Sayansi na uchawi !

Sayansi na uchawi !

Uchawi umeshindwa kuthibitishwa kwa phsical, chemical and biological laws. Ndio maana sio sayansi na haiwezi ikawa. Uchawi unaexist in a realm of its own, different from the realm of science. Ila, ukiresearch sana utaona kuwa kuna mahali hizi realms zinakutana. Some things are common in both science and magic.
 
mkuu Eiyer, this is interesting.

nina swali moja....hiyo stori ya kichawi iliyo-narate hapo juu, je mhusika ni wewe mwenyewe au ni jamaa yako aliyekusimulia?
 
Kuna mambo yanatokea huku duniani na pia tunaambiwa kuna watu wanafanya utafiti kuhusu mambo mbali mbali, najiuliza hivi kuna maeneo maalum tu ya kufanyia utafiti au ni kila eneo? Nauliza swali hilo kwa sababu kuna mambo ambayo yanatokea huku mtaani ambayo yanatia mashaka kabisa kuwa hiki kinachosemwa kukihusi kipo kwa uwazi mkubwa sana Tumekuwa tukielezwa kuwa sayansi imeshindwa kabisa kuthibitisha uwepo wa uchawi na kwa sababu hiyo basi uchawi umebakia kuwa ni hadithi tena za nchi masikini kama zetu na zaidi sana ni story za kufikirika! Natilia mashaka kuwa inawezekana hawa wanasayansi wanajua kabisa uwepo wa hii kitu na wanakana kuthibitisha kwa sababu tu unawafaidisha kwa namna moja au nyingine au sayansi ni dhaifu sana kiasi kwamba inashindwa kutoa majibu ya mambo kadhaa yanayotokea kwa uwazi mkubwa Pia sitaki kuwa mpuuzi wa kudhani kuwa uchawi upo huku Afrika tu na haupo Ulaya kwani pote wanaoishi ni binadamu na kama kuna jambo moja mahali fulani uwezekano wa jambo lile lile kuwepo mahali pengine ni mkubwa kuliko zaidi. Hebu soma hiki kisa hapa chini halafu uamue mwenyewe ********************************************** Nilifahamiana na kijana huyu ambae kazi yake ni dereva taxi miaka mitano iliyopita wakati alipokuwa anafanya biashara ya mazao mkoani Shinyanga, aliondoka huko na kuhamia Mwanza kabla ya mimi kuhamia huku, mwaka jana alikuja na kuniambia kuwa baba yake amemtafutia mchumba huko kwao Bariadi na alitaka kwenda kuoa, nilimtakia kila la kheri na aliondoka na jamaa zake wanne kwenda huko kwa ajili ya kuoa... Harusi ilifanyika vyema na baada ya wiki mbili kijana alikuja na mkewe akiongozana na baba yake pamoja na zawadi kadhaa ambazo alipewa huko harusini, walifika na walikwenda kwenye nyumba ambayo ilikuwa imeandaliwa na kaka yake huyu jamaa yangu kuwa ndio watafikia hapo, kijana alifika na maisha ya ndoa yalianza rasmi.. Baada ya mwezi mmoja baada ya harusi kufungwa mkewe na jamaa yangu alianza kujisikia vibaya, alipelekwa hospitali na kupatiwa vipimo lakini haikuonekana kama alikuwa na maradhi yoyote yale na alirudi nyumbani na kupewa dawa za kupunguza maumivu tu, mkewe aliendelea na hali hiyo kwa muda wa mwezi mmoja na ulipofika mwezi wa 11 mwaka jana hali ilibadilika na kuwa nzuri kiasi... Jamaa yangu alipata dili la kuwapeleka jamaa fulani huko Kahama kwa gari yake na aliondoka kwa ahadi kuwa atarudi kesho yake, aliondoka na baada ya masaa kadhaa alitujulisha kuwa amefika salama na akasema ataanza safari kesho yake asubuhi ili awahi kurudi kwa kuwa mkewe hakuwa na hali nzuri... Ilipofika usiku nilipigiwa simu kuwa mke wa jamaa yangu hali yake sio nzuri, niliondoka na kwenda nyumbani kwa jamaa yangu na kumkuta shemeji yangu haongei na alikuwa ametoa macho tu, tulimkimbiza hospital ya mkoa na alipokelewa na alifanyiwa vipimo lakini hakuonekana kama ana tatizo lolote, lakini kila muda unavyokwenda alionekana hali yake inazidi kuwa mbaya, tuliamua kumpeleka Bugando hospital kwa uchunguzi zaidi lakini matokeo yalikuwa yale yale... Tuliamua kumjulisha baba yake na jamaa yangu nae alikuja pale hospital na kujaribu kutafakari