#COVID19 Sayansi inazidi kutokomeza Corona

#COVID19 Sayansi inazidi kutokomeza Corona

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
3,197
Reaction score
7,677
Taarifa ya WHO inasema kuwa maambukizi ya corona kwa wiki hii pekee yameshuka kwa 16%, na vifo kwa wiki hii pekee vimeshuka kwa 10%.

Tuiangazie Israel kama mfano wa kuigwa.

Israel ni Taifa dogo kwa ukubwa wa eneo la nchi na kwa idadi ya watu. Lakini Taifa hili ni la kwanza Duniani kwa ugunduzi wa Kisayansi. Wagunduzi wengi Duniani ni Waisrael au watu wenye asili ya Israel.

Covid 19 haikuiacha Israel, walipata maambukizi, na wapo waliokufa. Mpaka leo idadi ya walioambukizwa ni 744,513, waliokwishafariki ni 5,526, waliokwishapona ni 693,730, ambao bado wana virusi 45,257, na kati ya hao wenye virusi, ni 872 tu ndio wanaumwa hasa.

Hii ina maana kati ya wote waliopata maambukizi ni 0.7% ndio waliofariki. Wastani wa Dunia ni kwamba katika wote wanaoambukizwa corona, 3.5% hufariki.

Kwa kwa sasa, ni rahisi mara 10 zaidi mtanzania kufariki kwa malaria kuliko mwananchi wa Israel kufariki kwa Corona. Israel kwa sasa imeweza kupunguza vifo kwa 94%. Hii ina maana kuwa kati ya wote wanaoambukizwa corona, wanaofariki hawafiki hata 0.1%, yaani chini ya mtu 1 kati ya watu 1,000 walioambukizwa.

Siri ya Mafanikio

Israel, walijitahidi kuwapima karibia watu wao wote ili kujua ukubwa wa tatizo, na wakati wote wakiwa wanaendelea na majaribio mbalimbali ya management.

Kosa la kwanza la Magufuli ilikuwa kuzuia upimaji. Hilo lilikuwa kosa kubwa sana ambalo hakuna mwansayansi anaweza kulifanya maana huwezi kutambua ukubwa wa tatizo na wala huwezi kuwa na mpango wowote wa kukabiliana na tatizo usilolijua. Hapa Magufuli amethibitisha alisomea Sayansi lakini ameshindwa kuwa mwanasayansi. Sayansi ni data na utafiti.

Walichogundua Waisrael ni kuwa anayewekwa kwenye the Jewish Covid 19 Management Protocil ndani ya siku 5 za mwanzo tangu maambukizi, uwezekano wa kufa ni 0%. Swali kwa Magufuli, hata tukiujua ukweli huu, tutawatambua vipi wenye maambukizi ili waanze kupewa matibabu kabla hawajaanza kuugua?

Utafiti wa Waisrael uligundua kuwa, wenye maambukizi, siku 11 tangu maambukizi kurudi nyuma, hata kama wameanza kuugua, wakiwekwa kwenye the Jewish Covid 19 Anagement Pritocol, uwezekano wa kushindwa kupumua ni 0%, na usiposhindwa kupumua, uwezekano wa kufa kwa Covid 19 ni 0%. Vifo vingi vinawapata walioingia hatua ya kushindwa kupumua, ambayo huanza kutokea siku ya 18 tangu ulipopata maambukizi.

Tufanye Nini
Magufuli inaonekana amekataa kabisa kuwasaidia Watanzania, amewaacha kila mmoja ahangaike kwa utashi wake.

Kwa kuwa Serikali haitaki kuwasaidia wananchi, iziruhusu hospitali binafsi kununua vipimo na kuweza kufanya vipimo kwa wanaotaka. Na wale watakaokuwa positive, hospitali na NGOs ziwafundishe wananchi the Jewish Covid 19 Management Protocol. Hii protocol ni rahisi. Hutahitaji kwenda hospitali wala kumwona daktari. Tutaokoa maisha ya walio wengi.

Jamani tunakufa kwa sababu ya ujinga. Na tukifa kwa ujinga, hata Mungu hatatupokea. Ujinga na upumbavu siyo sehemu ya utakatifu. Mungu hujivunia watu werevu. Mungu ametushirikisha kwenye uumbaji, uponyaji na katika wokovu.

