kama ilivyo ada katika uchaguzi mbalimbali wa vyuo vikuu vya hapa nchini umetawaliwa na tofauti za kisiasa, yaani CCM na CHADEMA. Katika chuo cha Tumaini ya mkoani Iringa Jana jumamosi kulikua na uchaguzi wa vuta nikuvute ambapo wagombea walikua wengi ila ushindani ulirindima kati ya kijana mmoja mwanachama wa CCM na mwingine mwanachama wa CHADEMA ambapo ikabadili sura na kuufanya uchaguzi uwe kati ya vyama ivi viwili maarufu hapa nchini.
Kazi ilianza tangu jumatatu ambapo kijana wa CCM alionyesha kuwa na nguvu kubwa kutokana na support kutoka utawala wa chuo na pia alipigwa tafu kiuchumi na kada maarurufu wa CCM wa Iringa almaarufu kama ASAS. Kama kawaida vijana wenye kupenda mabadiliko wakakusanyika, wakautangaza ukweli ukaeleweka kijana wa CHADEMA kutoka faculty ya sheria kwa jina Method Kagoma akaibuka kidedea kwa nguvu ya umma. Ivyo basi Tumaini Iringa ina Rais mwanachama wa CHADEMA.
Peoples Power!!!!!!!!!!
 

siku hizi ukijipamnanua kuwa wewe ni CCM ni sawa na kujitangazia gundu
 
siku hizi ukijipamnanua kuwa wewe ni CCM ni sawa na kujitangazia gundu

Ndugu umenena, linapokuja swala la vijana hasa vyuoni ukijulikana kuwa CCM imekula kwako.

Kwa CCM kuna jambo la kujifunza hapa,vijana hawawataki tena and there is no turning back.
 


Hapo kwenye red - vijana wamkomeshe huyu bwana na kwa kususia Yorgut za Asas. Pata Serengeti instead.
 
Sasa ccm hawana chao kila sehemu. Hata uchaguzi ukifanyika kwenye shule ya chekechea, lazima makundi ya ccm na chadema yaibuke na chadema lazima ishike usukani. Aibu!
 
Bravo wana Tumaini Iringa.
Mmechagua mabadiliko, na ni dalili njema kwa Taifa letu, hasa kwa siku chache zijazo!
Look!...Hundred miles away from Iringa tunafurahia pamoja!
 
This is holy crap.
Hivi hapo mlikuwa mnachagua viongozi wa chuo wenye upeo wa kuongoza au viongozi wa chama? Ningekuelewa kama ungesema tumechagua kiongozi anayetufaa na mwenye uwezo wa kuongoza lakini kusema tumechagua chadema, nathubutu kusema huu ni utahira. Naenda mbali zaidi kuwa ni taahira mpaka huyu mleta maada kwani hawezi kufikiria na kuelewa kuwa walikuwa wanachagua viongozi wa nini. Hawezi kutofautisha viongozi wa wanafunzi na wa siasa. Hata kama kiongozi huyo ni mwanachama na CUF, CCM, Chadema au kinginecho. Hawa ndo graduate wetu watarajiwa kutoka tumaini Iringa. We have a lot to do and a long to go.
 
Taifa lisipo endelezwa na vijana nani mwingine ataliendeleza?hongereni vijana wasomi nyie ndio mtakao wakomboa watanzania kwenye mikono ya manyangau ,wanyonyaji,madikteta sisiemu.big up vijana wasomi.
 

Habari ndiyo hiyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Peoples power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Siwaamini wate mnaoleta taarifa kama hizi,..
kuna jamaa alisema UDOM kashinda mdada na ni mwanachama wa chadema
kumbe wapi,mwanachama wa ccm na alichaguliwa kwa sababu za udini!

So far so good,i wish iwe kweli
 
Siwaamini wate mnaoleta taarifa kama hizi,..
kuna jamaa alisema UDOM kashinda mdada na ni mwanachama wa chadema
kumbe wapi,mwanachama wa ccm na alichaguliwa kwa sababu za udini!

So far so good,i wish iwe kweli
Mkuu naomba uelezee kwa undani kidogo hapo kwenye nyekundu please.
 
There is no turning point in the real freedom of Democracy ni mabadiliko kwa kwenda mbele kila mahali.
Ukipita mitaani hata watoto wa chekechea wanaimba Peoples Power!
The next coming general election CCM wajiandalie kaburi la kujizika wenyewe, kabla hatujawazika kwa nguvu. vijana wenye umri wa miaka 15 leo atakuwa ametimiza haki ya kupiga kura 2015, na katika hili hakuna shaka chadema wataibuka kidedea, vijana wamechoka kunyanyaswa na kuonewa na serikali ya ******. CCM imekuwa mali ya matajiri mafisadi.
HONGERENI SANA TUMAINI IRINGA mmeonyesha njia kwa vyuo vingine kufuata nyayo.

wish you the best, YES CHANGE WE CAN!
 

Katika pitapita zangu nilifika Iringa nanikafanikiwa kushuhudia uchaguzi pale RUAHA UNIVERSITY (RUCO). The so called mkwe wa JK (Asas) alijaribu kurubuni nguvu ya umma ya wanaRUCO kwa kumdhamini mgombea anayeaminika kuwa ni wa CCM, na ilifikia hatua hata ya kuwahonga TANESCO wazime umeme wakati wa kuhesabia kura lakini wadau walishashtukia mchezo na walikuwa na tochi; umeme ulipozima tu wakaziwasha tochi na mwisho wa siku nguvu ya umma ikashinda kwa kishindo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…