cha kufanya, baba yake na jamaa yangu aliamua kutokumuambia jamaa yangu hali ya mkewe kwa sababu angeweza kuchanganyikiwa na kuamua kuanza safari usiku huo huo kitu ambacho hakikuwa salama kwake, daktari alimuita baba wa jamaa yangu na kumwambia kuwa anapaswa awaze kama mtu mzima kuhusu mgonjwa maana hali haikuwa njema... Baba yake na jamaa yangu alimuelewa daktari na aliomba alale pale na kupatiwa huduma ya kwanza ili ajaribu kufikiri cha kufanya, shemeji yangu alipatiwa huduma pale japokuwa ilikuwa ni huduma ya kubahatisha tu kwa sababu vipimo vyote havikuonesha kuwa alikuwa anaugua nini, tulimuacha pale hospital na mama yake jamaa yangu na baadae baba yake na jamaa yangu ilibidi ampe taarifa jamaa yangu kuhusu hali ya mkewe, jamaa yangu aliahidi kuondoka alfajiri sana kuwahi ili wajue cha kufanya.. Tulilala na asubuhi na mapema nilifika pale hospital na tulikuwa tunamsubiri jamaa yangu afike ili tujaribu kufikiri cha kufanya, jamaa yangu alifika kwenye saa nne hivi asubuhi na baba yake na jamaa yangu alituambia tuongozane nae na alituambia kuwa hapa hakuna namna nyingine tofauti na kwenda kwa "wataalam", jamaa yangu hakugoma na tuliingia kwenye gari na safari ilianza, nilikuwa kimya tu huku nikiona matokeo ya hili jambo.. Tulifika kwa mtaalam baada ya nusu saa na tulikaribishwa ndani moja kwa moja maana ilionekana kuwa huyu mtaalam alikuwa na taarifa ya ujio wetu, tuliingia na tulikalishwa kwenye viti na mtaalam aliambiwa tatizo la shemeji yangu ambae wakati huo bado alikuwa Bugando, mtaalam alisikiliza na baadae alianza kuchanganya madawa yake pale na baada kama ya dakika tatu hivi alituambia kuwa tusiogope maana "watu" wake wanakuja, nilijisemea kimoyo moyo kuwa ngoja leo nione, aliposema hivyo tulisikia kishindo mule ndani na tukasikia sauti ambayo hatukuona ilipokuwa inatokea na ilikuwa ni ya lugha ambayo sikuielewa na iliongea kwa muda kama wa dakika nne hivi kisha kukawa kimya... Mtaalam alileta kioo cha kujiangalia na baadae alikimwagia dawa fulani hivi na ghafla kikabadilika na kuwa TV na tulianza kushangaa sana tulipoona harusi yote ilivyofanyika kule kijijini na kila kitu kilichofuatia na tuliona mengi lakini machache ni kwamba nyama ambayo walikula kule harusini haikuwa nyama ya ng'ombe kama wao walivyodhania bali walikula nyama ya tumbili ambao tuliona walivyoandaliwa hadi kupelekwa kwenye harusi na wale ng'ombe waliochinjwa nyama yao ilichukuliwa na wale watu waliochinja wale tumbili... Baada ya harusi walikaa kikao na kuamua wamuue yule dada ambae ni mke wa jamaa yangu kisa eti amepata mchumba kabla ya dada zake wanne na kiongozi wa kikao kile alikuwa ni mama mkubwa wa mke wa jamaa yangu, baadae tuliona vile jamaa yangu alivyoondoka hadi alipofika na kwenda kwenye nyumba aliyofikia, tuliona mengi sana ila kwa uchache ni hayo, baada ya kuona hayo mtaalam alituambia kuwa mke wa jamaa yangu alilishwa mawe ambayo yanamkaba bila kupata hewa vyema lakini pia alilishwa mjusi [wale mijusi ambao wanakaa sana kwenye majengo mabovu wanakuwa na rangi mbili, pink na rangi ya udongo]... Nilimuona jamaa yangu akistuka sana na mtaalam alituambia kuwa hata sasa tukirudi hospital tutamkuta viganja vya mikono vya mke wa jamaa yangu vimeanza kubadilika na kufanana ngozi ya mijusi wale, nilihisi kijasho kikinitoka na nilisema ngoja nikifika Bugando nitaangalia mikono ya shemeji yangu, baadae mtaalamu alituambia kuwa mke wa jamaa yangu angeendelea na hali hiyo na baada ya wiki mbili angefariki... Mtaalam alisema kuwa atakwenda na sisi mchana huo na tutakwenda kumtoa hospital na kwenda nae nyumbani kumtibu, baada ya maelezo hayo tuliondoka