Sayansi na uchawi !

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,891
Kuna mambo yanatokea huku duniani na pia tunaambiwa kuna watu wanafanya utafiti kuhusu mambo mbali mbali, najiuliza hivi kuna maeneo maalum tu ya kufanyia utafiti au ni kila eneo?

Nauliza swali hilo kwa sababu kuna mambo ambayo yanatokea huku mtaani ambayo yanatia mashaka kabisa kuwa hiki kinachosemwa kukihusi kipo kwa uwazi mkubwa sana

Tumekuwa tukielezwa kuwa sayansi imeshindwa kabisa kuthibitisha uwepo wa uchawi na kwa sababu hiyo basi uchawi umebakia kuwa ni hadithi tena za nchi masikini kama zetu na zaidi sana ni story za kufikirika!

Natilia mashaka kuwa inawezekana hawa wanasayansi wanajua kabisa uwepo wa hii kitu na wanakana kuthibitisha kwa sababu tu unawafaidisha kwa namna moja au nyingine au sayansi ni dhaifu sana kiasi kwamba inashindwa kutoa majibu ya mambo kadhaa yanayotokea kwa uwazi mkubwa

Pia sitaki kuwa mpuuzi wa kudhani kuwa uchawi upo huku Afrika tu na haupo Ulaya kwani pote wanaoishi ni binadamu na kama kuna jambo moja mahali fulani uwezekano wa jambo lile lile kuwepo mahali pengine ni mkubwa kuliko zaidi.

Hebu soma hiki kisa hapa chini halafu uamue mwenyewe

**********************************************

Nilifahamiana na kijana huyu ambae kazi yake ni dereva taxi miaka mitano iliyopita wakati alipokuwa anafanya biashara ya mazao mkoani Shinyanga, aliondoka huko na kuhamia Mwanza kabla ya mimi kuhamia huku, mwaka jana alikuja na kuniambia kuwa baba yake amemtafutia mchumba huko kwao Bariadi na alitaka kwenda kuoa, nilimtakia kila la kheri na aliondoka na jamaa zake wanne kwenda huko kwa ajili ya kuoa.

Harusi ilifanyika vyema na baada ya wiki mbili kijana alikuja na mkewe akiongozana na baba yake pamoja na zawadi kadhaa ambazo alipewa huko harusini, walifika na walikwenda kwenye nyumba ambayo ilikuwa imeandaliwa na kaka yake huyu jamaa yangu kuwa ndio watafikia hapo, kijana alifika na maisha ya ndoa yalianza rasmi.

Baada ya mwezi mmoja baada ya harusi kufungwa mkewe na jamaa yangu alianza kujisikia vibaya, alipelekwa hospitali na kupatiwa vipimo lakini haikuonekana kama alikuwa na maradhi yoyote yale na alirudi nyumbani na kupewa dawa za kupunguza maumivu tu, mkewe aliendelea na hali hiyo kwa muda wa mwezi mmoja na ulipofika mwezi wa 11 mwaka jana hali ilibadilika na kuwa nzuri kiasi.

Jamaa yangu alipata dili la kuwapeleka jamaa fulani huko Kahama kwa gari yake na aliondoka kwa ahadi kuwa atarudi kesho yake, aliondoka na baada ya masaa kadhaa alitujulisha kuwa amefika salama na akasema ataanza safari kesho yake asubuhi ili awahi kurudi kwa kuwa mkewe hakuwa na hali nzuri.

Ilipofika usiku nilipigiwa simu kuwa mke wa jamaa yangu hali yake sio nzuri, niliondoka na kwenda nyumbani kwa jamaa yangu na kumkuta shemeji yangu haongei na alikuwa ametoa macho tu, tulimkimbiza hospital ya mkoa na alipokelewa na alifanyiwa vipimo lakini hakuonekana kama ana tatizo lolote, lakini kila muda unavyokwenda alionekana hali yake inazidi kuwa mbaya, tuliamua kumpeleka Bugando hospital kwa uchunguzi zaidi lakini matokeo yalikuwa yale yale.

Tuliamua kumjulisha baba yake na jamaa yangu nae alikuja pale hospital na kujaribu kutafakari cha kufanya, baba yake na jamaa yangu aliamua kutokumuambia jamaa yangu hali ya mkewe kwa sababu angeweza kuchanganyikiwa na kuamua kuanza safari usiku huo huo kitu ambacho hakikuwa salama kwake, daktari alimuita baba wa jamaa yangu na kumwambia kuwa anapaswa awaze kama mtu mzima kuhusu mgonjwa maana hali haikuwa njema.

