spidernyoka
JF-Expert Member
- Jan 2, 2020
- 7,557
- 20,477
Unatuchokoza ami yangu🤣milivyomuana hana kisogo nikajua tu huyu anamatatizo ya akili.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unatuchokoza ami yangu🤣milivyomuana hana kisogo nikajua tu huyu anamatatizo ya akili.
hahahahahahakocha wa makombe, kocha wa soka la kasi zitapigwa pasi mpaka msinzie, kocha la bei mbaya
Mimi nashindwa kuelewa. Simba walisema wamesain mkataba na M-BET bil26 sasa wanashindwa nini kutoa mil450 kuvunja mkataba wa manzoki na vipers?sijaona kosa la kocha zaidi ya kumtoa chama, viongozi wa simba ni wapumbafu
huwezi kua na malengo ya kufika nusu final ya caf halafu unashindwa kununua mchezaji kwa tsh 400ml
pumbafu kabisa viongozi wa simba
halafu utalisikia li CEO linaropoka nyooo tunataka kumuuza sakho, pumbafu!
mnaifanya timu ya simba sehemu ya biashara huku mkiwa na malengo ya kufika mbali kwenye caf champions league? pumbafu sana.
Yaani kisa kafungwa na yanga, statistics za ile mechi ziko vipi?Hataufai, hajui mechi zetu, anakurupuka, atatugharimu.
Bora kuziba ufa mapema kabla hatujavunja nyumba.
Nasema No, aondoke
Uliziona wapi hizo pesa?Mimi nashindwa kuelewa. Simba walisema wamesain mkataba na M-BET bil26 sasa wanashindwa nini kutoa mil450 kuvunja mkataba wa manzoki na vipers?
Mkuu usinihamishe🤣🤣🤣🤣🤣Ndivyo urusi itakavyokung'utwa na Ukraine hatimaye[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nimeshasema wake za watu acheni kujadili soka,mnadandia dandia tu hoja bila kujua.Haya maswali huonekana humu jukwaani pale tu simba ikifungwa! Ikishinda, huwezi kuyaona. Mashabiki wa simba mnatakiwa kuwa wavumilivu.
Umeandika ujinga tu na majunguMkuu umeongea Vyema Sana,
Pamoja na Mambo mengine lakin tatizo la Simba ni Matola sema amejificha kweny kivuli cha Ukongwe ili kuwapumbaza watu na Siku wakijakushtuka ni kumekucha,
Bahati mbaya zaidi hakuna wanaoliona kama ni tatizo,
Yanga walishagundua tatizo kama hili linaloitafuna Simba ndo maan Wakaamua kuachana na Watu wa Aina ya Matola kv Mkwasa na Mwambusi.
Simba inabidi wafanye Maamuz Magumu Either wamuondoe Matola ili timu ibaki na Wageni pekee (makocha) au Wawafukuze Wageni (Makocha) ili timu ibaki na Wazawa (Matola na Wenzie) Lakin kuendelea kuleta Wageni ili wafanye kazi na Matola, ni Jinamizi litakolitafuna Simba Kwa Muda mrefu.