pale na mtaalam na vifaa vyake na baada ya nusu saa tulikuwa tumefika hospital, tulifanya taratibu zote na tuliondoka na mgonjwa, nilimtazama viganja vyake na kweli niliona vimebadilika kama mtaalam alivyosema, tulifika nyumbani kwa jamaa yangu baada ya dakika ishirini na kazi ilianza... Mke wa jamaa yangu alinyweshwa maji fulani na alitapika mawe mawili na baadae alitapika mjusi ambae mtaalam alitueleza kabla na cha ajabu mjusi yule alikuwa hai, nilishangaa sana kwa kweli, na baada ya kutapika hayo nilimuona akianza kuhema kawaida tofauti na mwanzo na aliomba maji ya kunywa kitu ambacho hakikutokea mwanzo kabisa, mtaalam aliagiza apewe maji na alipewa na baada ya kunywa alinyanyuka na kukaa kitako pale kitandani, mimi nilikuwa natafakari sana haya mambo huku nikijisemea kuwa huku duniani kuna mambo.... Alipewa dawa nyingine akanywa kisha aliambiwa alale na aamke baada ya saa moja, alifanya hivyo na alipoamka aliomba kwenda kujisaidia haja kubwa na alikwenda na aliporudi alisema kuwa amejisaidia haja kubwa nyeusi kama mkaa na aliogopa sana, kumbuka mtu huyu asubuhi tu alikuwa haongei na wala alikuwa haonekani kama hata anahema na alikuwa ametoa macho tu lakini ghafla baada ya masaa mawili mtu amechangamka utadhani labda alikuwa anaumwa kichwa tu.. Mtaalam alisema vitu alivyojisaidia ni madawa ambayo aliyanywa kwenye maji kule kijijini, baada ya hayo alipewa dawa ya kutumia kwa wiki moja na aliambiwa kuwa atakuwa salama,nilikaa pale hadi jioni na niliaga na kuondoka huku nikistaajabu na kushangaa sana yote yale... Niliendelea kwenda kumjulia hali shemeji yangu na alipona kabisa na sasa anaendelea na maisha yake na sijui walichofanya kuhusu wale waliowafanyia yote hayo na sikuuliza kabisa.. ************************************************************************************** Sasa hilo ni tukio moja tu, yapo mengi sana na yanastaajabisha na kuonesha kwamba kuna nguvu hii ambayo inadaiwa kuwepo nguvu ambayo ni hasi na inaitwa uchawi, sasa hawa wanasayansi hawayajui haya au wanajidai tu hakuna huku wakijua kabisa upo? Huo utafiti wao unahusu maeneo gani kama wanasema haya ni hadithi tu? Hivi tukio kama hilo ni hadithi kweli? Sidhani, hapa naona hii sayansi na wanasayansi wanajua kabisa kuna huu uchawi ila wanaamua tu kukanusha kwa faida yao au hii sayansi ni dhaifu kwa kiasi kikubwa sana maana imeshindwa kutoa majibu kwa mambo yaliyo wazi kama haya. Wewe unaonaje haya? Je una uzoefu wowote ambao unaweza kushea nasi hapa? Kama unao hebu tueleze ili tufikie mahali tukubali mambo mengine hata kama hii sayansi yao inakana au wanajidai kukana. Hatuwezi kukana mambo yaliyo wazi kama haya!
Uchawi upi na vitabu havijafumbia macho.Uchawi ni una missing ktk uongo ,greed, na envy. Utaona wivu ndio motive..then uongo wa kudanganya wengine na kuwawekea vilivyo vibaya kwa vile mchawi anaona kila kitu kilipaswa kuwa chake.Sayansi za kuhundua natural phenomenon zinatoka ktk roho ambapo Mungu Husanya shetani hu imitate ili ili apate abudiwa.Watu wakubwa ktk dunia ya mashetani ,wapagani na hata ktk Sayansi tuijuayo.Walipata clues au complete msg ktk spirit.Mizimu iliwatokea, Malaika au hata wengine walisoma ktk vitab.Akina Newton wote walisoma Biblia. Km Biblia yupo Nabii alihitaji ufunuo kumuua Dinosour .Alihtaji msaada wa kiroho kuweza pata akili na kuwa alihitaji ujasiri tuu asogee hadi karibu sana na yule kiumbe ili atakapofungua mdogo ndipo ampige mkuki kupitia mdomoni ndipo angepata viungo muhimu na sehemu pekee laini.Kwingine nimagamba magumu.Wapo watu wengine kutuliza akili kulitosha kuachia ubongo kutumia uwezo wake uliojificha na kuja na ugunduzi.
 
