Natanguliza pole kwa wahanga waliofikwa na maafa ya tetemeko la ardhi lilitokea tarehe 10/9/2016 katika mikoa ya Kagera na mwanza. Kuna mambo napenda kuuliza kwa wanajamvi wenye uelewa kuhusu matetemeko ya ardhi,
1.je kuna mfumo au sayansi inayoweza kugundua viashiria au dalili za kutokea tetemeko la ardhi na kutoa taarifa kabla halijatokea
2.Je kwa nchi yetu ya Tanzania kuna kituo cha kuratibu mateemeko ya ardhi
3.Kwa jiografia ya nchi yetu ni maeneno gani yako katika hatari ya kukumbwa na tetemeko la ardhi?
1: Pamoja na ukuaji mkubwa wa Technologia yenye vifaa vya kisasa kabisa hapa Duniani, hakuna kifaa au hakuna tekinolojia ya kuweza Kupredict kwamba tetemeko litatokea sehemu fulani na kwa muda fulani, watu wanachanganya sana na haya mambo ya kupatwa kwa jua au mwezi na mwisho wa siku wanaona ni kama vitu vinavyofanana kumbe sio
Mzunguko wa Jua, Mwezi na Dunia unajulikana na pia speed ya hivyo vyote inajulikana na kutokana na hivyo wanasayansi wanaweza kujua ni lini vitu hivyo (Dunia, Jua na Mwezi) vitakuwa kwenye mstari mmoja na uelekeo wake yaani sehemu gani huo muelekeo ndio utaonekana at maximum, so Dunia, Jua na Mwezi haviwezi kuwa kwenye mstari mmoja kwa dunia nzima bali ni sehemu tu na kwa Mwaka huu sehemu ya Wangingombe ndio hivyo vitu vilikuwa viko kwenye Mstari mmoja,
Kwa kifupi hakuna kipimo cha kupredict Tetemeko la Ardhi
2: sijui hapo unamaanisha nini, kuratibu kwa maana gani?,
3: East African lift Valley inaanzia Bahari ya Sham na kuishia Mozambique, inaanza kama lift valley moja na ikifika maeneo ya kuanzia Ethiopia, linaanza kugawanyika na kwa hapa Tanzania tunapata pande mbili za lift Valley, Eastern na Western na hizo branch zinaenda kuungangana tena kwenye ziwa Nyasa na zinaingia Mozambique kama rift valley moja
Kwa branch ya Eastern Mikoa inayokuwa na Matetemeko ni Arusha, Dodoma, Singida, Morogoro (kidogo) kisha lift valley ianenda kuungana na Western branch, Branch ya Western ina Mikoa ya Kagera, Kigoma, Rukwa, Katavi, Mbeya na kisha inaingia Nyasa
Vitu kama Lake Tanganyika, Lake Nyasa, safu za Milima (Kitonga, Senkeke), Mt. Kilimanjaro, Meru, Oldonyo Lengai, Ngorongoro Crater ni evidence za hizo lift Valley
Ziwa Victoria mpaka sasa halijathibitishwa kuwa lina uhusiano wowote na lift Valley