Sauti za Wananchi, Vyama Pinzani na Wanaharakati zasikika Tozo za miamala

Sauti za Wananchi, Vyama Pinzani na Wanaharakati zasikika Tozo za miamala

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
520
Reaction score
2,930
Sauti za wananchi zimesikika

Binafsi ninapongeza maamuzi ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala hili. Sioni haja ya watu kugeuka tena kusema mbona Rais huyo huyo alisaini sheria na sasa anatengua? Kwani malalamiko yetu dhidi ya hizi tozo yalikuwa na lengo gani?

Lengo lake ilikuwa kufanyike marekebisho juu ya hizi tozo, Rais amesikia malalamiko hayo wameamua kupitia through kanuni. kwanini tena tuhoji kwanini Rais alisaini!

Mchakato wa Bajeti una mlolongo mkubwa kuanzia kwenye hatua ya kuandaa Budget Guideline by Budget Guideline Committee kupitiwa, kwenda Inter-Ministerial technical Committee (IMTC), kwenda Cabinet Secretariat baadaye kwenda baraza la mawaziri baadaye kwenda Bungeni kusomwa, kujadiliwa katika kamati na kusomwa tena baadaye kupitishwa (Approved) in the house. Baada ya hapo Bajeti hiyo hutungiwa sheria, sheria ya makusanyo na sheria ya matumizi huitwa Annual Finance Act na Annual Appropriation Act.

Sheria inayohusu makusanyo pamoja na makato ya tozo hii ni Annual Finance Act, ambayo Bunge ilipitisha na Rais kuridhia na hupaswa kutengenezewa Kanuni chini ya waziri wa fedha ili kutekelezwa.

Tunapaswa kuelewa mambo kadhaa katika kufanya marekebisho au kubadili maamuzi ya jambo liliopitishwa na serikali kwa wananchi kabla ya kukusanya maoni ya wananchi. Tutambue serikali inaongozwa na viongozi ambao ni watu pia, sio kila maamuzi yanaweza kuwa sahihi muda wote kwa wananchi hata kama yana nia njema. Hivyo serikali huwa inapata picha ya maamuzi yake namna yalivyo na athari kupitia Bunge au umma (public opinions & complaints) yaani wananchi.

Bunge linapaswa kujadili, kukosoa na kuishauri serikali bahati mbaya Bunge tulilo nalo sasa hivi ni eehh Mungu tusaidie. Hivyo Serikali haikuona athari ya maamuzi yake kupitia Bunge, ababu ya aina ya Bunge tulilo nalo sasa.

Serikali imeona athari ya maamuzi yake kupitia malalamiko ya wananchi (public opinions and complaints). Hii ndio maana haswa ya nchi kupaswa kuongozwa kidemokrasia sababu wananchi wawe huru kukosoa, kushauri na kupendekeza dhidi ya maamuzi yenye athari kwao.

Watu wameshauri, wamekosoa na kupendekeza kwa lengo la Serikali kuchukua hatua na marekebisho, ni hatua kubwa na nzuri Serikali kusikia malalamiko ya wananchi na kuyazingatia.
 
Tengeneza tatizo tatua tatizo kisha nenda kajisifu wewe ni Raisi was wanyonge utasikia kina jingalao wakishangilia pumbafu sana CCM
 
Kwa hiyo yeye masuala ya hizi tozo ameyajua baada ya wananchi kulakamika?

Kwamba mpaka mambo yanaingia bungeni alikuwa hajui kitu? Wananchi tumegeuzwa maabara ya majaribio!
 
Poleni kwa kipigo cha jana kule Mbagala, nimemuona mwenzenu anapakiwa kwenye wheelchair, sijui wamemfanyaje kiuno.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Msaliti mwingine huyu.
 
Back
Top Bottom