Sina kumbukukumbu vizur Msimu ambao Simba alikuwa Unbeaten alifundishwa na Makocha wa namna gani (Wageni wote au Wazawa wote au mzawa na mgeni) nikimaanisha Kocha Mkuu na Msaidizi wake,
Kipind cha Uchebe,pamoja na kwamba timu ilikuwa inafungwa lakin Mpira uliokuwa unachezwa kila mtu alikuwa anauona na hii yote ni baada ya Uchebe kukataa kuletewa Kocha msaidiz mzawa wakati yeye alipendekeza wa kwake ambae Viongozi hawakumtaka, na Uchebe ikabidi apige kazi Mwenyew,
Kipind Simba anafungwa Mbele ya Magufuli, Makocha hawakuwa Wazawa na kila mtu alikuwa anaona Mpira uliokuwa unachezwa kipind hicho na hata hiyo mechi ilikuwa ni Kama Bahati mbaya tu,
Tangu Matola aaminiwe kuwa Kocha msaidiz Mashabiki wa Simba wamekuwa Roho kwatu Simba inapokuwa Inacheza,
Yaan furaha Yao Hadi Mpira uishe kabisa,
Matola na Makocha wa Kigeni hakuna wa Kumtuma Mwenzie (hawaheshimiani),
Matola yeye anajifanya ni Mtoto wa Msimbazi,mkongwe,mzawa nk kitu Ambacho kinawapumbaza Mashabiki,Viongozi,Wanachama na Wakereketwa wa Timu ya Simba kiasi kwamba na yeye anatumia Ka upenyo hakohako kuwagawa baaadhi ya wachezaji na Makocha Kwa Uongozi na kuna wakati anajifanya ameshauri Ila Ushaur wake haujafanyiwa kazi mwisho wa siku Kocha Mkuu ndo anaonekana tatizo Yanga walishagundua yote haya Kwa Kina Mkwasa,
Kuna Tukio flani,Kocha Mmadrido (Pablo) alishawahi kugomea Sub ya Matola na Hadi akawa anapiga viti mateke japo Viongozi waliifumba fumba Tu ili tusijue kinachoendelea kiundani Zaidi,
Pamoja na kwamba hata Pablo Hakuwa Kocha Mzuri lakin Suala la kuingiliwa katika Maamuzi Kwa Sababu Tu ya Uzawa wa Matola sio Suala zuri,
Walikuwa KIMBIJI sio Kigamboni😆Kwa hiyo kambi ya Misri haikua na tija, au! Maana Yanga walichekwa na kukejeliwa humu jukwaani kwa kuweka kambi Avic Town Kigamboni!
Jambo la kushukuru, mashabiki wao tuliwaunga mkono kwa 100%!!!
Kweli kabisa bahati nzuri watu walivyoona kikosi wakanza kutukana, kocha kayasababisha yooteBenchi la ufundi la Simba na zaidi hasa kocha mkuu waastahili kupokea lawama kutoka kwa wanasimba kwa kipigo walichopata jumamosi japo kufungwa ni sehemu ya mchezo. Toka mechi ya St. George ni watu wachache sana tuliona matatizo ya Simba kuzuia kwa pamoja pale adui anapokuwa na mpira na hasa wanaposhambuliwa. Benchi la ufundi linapaswa kutengeneza mfumo wa kujilinda haraka ili timu ijilinde kuanzia mbele wakati wamepoteza mpira
Simba wameachana na Lwanga lakini ni nani aliyebaki pale Simba ambaye analinda beki "four" yake kwa ushahihi? Watu wengi sana nikiwemo mimi tuliwatahdharisha sana tena kwa muda mrefu kuwa wakuti wanaachana na Lwanga kwa sababu waliyosema wao kuwa majeruhi basi Simba wanapaswa kusajili kiungo mkabaji mwenye iwezo wa kuilinda beki "four"yake kwa usahihi. Lakini kilichotokea wamemsajili Akpan ambaye hana tofauti sana na Kanoute. Wote hawa wanawaza kushambulia muda wote hata wakipangwa kiungo cha kukaba lazima utawakuta mbele wanajisahau kuwa wao wanatakiwa muda wote kuwalinda mabeki wao.
Lakini yote kwa yote kocha ana lawama zake binafsi kwa sababu yeye ndio amebeba dhamana ya timu nzima ikiwemo benchi la ufundi.
1. Hivi alifikiria nini kuanza na Mwenda badala ya Kapombe? Mfumo wa Simba ni kushambulia tokea pembeni kwa kupitia mabeki wake. Na Kapombe kazi yake inajulikana na krosi zake zinakuwa na macho na kikubwa zaidi uzoefu kwani ameshacheza mechi nyingi za kimataifa na amekutana na wachezaji wengi wa mataifa mbali mbali.
2. Pia ilikuwaje akaanza na Kyombo badala ya Phiri wakati iliruhusiwa kuchezasha wageni wote? Phiri kasi yake, mashuti yake ya nje ya "box", uzoefu wake, uwezo wake wa kuchambua mabeki wa timu pinzani ukimlionganisha an Kyombo ni kama mbungu na ardhi.
3. Kama kocha tu upangaji wa timu ni changamoto vipi mbinu nyingine za mchezo?
Ni mtizamo tu.
Kila mtu ana mtazamo wake,Umeandika ujinga tu na majungu
Hataufai, hajui mechi zetu, anakurupuka, atatugharimu.
Bora kuziba ufa mapema kabla hatujavunja nyumba.
Nasema No, aondoke