mkuu Eiyer, this is interesting.

nina swali moja....hiyo stori ya kichawi iliyo-narate hapo juu, je mhusika ni wewe mwenyewe au ni jamaa yako aliyekusimulia?

Sikusimuliwa haya mambo bali nilishuhudia .......!!
 
Uchawi umeshindwa kuthibitishwa kwa phsical, chemical and biological laws. Ndio maana sio sayansi na haiwezi ikawa. Uchawi unaexist in a realm of its own, different from the realm of science. Ila, ukiresearch sana utaona kuwa kuna mahali hizi realms zinakutana. Some things are common in both science and magic.
Ni km kukataa unapoambiwa mtu kaota kwa vile umeshindwa ithibitisha.Utazidi kupata ugumu zaidi utakapohadithiwa ndoto na mtu halafu baadae yakatokea yote.Niliwahi chughudia watu wanaota ndoto mbaya usiku wanalia sanana asubuhi wanapewa taarifa watu wa karibu yao sana wamekufa ,tena saa ileile walikuwa akilia.Niliwahi ona jamaa kamwona binti mzuri kwa mbali, akasema si aje tuu..si muda bint akasimama na kuja kuulizia njia,ktk eneo lile mbel na pembeni kulikuwa na watu wengine wengi wasio wahuni ila aliwaruka na kuja tulipokuwa.sijui km jamaa alikuwa mchawi ila naamini kulikuwa na mind communication.
 
Sikusimuliwa haya mambo bali nilishuhudia .......!!
Watu hawajui kuwa uchawi unaweza kuwa ni matokeo ya sayansi kutumika vibaya, na mara nyingine ni tricks hutumika kufikia matokeo sawa na ya sayansi.All in all mchawi anataka superiority na hivyo hawezi reveal kila kitu kwa vile anataka kuwa ahead ktk huo uchawi.
 
Back
Top Bottom