Sayyid Salim Omar L' Attas

Sayyid Salim Omar L' Attas

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SAYYID SALIM OMAR L’ATTAS

Nina kawaida kila ninapopata taarifa za historia za watu ambao jamaa zao wapo hai huwa nawapelekea ili ikiwa wana jambo ambalo mimi silijui wapate kunifahamisha na hii inanisaidia katika kuwa na historia iliyokamilika na ya uhakika.

Kuna masahihisho katika picha niliyopata kutoka kwa Sheikh Saleh Attas ambayo nitayaweka hapa In Shaa Allah lakini kabla napenda nieleze imekuwaje hadi tukafika kwa Sayyid Omar L’ Attas.

Nimeweka mtandaoni barua ya tarehe 16 June 1945 kutoka kwa Al Jamiyyatul Islamiyya Fi Tanganyika (The Muslim Association of Tanganyika) iliyoandikwa na Hon. Secretary Mwalimu Adam Issa kwenda kwa Mzee Rajabu, Machame, Moshi.

Katika barua hii inamuonyesha Sayyid Salim Omar L’Attas kama Patron wa Al Jamiyyatul Islamiyya.

Barua hii inampa habari Mzee Rajabu kuhusu safari ya Sheikh Hassan bin Ameir Machame.

Ni nani Mzee Rajab?

Jina lake kamili ni Rajab Ibrahim Kirama (1843 – 1962).

Historia ya Rajabu Kirama haijaandikwa na umuhimu wake ni kuwa yeye ndiye aliyepandisha bendera ya Uislam Machame Nkuu katika miaka ya 1930 na kutoka hapo Uislam ukaenea Kilimanjaro yote na kusambaa hadi Upare.

Mzee Rajabu kama alivyojulikana alisaidia kujenga misikiti, madrasa na shule za Kiislam.

Historia yake na misukosuko aliyopata inasisimua kuisikiliza na kutafiti.

Naweka barua moja katika nyaraka zake nyingi ambazo sasa zina umri wa miaka 90 na hakuna mtafiti yeyote ambae amepata kuzipitia kabla.

Hapo ndipo utakapoliona jina la Patron wa Al Jamiatul Islamiyya Sayyid Salim Omar L' Attas.

Tuje kwa ukoo wa L’Attas.

Ukoo wa L’Attas una historia kama hiyo hapo juu kuwa walipata kuwa viongozi wa Waislam wa Tanganyika na hapa ndipo historia hii ya Sayyid Omar L’ Attas inapokutana na historia ya Mzee Rajabu.

Lakini katika miaka hii ya karibuni historia ya mmoja katika ukoo huu wa L’Attas, Shariff Abdallah Omar L’ Attas imekuja kuwa maarufu na kusomwa na watu wengi pale ilipokuja kufahamika kuwa Shariff L’ Attas alikuwa mtu wa karibu sana na Julius Nyerere alipofika Dar es Salaam 1952.

Historia ya Shariff L’Attas ilipoandikwa ikawa imeongeza mengi katika historia ya Baba wa Taifa ambayo ilikuwa haifahamiki na wengi.

SHARIFF ABDALLAH ATTAS.jpg

Shariff Abdallah Omar L'Attas katika ujana wake 1950s akifanya kazi Soko la Kariakoo

RAJAB IBRAHIM KIRAMA (1833 - 1961).jpeg

Mzee Rajabu Ibrahim Kirama

BARUA MWALIMU ADAM ISSA KWA RAJAB KIRAMA 1945.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu jaribu kumtafuta Abdullaleem El Attas anaishi Abu Dhabi unaweza kupata mengi huko anaongea kiswahili safi kabisa aliwahi kuwa makerting manager kampuni ya kuuza landrovers Tanganyika miaka ya mwanzoni ya 70.
 
Back
Top Bottom