Wakaguongo
Member
- Sep 23, 2026
- 95
- 38
Lakini kuna swali moja kubwa ambalo linaweza kumfanya mtu asimame kidogo:
Mafuta ghafi yenyewe yatatoka wapi?
Kwa lugha nyepesi, refinery ni kiwanda kinachochukua mafuta ghafi (crude oil) na kuyachakata, yaani kuyasafisha kuwa bidhaa kama petroli, diseli na bidhaa nyingine. Kwa hiyo, kujenga refinery ni upande mmoja wa equation. Upande mwingine ni kupata mafuta ghafi ya kutosha kuiendesha.
Na hapa ndipo mambo yanaanza kuwa 'interesting'. Kenya ina mafuta katika Lokichar Basin, kaunti ya Turkana, lakini uzalishaji wa kibiashara bado haujafikia kiwango ambacho kinaweza peke yake kulisha refinery yenye uwezo wa mapipa 700,000 kwa siku.
Kumekuwepo na ripoti kwamba vyanzo vinavyoweza kuhusika ni pamoja na Kenya, Uganda na South Sudan, lakini kila moja ina changamoto zake za miundombinu na usafirishaji.
Aidha pia kuna wazo la "Lokichar–Lamu Crude Oil Pipeline" yaani bomba la takriban kilomita 824 ambalo lingeunganisha maeneo ya mafuta ya Turkana na Lamu. Rais William Ruto hivi karibuni alisema Serikali inazungumza na Dangote kuhusu kujenga bomba hilo sambamba na refinery. Hata hivyo, bomba hilo haliko tayari na kwa hiyo awamu ya kwanza ya uzalishaji wa mafuta, Kenya italazimika kushikilia mpango wa awali wa kutumia barabara, na baadaye reli, kusafirisha mafuta.
Na hapo ndipo swali linakuwa kubwa zaidi:
Ikiwa refinery inahitaji mamia ya maelfu ya mapipa kila siku, mafuta hayo yatapatikana kwa kiwango gani kutoka Turkana?
Je, Kenya italeta crude oil kutoka Uganda au South Sudan? Au tutategemea meli kuleta mafuta ghafi kutoka masoko ya kimataifa, kisha kuyachakata Lamu?
Ikumbukwe Dangote refinery haijapangwa kuhudumia Kenya pekee. Inatarajiwa kusambaza bidhaa za mafuta katika masoko kadhaa ya Afrika Mashariki, ikiwemo Uganda, Tanzania, South Sudan, Rwanda, Burundi, Ethiopia na DRC.
Kwa hiyo, tunapoangalia shilingi trilioni 2.2, mapipa 700,000 kwa siku, Lamu Port na soko la Afrika Mashariki, kuna sehemu nyingine ya equation ambayo huenda ikawa muhimu zaidi:
Mafuta ghafi ya kuiendesha refinery hii yatatoka wapi? Na je, yatafikaje Lamu?