Baba yake na jamaa yangu alimuelewa daktari na aliomba alale pale na kupatiwa huduma ya kwanza ili ajaribu kufikiri cha kufanya, shemeji yangu alipatiwa huduma pale japokuwa ilikuwa ni huduma ya kubahatisha tu kwa sababu vipimo vyote havikuonesha kuwa alikuwa anaugua nini, tulimuacha pale hospital na mama yake jamaa yangu na baadae baba yake na jamaa yangu ilibidi ampe taarifa jamaa yangu kuhusu hali ya mkewe, jamaa yangu aliahidi kuondoka alfajiri sana kuwahi ili wajue cha kufanya.

Tulilala na asubuhi na mapema nilifika pale hospital na tulikuwa tunamsubiri jamaa yangu afike ili tujaribu kufikiri cha kufanya, jamaa yangu alifika kwenye saa nne hivi asubuhi na baba yake na jamaa yangu alituambia tuongozane nae na alituambia kuwa hapa hakuna namna nyingine tofauti na kwenda kwa "wataalam", jamaa yangu hakugoma na tuliingia kwenye gari na safari ilianza, nilikuwa kimya tu huku nikiona matokeo ya hili jambo..

Tulifika kwa mtaalam baada ya nusu saa na tulikaribishwa ndani moja kwa moja maana ilionekana kuwa huyu mtaalam alikuwa na taarifa ya ujio wetu, tuliingia na tulikalishwa kwenye viti na mtaalam aliambiwa tatizo la shemeji yangu ambae wakati huo bado alikuwa Bugando, mtaalam alisikiliza na baadae alianza kuchanganya madawa yake pale na baada kama ya dakika tatu hivi alituambia kuwa tusiogope maana "watu" wake wanakuja, nilijisemea kimoyo moyo kuwa ngoja leo nione, aliposema hivyo tulisikia kishindo mule ndani na tukasikia sauti ambayo hatukuona ilipokuwa inatokea na ilikuwa ni ya lugha ambayo sikuielewa na iliongea kwa muda kama wa dakika nne hivi kisha kukawa kimya.

Mtaalam alileta kioo cha kujiangalia na baadae alikimwagia dawa fulani hivi na ghafla kikabadilika na kuwa TV na tulianza kushangaa sana tulipoona harusi yote ilivyofanyika kule kijijini na kila kitu kilichofuatia na tuliona mengi lakini machache ni kwamba nyama ambayo walikula kule harusini haikuwa nyama ya ng'ombe kama wao walivyodhania bali walikula nyama ya tumbili ambao tuliona walivyoandaliwa hadi kupelekwa kwenye harusi na wale ng'ombe waliochinjwa nyama yao ilichukuliwa na wale watu waliochinja wale tumbili...

Baada ya harusi walikaa kikao na kuamua wamuue yule dada ambae ni mke wa jamaa yangu kisa eti amepata mchumba kabla ya dada zake wanne na kiongozi wa kikao kile alikuwa ni mama mkubwa wa mke wa jamaa yangu, baadae tuliona vile jamaa yangu alivyoondoka hadi alipofika na kwenda kwenye nyumba aliyofikia, tuliona mengi sana ila kwa uchache ni hayo, baada ya kuona hayo mtaalam alituambia kuwa mke wa jamaa yangu alilishwa mawe ambayo yanamkaba bila kupata hewa vyema lakini pia alilishwa mjusi [wale mijusi ambao wanakaa sana kwenye majengo mabovu wanakuwa na rangi mbili, pink na rangi ya udongo]

Nilimuona jamaa yangu akistuka sana na mtaalam alituambia kuwa hata sasa tukirudi hospital tutamkuta viganja vya mikono vya mke wa jamaa yangu vimeanza kubadilika na kufanana ngozi ya mijusi wale, nilihisi kijasho kikinitoka na nilisema ngoja nikifika Bugando nitaangalia mikono ya shemeji yangu, baadae mtaalamu alituambia kuwa mke wa jamaa yangu angeendelea na hali hiyo na baada ya wiki mbili angefariki.

Mtaalam alisema kuwa atakwenda na sisi mchana huo na tutakwenda kumtoa hospital na kwenda nae nyumbani kumtibu, baada ya maelezo hayo tuliondoka pale na mtaalam na vifaa vyake na baada ya nusu saa tulikuwa tumefika hospital, tulifanya taratibu zote na tuliondoka na mgonjwa, nilimtazama viganja vyake na kweli niliona vimebadilika kama mtaalam alivyosema, tulifika nyumbani kwa jamaa yangu baada ya dakika ishirini na kazi ilianza...

