Sawa, kila la kheri Msigwa ni uamuzi wako na utaheshimiwa ila usiibomowe CHADEMA

Kumbe Zito Kabwe alionewa, zito akampa mkono msigwa akagoma kuupokea.Zito akufukuzwa Bungeni. Maisha ya wanasiasa ni unafiki mtupu
 
Daaaa naona basi kama ni kweli basi Mbowe ni Jasusi hatari sana na alikuwa sahihi kumbania Uchairman wa Kanda,Haiingii akilini kwa Mtu kama Msingwa kujiunga Ccm kwa wakati kama huu.

Huyu Msigwa yumkini hakuhama CHADEMA leo. Atakuwa muda mrefu alikuwa CHADEMA lakini akiitumikia CCM. Bila shaka intelijensia ya huko CHADEMA ilimshtukia ndiyo maana zikafanyika jitihada kuhakikisha anakaa nje ya inner circle ya chama.

Ikumbukwe hata wakati wa marehemu, viongozi wa CHADEMA walipowekwa ndani, marehemu aliamua kumtoa Msigwa, lakini bila shaka, kwa maagizo Msigwa akakataa ili wanaochanga, wachange pesa ya kumtoa, na iliyokuwa imetolewa na ikulu, aitie mfukoni.
 
Yule mbunge wa hoja za ngono Iringa anasemaje
 
Uongozi uliotukuka wa Rais Doctor Samia Suluhu Hassan hata nchi za mbali kama Russia na Norway wameona wafuate uongozi wetu hakika Msigwa inastahili kuingia CCM kujifunza Medani mya za siasa
 
Daaaa naona basi kama ni kweli basi Mbowe ni Jasusi hatari sana na alikuwa sahihi kumbania Uchairman wa Kanda,Haiingii akilini kwa Mtu kama Msingwa kujiunga Ccm kwa wakati kama huu.
Kwa ujumla alichokiongea Msigwa leo inaonyesha ni jinsi gani kuhama kwake hakutakuwa na impact yeyote. Kila kidogo amuingize Lisu chaka.
 
Watanzania tulio wengi hatuna ustaarabu wa kuondoka sehemu tukapaacha salama, lazima tupachafue tu. Ndilo jambo rahisi tunaloweza kufanya. Mambo mengine ya kusema 'tenda wema nenda zako' tunaona haiwezekani. Hatuwezi kuwa positive kwa sehemu tunakotoka/hama. Hata kwa mambo ya ndoa ni hivyo. Wanandoa wakitalakiana/tengana kila mmoja atamwaga siri za mwenzake hadharani, na tunaona na vizuri tu. Kwa nini? Ni kwa sababu akili na mioyo yetu imejaa kinyongo/fitina/hila/chuki. Lakini ni jambo jema kiasi gani kubaki 'positive'! It's very fulfilling! Tujitahidi kila mara kuwa positive - tuondoke sehemu, twende huko tunakokwenda, lakini tusichafue huku tunakotoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…