Mbarikiwe sana wana wa Mungu

Note:

Watu wengi wameomba Covid 19 Management Protocol wanayotumia Waisrael. Kwa sasa mataifa mengi wanaitumia, na imeidhinishwa na FDA. Nimeiambatanisha hapa. Nadhani inaeleweka, kama kuna haja ya kuitafsiri kwa Kiswahili, au kama kuna mahali unahitajika ufafanuzi tuelezane.

Shida moja kubwa kwa sasa, dawa hii ya ivermectin imeadimika ghafla, na ukiipata, watu wa pharmacy wameipandisha bei zaidi ya mara 5 ya bei yake ya kawaida. Wauzaji tafadhali kuweni wenye huruma, msishiriki mauaji kwa kuwafanya watu washindwe kuinunua.
Vijana tafuteni dawa hii, wapeni wazee wenu, wanywe kam kinga, msisubiri waugue.

Kwa kinga:

Kunywa 12mg siku ya kwanza, 12mg siku y 3, na 12mg kila baada ya wiki 2. Tutapunguza vifo vingi tukifanya hivyo.

Kwa tiba:

Kunywa 12mg za ivermectin kwa siku 5. Dawa nyingine kama vitamins na doxycyclineni ni za kuongezea ii kuongeza spidi ya uponyaji na kuzuia usiingie kwenye kushindwa kupumua (kama umechelewa kuanza kupata tiba) lakini hiyo ivermectin pekee yake ina uwezo wa kukuponya alimradi usiwe umeingia hatua ya kushindwa kupumua.

Ujumbe huu ubebe baraka za Mungu maana kwa kupitia ujumbe huu nimeshiriki katika kazi ya Mungu ya uponyaji, ambao ni wajibu wa kila aliye na Roho wa Mungu.
 
Attachments

Je, ni nchi gani za Afrika wamewapima wananchi na kujua kiwango cha tatizo
Jifunze kutoka kwa aliyefanikiwa. Dunia siyo Africa pekee. Tungedhamiria tungeweza. Kwanza tulipewa msaada wa zaidi ya bilioni 100 ili kupambana na corona, tungeweza kuitumia hela hii kuwapima watu wetu. Bahati mbaya, tukaitapanya na kupeleka kungine.
 
Unajua ni gharama kiasi gani kufuata huo mlolongo wa sayansi na kuzinatia matokeo yake?
Gharama kubwa ni kwa waliofanya utafiti huo na kutengeneza hiyo management protocol, kucopy hakuna gharama zaidi ya gharama ya kupima na dawa. Na gharama ya dawa ni ndogo sana, wananchi wangeweza kuchangia.

Kwetu sisi isingekuwa lazima kuwapima watu wote, tungefanya tu kwa watu wa mijini na wanaotoka vijiji kwenda mjini maana huko ndiko maambukizi yalikoanzia, hata sasa ndiko kwenye maambukizi makubwa.
 
... ndio maana wapo waliokuwa wanahoji andiko (thesis) la kisayansi la huyu BWANA linapaticana wapi? Andiko la kutunukiwa PhD halijawahi andikwa bila utafiti wa kisayansi. Madai yale ya kuoneshwa andiko hata kama hayajawahi kutekelezwa yalikuwa na bado yana maana nzito sana.
 
Israel yenye watu milioni 9 ilikuwa na maambukizi karibu milion 1 na vifo elfu 5 kama ulivyosema.

Bado hoja yangu iko palepale, kwamba pamoja na ustarabu wote wakujifungia ndani na kuvaa mibarakoa bado covid 19 imewatandika vilivyo.

Hitimisho: hakuna njia yeyote iliyoonesha matunda ya kupunguza corona zaidi ya kuijiondokea yenyewe naturally. Naungana na rais, tusitishane.
 
Zamani watu ulaya waliamini sana utatuzi wa matatizo kwa kumuachia Mungu. Hilo lilifanya kanisa licontrol kila kitu, hasa elimu. Kutumia maiti za wanadamu kujifunza ilikatazwa na kanisa. Sayansi ilikuwa lazima iandane na kanisa.

Baada ya kutokea mlipuko wa homa ya mapafu karne ya 14. Watu walishangaa hata hao wanaohubiri kanisani wanakufa vibaya na hawana msaada wowote. Hapo ndipo watu wakaigeukia sayansi na uchunguzi wa magonjwa na mambo mengine ukashika kasi. Pengine na sisi tutajifunza kutokana na hili, japo kulikuwa hakuna haja ya kupita njia walizopita wenzetu miaka zaidi ya mia saba iliyopita.
2235604_1575881966772.png
 
Gharama kubwa ni kwa waliofanya utafiti huo na kutengeneza hiyo management protocol, kucopy hakuna gharama zaidi ya gharama ya kupima na dawa. Na gharama ya dawa ni ndogo sana, wananchi wangeweza kuchangia.

