Torque ni maximum angular force available
Horse power ni maximum Power ya engine
Katika malori tuna msemo use torque and not power to haul, Maana kuwa ukitaka kubeba mizigo tumia uwezo wa engine na sio mabavu ya engine
Ki uhalisia diesel engine huwa Inatoa maximum torque katika engine revoliutions ndogo Sana up to 1400 rpm Maxx, yaan ikizid 1400 rpm, torque hupungua na power kuongezeka kadiri ya mizunguko, hii ndo sababu katika mchezo ya spinning diesel engine haziwezi sababu huwa torque unapatikana mwanzo tu, unlike petrol cars, ambazo torque hupatikana kadiri unavoitafuta power,
hii pia ndio imepelekea malori kuwa na gear nyingi( 12 Scania, daf iveco up to 16.) lengo ni kuwa dereva aweza ku negotiate speed bila Kutoka kwenye max torque range, malori yangekua na gear tano kwa mfano, yasinge kuwa economical, sababu muda mwingi dereva angekuwa anaendesha kwa kufata power na si torque
Mfano tuchukulie Volvo ya gear 16. Volvo nyingi max torque huwa ni 1300 rpm, Dereva a naweka namba Moja, na kuvuta moto hadi 1300 rpm, kwa muda huo speed inakuwa may be 6km/h, , akiweka namba mbili rpm itashuka had 700rpm, anavuta Tena moto had 1300rpm kwa muda huo speed inakuwa may be 13km/h, sequence ni hiyo mpaka Lori linapata speed ya kutosha bila Kutoka nje ya 1300 rpm.