Mke wa jamaa yangu alinyweshwa maji fulani na alitapika mawe mawili na baadae alitapika mjusi ambae mtaalam alitueleza kabla na cha ajabu mjusi yule alikuwa hai, nilishangaa sana kwa kweli, na baada ya kutapika hayo nilimuona akianza kuhema kawaida tofauti na mwanzo na aliomba maji ya kunywa kitu ambacho hakikutokea mwanzo kabisa, mtaalam aliagiza apewe maji na alipewa na baada ya kunywa alinyanyuka na kukaa kitako pale kitandani, mimi nilikuwa natafakari sana haya mambo huku nikijisemea kuwa huku duniani kuna mambo.

Alipewa dawa nyingine akanywa kisha aliambiwa alale na aamke baada ya saa moja, alifanya hivyo na alipoamka aliomba kwenda kujisaidia haja kubwa na alikwenda na aliporudi alisema kuwa amejisaidia haja kubwa nyeusi kama mkaa na aliogopa sana, kumbuka mtu huyu asubuhi tu alikuwa haongei na wala alikuwa haonekani kama hata anahema na alikuwa ametoa macho tu lakini ghafla baada ya masaa mawili mtu amechangamka utadhani labda alikuwa anaumwa kichwa tu..

Mtaalam alisema vitu alivyojisaidia ni madawa ambayo aliyanywa kwenye maji kule kijijini, baada ya hayo alipewa dawa ya kutumia kwa wiki moja na aliambiwa kuwa atakuwa salama,nilikaa pale hadi jioni na niliaga na kuondoka huku nikistaajabu na kushangaa sana yote yale...

Niliendelea kwenda kumjulia hali shemeji yangu na alipona kabisa na sasa anaendelea na maisha yake na sijui walichofanya kuhusu wale waliowafanyia yote hayo na sikuuliza kabisa..

**************************************************************************************

Sasa hilo ni tukio moja tu, yapo mengi sana na yanastaajabisha na kuonesha kwamba kuna nguvu hii ambayo inadaiwa kuwepo nguvu ambayo ni hasi na inaitwa uchawi, sasa hawa wanasayansi hawayajui haya au wanajidai tu hakuna huku wakijua kabisa upo?

Huo utafiti wao unahusu maeneo gani kama wanasema haya ni hadithi tu? Hivi tukio kama hilo ni hadithi kweli?

Sidhani, hapa naona hii sayansi na wanasayansi wanajua kabisa kuna huu uchawi ila wanaamua tu kukanusha kwa faida yao au hii sayansi ni dhaifu kwa kiasi kikubwa sana maana imeshindwa kutoa majibu kwa mambo yaliyo wazi kama haya.

Wewe unaonaje haya?

Je una uzoefu wowote ambao unaweza kushea nasi hapa?

Kama unao hebu tueleze ili tufikie mahali tukubali mambo mengine hata kama hii sayansi yao inakana au wanajidai kukana.

Hatuwezi kukana mambo yaliyo wazi kama haya!
 
Kuna wabishi watakuja hapa na kudai kama uchawi upo basi warogwe!!!!!!!!!!
:focus:
Binafsi nahisi science inarely sana kwenye physical world rather thanspiritual world.

Uchawi upo na hata madoctor wanajua hivyo ila ethic zao haziruhusu kukubali hiyo kitu. Madoctor wengine wanaongea ukweli, akiona tu ugonjwa hauonekani anakwambia tafuta mganga wa jadi.
 
Aisee umenikumbusha leo nikiwa naelekea kazini nimeskia hayo mambo nikabaki namshangaa huyo muhusika.
Nlikua kwenye gari, gafla akapita mtoto mmoja( mwanafunzi) anaelekea shule.Kwenye gari kulikua kuna walimu wa huyo mtoto wakawa wanaoneshana muone flani hana hata haraka.Mi nikadakia atafika Leo kweli.( kuna kaumbali toka hapo tulipokua hadi shuleni kwao.) Mwalimu mmoja akasema unaeza shangaa unafika unamkuta anafagia.

Ukimuuliza ulipanda gari au boda boda anasema hapana.Kwa kifupi ana sayansi nyingine.
 
