CHIPESI NAMISUKU
Member
- Oct 7, 2019
- 51
- 157
Mojawapo ya makosa makubwa ya Kampeni na uchaguzi duniani Kote Ni kumu-Underestimate opponent wako. Hili kosa huwa halifanyiki kwenye Siasa tu hata kwenye michezo na kwenye medani za kivita Ni kosa kuu Kati ya makosa makubwa yanayotajwa.
Kuelekea October kila mwana CCM anayezungumza anasema kuwa tunaenda kushinda kwa asilimia zaidi ya 90 lakini kabla ya kujipa Ushindi huo mkubwa namna hiyo TUWEKEZE kwenye kuomba kura zaidi kwa Sasa.
Twende sawa
Waliomchagua Rais Magufuli 2015 walikuwa jumla ya watanzania 8,882,935 (milioni nane, laki nane na Themanini na mbili elfu, mia Tisa thelathini na tano)
Wakiomchagua mpinzani wake Mkuu ambaye ni Edward Lowassa walikuwa 6,072,848( milioni sita sabini na mbili elfu mia nane arobaini na nane)
Ukitafuta tofauti ya Kura hizi yaani ukifanya hesabu za kutoa utapata tofauti ya kura 2,807,087 yaani JPM alimzidi Lowassa kwa kura Million Mbili na laki nane plus.
UCHAGUZI WA 2020
Tukitumia muundo mpya wa CCM ni kwamba CCM ina jumla ya mashina 222,230 na kila Shina lina jumla ya wanachama 50 hivyo ukizidisha jumla ya mashina na jumla ya wanachama kwa kila shina utapata jumla ya wana CCM 11,111,500 hii ni idadi ya wanaccm wote nchi nzima.
Jumla ya waliojiandikisha kupiga kura hadi kufikia 2018 walikuwa wapiga kura 23,161,440. Takwimu za karibuni Sina zinaweza kuongezeka lakini tutumie tu hizi hizi za mwaka 2018. Katika jumla hii ya wapiga kura ukitoa hapo wanaccm wote unabakiwa na wapiga kura ambao si wanachama wa CCM 12,049,940. Idadi hii ambayo si wanaCCM ni kubwa kuliko wanaccm wenyewe.
KAZI MBILI ZILIZOPO MBELE YA CCM
Ya kwanza ni kulinda Kura za wanachama wake wote yaani isipotee hata moja. Kazi ya Pili ni kujenga ushawishi kwa ambao sio wanachama ili kujazia kura za wanachama wa CCM na tuibuke kidedea tena.
Sijui kama naeleweka hebu sikiliza
Sensa ya mwaka 2012 inatuambia kwa statistics kwamba idadi kubwa ya watu waliopo Tanzania ni watoto na vijana. Watoto ni asilimia 44 huku vijana wakiwa asilimia 35. Ikumbukwe kuwa watoto ni vijana wa Kesho. Hadi kufikia mwaka 2012 Takwimu za sensa zilikuwa zinaeleza kuwa kwa kila watu 10 wa Tanzania, wanne ni vijana ambao umri wao ni kati ya miaka 15 na 35. Hao sita wengine waliobakia ni Watoto na watu wazima.
Takwimu hizi zinaoana na waliojitokeza kujiandisha kupiga kura mwaka 2015 ambapo vijana kati miaka 18-35 waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 12,894,576 sawa na asilimia 57 ya wapiga kura wote. Yaani vijana walikuwa Ni asilimia 57 ya Wapiga Kura wote 2015.Japokuwa kwa takwimu hizi zinatuonyesha kuwa kuna vijana wengi sana ambao hawakujiandikisha kupiga kura kutokana na sababu mbalimbali.
Kama vijana wote watajiandikisha kupiga Kura 2020 basi idadi ya wapiga kura vijana inaweza kuwa asilimia 70 na zaidi, asilimia hizi zinaonekana kuongezeka kutokana na kundi kubwa la watoto wanaoingia kundi la vijana.
TAFSIRI YAKE NI NINI?
Tafsiri yake ni Moja tu kuwa atakayefanya siasa na Kundi hili la vijana ndiye atakayekuwa na wapiga kura wengi 2020.
Utafiti wa Mwaka 2016 wa Twaweza ulionyesha Mwelekeo mzuri wa Kukubalika kwa Vyama vya upinzani kutoka kwenye Kundi hili la vijana. Hivyo hili ndio Kundi linalopaswa kupiganiwa na kila chama ili Kujihakikishia Ushindi wa 2020.
Kundi hili Kubwa ni wamachinga, vijana waliomaliza vyuo na waliopo vyuoni huku wengine wakiwa madarasa ya juu ya shule za Sekondari. Kwa CCM wajiangalie wamewagusa kundi hili kiasi gani na kwenye ilani yetu ijayo tumewagusa kiasi gani.
Hitaji la kundi hili la muhimu ni ajira, wasomi wa vyuo wameongezeka mno mtaani, huyu hata umwimbie nini hatoweza kukusikia Kama hujamwonyesha Mpango wa ajira.
Kundi hili pia litaathiri Kampeni kwa kuwa limeathiriwa sana na ukuaji wa sayansi na technologia, na ndio mfumo rahisi wa mawasiliano kwa sasa nafikiri tunaelewana hapa. Hawa wakikusaidia kwenye Kampeni hupati shida sana kujinadi.
Tuendelee kuomba kura kwa Nguvu, tuendelee kutengeneza mipango, tuendelee kuchambua Sera zetu, tuendelee kuwavuta vijana toka walipo.
Kidumu chama Cha Mapinduzi, Kidumu chama tawala.