Scheduled Maintenance

Scheduled Maintenance

Invisible

JF Admin
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,286
Reaction score
8,380
Heshima zenu wana JF!

Kuanzia kesho tunatarajia kuwa na marekebisho "Makubwa" ya JF ikiwa ni pamoja na mabadiliko kadhaa kwa ufanisi zaidi wa majukwaa yetu.

Tunaweza kwenda "offline" kwa muda wa masaa 6 hadi 12 kwa siku ya Jumamosi ama Jumapili ili kuweza kupitia posts zote na topic zote na kuweza kuzipangilia katika mpangilio sawa.

Tunatambua ugumu wa kazi hii na tunaomba uvumilivu wakati wa week end hii ili kuweza kuweka majukwaa yetu katika hali nzuri.

Juma lijalo tutakuwa na matengenezo mengine ambapo tutakuwa tunahamisha baadhi ya data za JF kuelekea kwenye servers zetu nyingine tatu ili kuweza kuongeza loading speed ya JF ikiwa ni pamoja na mirroring ya JF kwa servers zetu za Tanzania ili kuwasaidia wanachama wetu walio Tanzania kuipata JF kwa speed nzuri zaidi.

Once again, kazi hii itakuwa ngumu na itahitaji umakini mkubwa katika kuitekeleza, tunaweza kufanya kila kitu JF ikiwa inaendelea na mijadala lakini haipendezi wakati wa maintenances kadhaa kuiacha on kwani baadhi ya watu watakereka.

Tunawashukuru kwa ushirikiano na tunaomba uvumilivu wakati wa kazi hii ngumu tunayotarajia kukumbana nayo.

Sikitiko langu: Kuna baadhi ya posts zitaondoshwa wakti wa mapitio ya majukwaa yote na hasa zile ambazo zitaonekana hazina manufaa kwa jamii yetu.

Ahsanteni
 
Mkuu tumekupata,Tunakutakia kila la kheri,Ukielemewa usisite kuhitaji msaada wetu TUPO PAMOJA.
 
Sikitiko langu: Kuna baadhi ya posts zitaondoshwa wakti wa mapitio ya majukwaa yote na hasa zile ambazo zitaonekana hazina manufaa kwa jamii yetu.

Mkuu Invisible, hakuna haja ya kusikitika kama unaona posts hazina manufaa kwa jamii yetu. Ila sijui utatumia vigezo gani kulifikia hilo?. NAWATAKIENI KAZI NJEMA KATIKA KUIBORESHA JF.
 
Ahsante mkuu, kulifikia hilo itatubidi kumwomba Mwenyezi Mungu atupe hekima ya kung'amua kipi chema kwa jamii yetu na kipi hakifai.

Nina imani baada ya kupitia kila kitu na kukiweka sawa wadau wengi (si wote) watakubaliana nasi kuwa kazi itakayokuwa imefanyika imefanyika kwa busara kubwa. Kwa uweza wa Mungu tutafanikisha mkuu.

Ahsante kwa wishes
 
Sikitiko langu: Kuna baadhi ya posts zitaondoshwa wakti wa mapitio ya majukwaa yote na hasa zile ambazo zitaonekana hazina manufaa kwa jamii yetu.

Ahsanteni
Kazi njema mkuu......maslahi ya taifa mbele....
 
Mkuu Invisible, hakuna haja ya kusikitika kama unaona posts hazina manufaa kwa jamii yetu. Ila sijui utatumia vigezo gani kulifikia hilo?. NAWATAKIENI KAZI NJEMA KATIKA KUIBORESHA JF.

Ndugu Mfumwa, unaonaje kwa wale ambao tuna kihelehele cha kutuma post wakati hatuchaangii ndio kikawa kigezo namba moja? Kazi njema Invisible
 
KILA LA KHERI BABA! tunakutakia ufanisi mwema EEH BABA?!
 
Mkuu invisible, nawatakia kila la heri kwenye hiyo kazi ngumu. Naamini Busara na hekima za kimungu zitawaongoza ktk utekelezaji wa hilo zoezi GUMU kwa manufaa ya jamii yetu ya Tanzania.
 
Thank you Mkuu Invisible and all Administration crews. Naamini ulipumzika vema juzi na sasa una nguvu tele na moral juu. Mungu aendelee kukupa nguvu na moyo wa kuitumikia Tanzania kupitia JF na nyinginezo. At least wale ambao wanashinda JF week ends watapata nafasi nzuri kwa couples wao or marafiki na kids (kama wapo)!!!! All the best!
 
Mkuu Invisible, Nakutakieni kila la heri katika kazi hiyo nzito. Mungu akujazeni hekima na busara katika utekelezaji wa kazi hiyo. Nina imani, baada ya maboresho hayo JF itakuwa "The Best Home of Great Thinkers". Idumu JF na wawezeshaji wake!
 
Heshima zenu wana JF!

Kuanzia kesho tunatarajia kuwa na marekebisho "Makubwa" ya JF ikiwa ni pamoja na mabadiliko kadhaa kwa ufanisi zaidi wa majukwaa yetu.

Tunaweza kwenda "offline" kwa muda wa masaa 6 hadi 12 kwa siku ya Jumamosi ama Jumapili ili kuweza kupitia posts zote na topic zote na kuweza kuzipangilia katika mpangilio sawa.

Tunatambua ugumu wa kazi hii na tunaomba uvumilivu wakati wa week end hii ili kuweza kuweka majukwaa yetu katika hali nzuri.

Juma lijalo tutakuwa na matengenezo mengine ambapo tutakuwa tunahamisha baadhi ya data za JF kuelekea kwenye servers zetu nyingine tatu ili kuweza kuongeza loading speed ya JF ikiwa ni pamoja na mirroring ya JF kwa servers zetu za Tanzania ili kuwasaidia wanachama wetu walio Tanzania kuipata JF kwa speed nzuri zaidi.

Once again, kazi hii itakuwa ngumu na itahitaji umakini mkubwa katika kuitekeleza, tunaweza kufanya kila kitu JF ikiwa inaendelea na mijadala lakini haipendezi wakati wa maintenances kadhaa kuiacha on kwani baadhi ya watu watakereka.

Tunawashukuru kwa ushirikiano na tunaomba uvumilivu wakati wa kazi hii ngumu tunayotarajia kukumbana nayo.

Sikitiko langu: Kuna baadhi ya posts zitaondoshwa wakti wa mapitio ya majukwaa yote na hasa zile ambazo zitaonekana hazina manufaa kwa jamii yetu.

Ahsanteni

Nawatakia kazi njema, na Idumu Jamiiforums.

Hivi kule kwa Mwanakijiji hatuwezi kujisitri kipindi hicho?. Samahani kama nitaonekana napiga debe ila tu nilitaka tuendelee kuchangamuka na kujuzana yanayoendelea duniani na hasa BONGO
 
Mkubwa Thanks for Infomation tuanze kutafuta sehemu za kwenda wikiend
Kazi Njema
 
Na atutafutie shughuli mbadala ya kufanya sasa...🙂😀🙂
Familia itafurahi sana kwa kupata attention this weekend....haya ni maradhi...😀
 
Kuna watu humu ndani sijui wataenda wapi?
 
Wa kwanza ni mimi maana weekend mimi uivuta kitandani nimelala maana sijui nende wapi.
Any way Invisible maintanence ni muhimu tu, na lazima yafanyike nitavumia na nitashinda nimelala hatakula sintakula labda nitakula usiku tu. Hii yote ili nisikumbuke kwamba natakiwa JF
 
Back
Top Bottom