Scandals na matukio ya mastaa yaliyovunja rekodi 2014..

Scandals na matukio ya mastaa yaliyovunja rekodi 2014..

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Ikiwa tumebakiza miezi mitano tu tumalize mwaka huu 2014, scandals na matukio makubwa mbali mbali ya kufuraisha na kuhuzinisha yametokea kwa baadhi ya mastaa wa fani tofauti tofauti apa nchini, scandals na matukio hayo ambayo yamekuwa gumzo na kuongelewa na watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi kwa mwaka huu wa 2014. baadhi ya matukio na scandals zilizovunja rekodi mwaka huu ni.

1.DIAMOND NA USHINDI WA TUZO 7.

Mwaka huu 2014 unaweza kuwa mwaka wa neema kama sio baraka kwa mwanamuziki wa bongo fleva diamond platnums, neema hiyo ilianza mapema miezi michache iliyopita baada ya mwanamuziki huyo maarufu kujishindia tuzo saba za ktma mfululizo na kufanikiwa kuvunja rekodi ya kuwa msanii pekee nchini kuweza kupata tuzo 7 kwenye vipengere vyote saba alizokuwa akiwania.
Mbali na tuzo hizo msanii huyo asiyekuwa na mpinzani kwa sasa alibahatika pia kuchaguliwa kwenye tuzo kubwa za heshima duniani kama BET na MTV ambazo alikuwa akishindania na wasanii wakubwa duniani.

2. UGOMVI WA WEMA NA KAJALA

Mwaka huu unaweza kuwa mbaya kwa mastaa maarufu wa filamu nchini, wema sepetu pamoja na aliyekuwa rafiki yake kajala masanja baada ya ugomvi mkubwa kutokea kati yao, chanzo kikidaiwa kuwa ni mwanaume, ugomvi huo ulifikia pabaya zaidi baada ya mashabiki wa wema kumtukana kajala pamoja na mwanae matusi makali ya nguoni na kumfanya kajala akose raha kwa miezi kadhaa, ugomvi huo ulifikia pabaya zaidi baada ya watu wasiojulikana kutengeneza picha za uchi za mama mzazi wa wema na kuzisambaza mitandaoni. Hata hivyo bifu hilo linadaiwa kuisha kwa sasa.

3.UGOMVI WA FLORAH MBASHA NA MUMEWE.

Huu unaweza kuwa mwaka mbaya kwa wanandoa na mastaa wa nyimbo za injili nchini, baada ya mdudu mbaya kuingilia ndoa yao na kuleta mtafaruku mzito. hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya mume wa florah kukumbwa na kashfa ya kubaka hali iliyoleta aibu kwa familia pamoja na mkewe kushutumiwa kutoka kimapenzi na mtumishi wa mungu gwajima, scandal hii imeongelewa zaidi na kuwafanya wanandoa hao kuwa maarufu zaidi, hata hivyo inadaiwa wanandoa hao wapo kwenye mchakato wa kuifufua ndoa yao.

4. VIFO VYA WASANII BONGO MOVIE
Mwaka huu unaweza usisahaulike kwa mastaa wa filamu nchini, kwani wamepoteza baadhi ya wasanii wenzao kwa mpigo tena ndani ya mda mfupi hali iiyozua hofu kwa baadhi ya wasanii. Baadhi ya mastaa waliopoteza maisha ni director maarufu nchini Adam kuambiana, George Tyson, recho haule pamoja na aliyekuwa mchekeshaji maarufu nchini mzee small.

5. NDOA YA VICKY KAMATA KUOTA MBAWA

Mbunge na mwanamuziki maarufu nchini, vicky kamata alipata aibu ya aina yake kama sio fedheha baada ya ndoa yake iliyoandaliwa kwa gharama na mbwembwe zote kuota mbawa, mbunge huyo alipata aibu ya mwaka baada ya aliyekuwa mchumba wake kumtapeli hali iliyomfanya alazwe hospital kwa mshtuko na aibu. Hii scandal ilivunja rekodi kwa kuongelewa na watu wengi zaidi kwa mwaka huu 2014.

6.PICHA CHAFU ZA MBUNGE KOMBA

Mbunge na mwanamuziki maarufu , john komba aliingia kwenye aibu ya aina yake baada ya picha zake akifanya uchafu kusambaa mitandaoni, hata hivyo mbunge huyo mwenye kitambi cha haja alikana picha izo kuwa si za kwake na kusema ni wabaya wake wanamchafua kisiasa.

