Say no kwa kocha wa Simba

Mimi nashindwa kuelewa. Simba walisema wamesain mkataba na M-BET bil26 sasa wanashindwa nini kutoa mil450 kuvunja mkataba wa manzoki na vipers?
 
Simba hakuna cha kocha hakuna cha wachezaji, simba tumebaki wachabiki tu,

Haji Manara alionekana kwenye hotel simba iliyopiga kambi, huyu bwanamdogo atakuwa 🤯 yaani haiwezekani kufungwa kibwege bwege hivyo , mmmh
 
Benchi la ufundi la Simba na zaidi hasa kocha mkuu waastahili kupokea lawama kutoka kwa wanasimba kwa kipigo walichopata jumamosi japo kufungwa ni sehemu ya mchezo. Toka mechi ya St. George ni watu wachache sana tuliona matatizo ya Simba kuzuia kwa pamoja pale adui anapokuwa na mpira na hasa wanaposhambuliwa. Benchi la ufundi linapaswa kutengeneza mfumo wa kujilinda haraka ili timu ijilinde kuanzia mbele wakati wamepoteza mpira

Simba wameachana na Lwanga lakini ni nani aliyebaki pale Simba ambaye analinda beki "four" yake kwa ushahihi? Watu wengi sana nikiwemo mimi tuliwatahdharisha sana tena kwa muda mrefu kuwa wakuti wanaachana na Lwanga kwa sababu waliyosema wao kuwa majeruhi basi Simba wanapaswa kusajili kiungo mkabaji mwenye iwezo wa kuilinda beki "four"yake kwa usahihi. Lakini kilichotokea wamemsajili Akpan ambaye hana tofauti sana na Kanoute. Wote hawa wanawaza kushambulia muda wote hata wakipangwa kiungo cha kukaba lazima utawakuta mbele wanajisahau kuwa wao wanatakiwa muda wote kuwalinda mabeki wao.

Lakini yote kwa yote kocha ana lawama zake binafsi kwa sababu yeye ndio amebeba dhamana ya timu nzima ikiwemo benchi la ufundi.
1. Hivi alifikiria nini kuanza na Mwenda badala ya Kapombe? Mfumo wa Simba ni kushambulia tokea pembeni kwa kupitia mabeki wake. Na Kapombe kazi yake inajulikana na krosi zake zinakuwa na macho na kikubwa zaidi uzoefu kwani ameshacheza mechi nyingi za kimataifa na amekutana na wachezaji wengi wa mataifa mbali mbali.
2. Pia ilikuwaje akaanza na Kyombo badala ya Phiri wakati iliruhusiwa kuchezasha wageni wote? Phiri kasi yake, mashuti yake ya nje ya "box", uzoefu wake, uwezo wake wa kuchambua mabeki wa timu pinzani ukimlionganisha an Kyombo ni kama mbungu na ardhi.
3. Kama kocha tu upangaji wa timu ni changamoto vipi mbinu nyingine za mchezo?

Ni mtizamo tu.
 
Haya maswali huonekana humu jukwaani pale tu simba ikifungwa! Ikishinda, huwezi kuyaona. Mashabiki wa simba mnatakiwa kuwa wavumilivu.
Nimeshasema wake za watu acheni kujadili soka,mnadandia dandia tu hoja bila kujua.

Kuna watu tulishasema hatutaki kocha mzungu kwa sababu wakiwa na ujinga wao wanao uamini huwezi kuwabadilisha.

Mmeona wenyewe kikosi cha yule mzungu.Umamwachaje Phiri kwa mfano?
Unaachaje kumsajili Manzoki eti kwa uharo wa mtambo feki wa Magoli
 
Umeandika ujinga tu na majungu
 
Zolan ni kocha bora sana, apewe watu sahihi.....
 
Kwa hiyo kambi ya Misri haikua na tija, au! Maana Yanga walichekwa na kukejeliwa humu jukwaani kwa kuweka kambi Avic Town Kigamboni!

Jambo la kushukuru, mashabiki wao tuliwaunga mkono kwa 100%!!!
Walikuwa KIMBIJI sio Kigamboni😆
 
Kweli kabisa bahati nzuri watu walivyoona kikosi wakanza kutukana, kocha kayasababisha yoote
 
Akuna kocha pale yeye pamoja na mtoto wa dadake Dejarn Mdhungu.
 
Umeandika ujinga tu na majungu
Kila mtu ana mtazamo wake,
Mimi nikupige majungu wewe (Matola) kwani ninakula kwako, au nimeajiliwa Simba kama wewe (Matola)?,
Kwa kuwa Simba ni Taasisi ya Watu wengi lazima itasemwa Tu.
Inawezekana nimeandika ujinga kutokana na Fikra zako lakin na Wewe ungeandika welevu wako hapa ili watu waone usivyomjinga
 
Nashukuru kwa kuufanyia kazi ushauri wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…