Kwetu sisi isingekuwa lazima kuwapima watu wote, tungefanya tu kwa watu wa mijini na wanaotoka vijiji kwenda mjini maana huko ndiko maambukizi yalikoanzia, hata sasa ndiko kwenye maambukizi makubwa.
Tz kuna ignorance wengi cha kuustaabisha hata professional wa matibabu wamekuwa foolish
 
Israel yenye watu milioni 9 ilikuwa na maambukizi karibu milion 1 na vifo elfu 5 kama ulivyosema.

Bado hoja yangu iko palepale, kwamba pamoja na ustarabu wote wakujifungia ndani na kuvaa mibarakoa bado covid 19 imewatandika vilivyo.

Hitimisho: hakuna njia yeyote iliyoonesha matunda ya kupunguza corona zaidi ya kuijiondokea yenyewe naturally. Naungana na rais, tusitishane.
Hakuna mahali ambapo corona imeondoka bila jitihada. Mataifa yote yaliyochukua hatua zisizo sahihi yameathirika sana. Angalia Brazil, Sweden, Italy, US, n.k.

Italy na US walichelewa kuchukua hatua. Italy ikachukua hatua madhubuti baada ya kuumizwa vibya, hali ikabadilika. US ilitegemea zaidi hatua za majimbo binafsi. Na kuna tofauti kubwa kati ya jimbo na jimbo kutegemeana na hatua walizochukua.
 
Mkuu kifo ni fumbo akuna awezaye kutegua ama kufahamu atakufa vipi.
Halafu Israel na Tanzania atuwezi kufanana kwa chochote
 
mkuu kifo ni fumbo akuna awezaye kutegua ama kufahamu atakufa vipi.
Alafu Israel na Tanzania atuwezi kufanana kwa chochote
Hatufanani. Ndiyo maana nimesema tungeweza ku-copy. Unakiri tupo chini. Ukiwa chini, na ukajua upo chini, ni wajibu wako kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa/waliokutangulia.

Mbona tunajifanya vichwa nguvu kama vile tunajua kuliko wote? Dalili ya kwanza ya kichaa ni kujifanya bingwa wa kila kitu. Kichaa hutembea katikati ya barabara kwa sababu anaamini ana nguvu kuliko magari yote.
 
Jifunze kutoka kwa aliyefanikiwa. Dunia siyo Africa pekee. Tungedhamiria tungeweza. Kwanza tulipewa msaada wa zaidi ya bilioni 100 ili kupambana na corona, tungeweza kuitumia hela hii kuwapima watu wetu. Bahati mbaya, tukaitapanya na kupeleka kungine.
kwenye kampeni za .... tuka sema tunatumia pesa za ndani...eh!
 
Israel yenye watu milioni 9 ilikuwa na maambukizi karibu milion 1 na vifo elfu 5 kama ulivyosema.

Bado hoja yangu iko palepale, kwamba pamoja na ustarabu wote wakujifungia ndani na kuvaa mibarakoa bado covid 19 imewatandika vilivyo.

Hitimisho: hakuna njia yeyote iliyoonesha matunda ya kupunguza corona zaidi ya kuijiondokea yenyewe naturally. Naungana na rais, tusitishane.
Mimi naungana na wewe,mwaka jana Magufuli kalaumiwa sana mara anaficha corona sijui watu wakufa kimya kimya mara sijui kaamua kuwatoa wananchi wake kafara ila mwishoni wote tukafanya nao kampeni bila tahadhari zozote na sasa wanasema corona ilipungua mwaka jana.
 
Hakuna mahali ambapo corona imeondoka bila jitihada. Mataifa yote yaliyochukua hatua zisizo sahihi yameathirika sana. Angalia Brazil, Sweden, Italy, US, n.k.

Italy na US walichelewa kuchukua hatua. Italy ikachukua hatua madhubuti baada ya kuumizwa vibya, hali ikabadilika. US ilitegemea zaidi hatua za majimbo binafsi. Na kuna tofauti kubwa kati ya jimbo na jimbo kutegemeana na hatua walizochukua.
Maambukizi ya awamu ya kwanza yaliondojaje vile,??
 
Back
Top Bottom