Eish!! Kweli tunatofautiana spending such long time typing all these letters; aye aye!!

hongera sana!
 
Mtumishi, ulikuwa unashuhudia ramli ikipigwa!? Haukuweza kufanya maombi!? Hata hivyo una uzoefu wa vitu naikumbuka na ile stori yako ya yule jamaa aliyetembea usiku mzima sehemu fupi kuelekea kwa rafiki yake kwenda kulala baada ya yule mzee kumshindwa pamoja na shemeji yake...

Kesho yake kwenda kufuata vitu vyake walianzisha mbio shemeji yake na yule mzee wakajua jamaa ni wa noma yaani mchawi zaidi, lakini huyo jamaa alionywa na mama yake lakini hakusikia ndio ikaja kumtokea hiyo, nakumbuka kama hicho kisa chako cha kwanza kilitokea maeneo ya Kamanga kama nakumbuka vizuri...
 
sayansi haiwezi kukubali uchawi japo inajua upo; sayansi ina deal na vitu vinavyoonekana; uchawi hauonekani upo more spiritual.
 

Huyo anatembea kwenye dimension ya time
 
Eiyer unaamini nini katika vitu hivi viwili. Binafsi naamini sayansi, uchawi na Mungu pia yupo, vitu hivi vitatu huwezi kuamini kwa masimulizi kama hujashuhudia.
Hey my friend. Do you believe in witchcraft or do you comprehend the existence of witchcraft? Just asking. Nothing personal.

I personal understand the existence of Witchcraft and I can cast out demons and break witchcraft through the Name of Jesus and His blood.

Science to me is part of Christianity since my God created everything in science, inter-alia, science is limited to verificationism of ex nihilos.
 
Vipi unapopiga simu ,waweza kuona jinsi data zinavyoenda??

huoni, the same to electricity; kwasababu uchawi ni spiritual ndo maana sayansi ime ignore na imani pia inahusika hapo!
 
Kama ni wasukuma sishamgai,nilifikili unampigia promo mganga kumbe sivyo.tuwekee namba zake nasi tukapate tiba
 
Eiyer unaamini nini katika vitu hivi viwili. Binafsi naamini sayansi, uchawi na Mungu pia yupo, vitu hivi vitatu huwezi kuamini kwa masimulizi kama hujashuhudia.
Nakubali sayansi ina mchango mkubwa sana kwenye maisha yetu lakini sio vyema kuifanya kuwa ndio last say ya kila jambo!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu kuna mahali Roho Mtakatifu anakuelekeza uwe mtazamaji tu na usifanye kitubna sababu anakuwa nazo mwenyewe

Sikuona ramli pale lakini huyo mganga nae ana namna yake ya tofauti sana ya kufanya mambo

Mkuu nilijifunza mengi kwenye tukio hili na kwanza nilikuwa kama mshuhudiaji tu kwa kweli!
 
Mtumishi umenena vyema sana,ni kweli kabisa sayansi ina limitation kwenye kuverify mambo na kama hili tutaluelewa tutaokoa maisha ya wapendwa wengi sana

Huyu jamaa yangu baada ya tukio hili nilimshauri kwamba aachane na waganga kwani kwa kuendelea kuwatumia anakuwa ni mtumwa na watakuwa wanamchezea tu na kimsingi nguvu iliyotumuka kumdhuru mkewe na iliyotumika kumponya ni ile ile hivyo hakuna uponyaji wa maana na anapaswa kumjua Mungu na kuachana na mambo ya waganga lakini alinicheka sana na kuniambia niache utani

Sikua na jinsi ya kumlazimisha lakini nimemuambia kuna siku atakumbuka kwani huko hakuna uponyaji wa kweli na wa maana

Jamaa haelewe na siku hizi waganga hawaishi nyumbani kwake

Nimeamua kumuangalia tu!
 
Mkuu ni maeneo ya wapi huko kwa mtalaamu?, ulimkubali sana mkuu mpaka ukamuita Mtaalamu, unaona mambo kwenye tv asilia, Vipi hamkupewa masharti!? maana hao jamaa huwa nawajua kwa masharti halafu huwa ni magumu, lakini pamoja na kusema ulishuhudia kuna jamaa wanaweza wakaja hapa wakakwambia thibitisha kama ulithibitisha...

Hivi tofauti ya Illusion na uchawi ni kitu gani!?
 
Mambo hayo yapo kaka! Uchawi upo na unatumika sana katika hiyo sayansi! Wazungu wanao uchawi kama huo! Vodoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…