hilo kulileta tz itabidi upewe kibali cha tanroads ili litumie barabara za tz alafu watataka hiyo axle ya kati kutoka tairi ya mbele itolewe maana hawaruhusu mabasi ya 6x3 wanaruhusu 4x2 na 6x2 bas na kwa huo urefu ujiandae kulipa faini kila likizidi mzani maana hapo kwa muonekano linazidi mita 12.5 ambazo wanataka wao tanroads hilo linachezea mita 13 au 13.5 na kwakuwa ni injini nyuma litakusumbua sana likipewa safari ndefu madreva wengi wa hapa kwetu huwa hawapo makini na ufatiliaji wa mifumo ya upozaji hasa katika magari yenye injini nyuma ndio maaana asilimia kubwa ya magari tunayotumia ni injini mbele