Hakukuwa na data lakini tuliona katika mitaa yetu au miji yetu vifo au wagonjwa mahospital kupungua haya mambo kwa ushuhuda. nakumbuka wakati naenda Hosp fulani wakati shida ndio imekuwa kubwa kulikuwa na ward imetengwa kwa corona sasa tatizo wakati ule hakukuwa na kipimo mgonjwa akija anahisiwa anawekwa kule ilikuwa watu wanakimbiana Hosp ila baada ya hatua kali kuchukuliwa kama kufungwa mashule, michezo, harusi na hatua zingine kama baada ya mwezi Hosp ileile nikwenda tena nilikuta hali fulani ya utulivu na hata vifo mitaani vilipungua sana sasa hiyo kwangu ni mambo yalikuwa yako wazi tunaona, sisemi 100% labda ndio sababu ila kwa mujibu wa wataalamu walikuwa wakitushauri hivyo na kila sababu ya kuamini kuna ukweli.
Tatizo hapa kujiuliza je ungonjwa ulipungua kwa sababu ya kuomba siku 3 kama tunavyoambiwa au zile hatua zilisaidia? kuomba ni imani maana unaomba lakini hujui kama umekubaliwa ni dhana ila vitendo ni bayana unaona.