7.NDOA YA 3 YA DIDA KUDAIWA KUVUNJIKA

Mtangazaji na mshereheshaji maarufu apa nchini, dida wa edzeni ameingia kwenye orodha ya mastaa waliokumbwa na mabalaa kwa mwaka huu 2014, baada ya ndoa yake ya tatu kudaiwa kuvunjika kisa kikiwa ni usaliti wa mumewe na vipigo anavyovipata kwa mumewe huyo serengeti boy ,hali iliyomfanya mtangazaji huyo kudai talaka kwa mumewe huyo.

8.UGOMVI WA CHUCHU,MAINDA NA JOHARI

Mwaka huu unaweza kuwa mbaya kwa msanii mkongwe maarufu nchini blandina chagula maarufu kama johari baada ya aliyekuwa my number one wake kuchukuliwa na msanii mwenzie wa filamu chuchu hans, hali iliyozua timbwili na kumfanya johari atoe dozi ya maana kwa mke mwenzie huyo. mainda nae aliingia kwenye mkumbo baada ya kuropoka kuwa aliwahi kuwa na mahusiano na ray na kutoa mimba yake na kufichua mahusiano ya johari na chuchu ambayo yaliyokuwa yamefichwa kwa mda mrefu na kuwafanya wote watatu kuingia kwenye ugomvi. Ni moja ya matukio yaliyozungumzwa sana kwa mwaka huu 2014.

9.PENZI LA SHILOLE NA MZIWANDA.

Msanii maarufu wa muziki wa mduara nchini, shilole mohamed ameingia kwenye penzi zito na kijana anayedaiwa kuwa ni serengeti boy anayejulikana na kwa jina la nuhu mziwanda, penzi lao hilo lilizua gumzo baada ya kijana huyo kujichora tattoo isiyofutika yenye jina la sugar mami wake huyo, ishu hiyo ilizua gumzo kwenye mitandao na wengi walimponda kijana huyo kuchukua uamuzi wake huo ambao wengi wanadai ni wa hatari.
 
Mbona hujaweka ya uwoya na serengeti wake msami?????
 
Wema kunyang'anywa vifaa vyaaa ofisini na nyumba ya milion 400 kumbe sio yakee teh teh hua siisahau hiiii
 
Jamani nimeona IG diamond kapata nominations katika tuzo nyingine tena
 
Wema kunyang'anywa vifaa vyaaa ofisini na nyumba ya milion 400 kumbe sio yakee teh teh hua siisahau hiiii

Eeeh binamu nikikumbuka hilo neno mil 400 nacheka sana mmh yan mama ubaya huyu kawafanya wabongo wote hamnazo, sasa ivi kafulia anamilik s5 ivi
 
Bado muvi inaendelea binamu ngoja tuzidi kusubiri

Tusubir mwenzangu matukio ya kufa mtu, ila mimi tukio ninalolisubir kwa hamu ni ndoa ya ndomo na mama ubaya, maana walisema mwaka hauishi lazima wafunge pingu
 
Nimependa ulivyomwelezea Almasi 'MSANII HASIYE NA MSHINDANI KWA SASA' nashukuru leo u team ana.con.da umeuweka kando.
 
Super star domo alipokwenda kupokea tuzo na ka sketi
 
Nimependa ulivyomwelezea Almasi 'MSANII HASIYE NA MSHINDANI KWA SASA' nashukuru leo u team ana.con.da umeuweka kando.

siwezi kuingiza chuki zangu binafsi kwenye hii makala , hayo ni mambo yangu binafsi, binamu mimi sinaga upendeleo boss wangu mwenyew jide aka cheusi dawa akivuruga tunamchana japokuwa siwezi kuficha mahaba yangu kwake
 
3.jpg
 
Diamond kuvaa Sketi wakati akipokea tuzo zake za Kili.
 
Eeeh binamu nikikumbuka hilo neno mil 400 nacheka sana mmh yan mama ubaya huyu kawafanya wabongo wote hamnazo, sasa ivi kafulia anamilik s5 ivi

Mi mbavu sinaa milioni 400 watu oooi ana pesaaa chafuuu kumbe uharo tu
 
clemenc ila alimkomesha utamuu akatia"baby yangu kasema ataninunulia ndani ya wiki mbili"llloh!kwa diomond ganii.....?????wema umefulia umebaki usupastaaa wa magazetini!
 
Back
Top Bottom