Wadau naomba mnifahamishe nataka kujiua. Schizophrenia ni nini na wanatambulika vipi watu waliokuwa nayo hapa duniani?
Mnamo tarehe 06/06/2006 nilipata maono nikiwa kule UESPANYA. Maono ya REVELATION. Na baada ya hayo maono kuna siku nilokuwa nimekaa kwenye PARK fulani nikiwa naota JUA kama ilivyokuwa desturi ya watu tunaoishi huku.
Nikiwa nimekaa kwenye bench naota JUA huku nikiwa naliangalia ghafla nikajihisi kitu nisichokijua bila ya kukiona kikitoka ndani ya JUA na kunipiga kwenye paji langu la uso na kujihisi km kimefumua kwa nyuma kwenye kisogo, kisha wkt huo huo nikaanza kusikia sauti ikoongea nami toka ndani ya JUA ikiniambia kuwa yeye ni MUNGU mkubwa mwenye namba 666 na amependezwa nami, kwahiyo kuna kitu anataka niuambie ulimwengu. Kwa kweli nilishangaa sana tukio hilo!
Sauti iliniambia mambo mengi kwakweli siwezi kuyaelezea hapa yote. Baada ya hapo hiyo sauti ikawa inanitokea kila mara lakini safari hii hiyo sauti ikawa naisikia kutoka ndani ya kichwa changu sio kutoka nje. Yaani sio km mfano wa kusikia sauti kutoka kwa mtu unaeongea nae, hapana, hiyo sauti nilikuwa safari hii nasikia ndani ya kichwa changu.
Baadae nikaja kusafiri na kwenda kuishi Ujerumani na sasa hivi nna miaka kumi tangu niwe na hilo tatizo cha ajabu ile sauti bado nnayo tu.
Nimejaribu kwenda hospitari lkn bila ya vipimo kwa kusikiliza maelezo yangu tu wakaniambia kuwa nna hiyo SCHIZOPHRENIA. Sasa basi bado najiuliza ni nini hiyo SCHIZOPHRENIA, na kama ni ugonjwa, je kuna uwezekano mtu kupata ugonjwa toka ndani ya JUA? Na cha ajabu madoctor wameniambia kuwa nisimwambie mtu yeyote kuhusu hili tatizo.
Tafadhali waungwana naomba mnishauri nifanye nini ili hii sauti initoke kichwani maana naona wazungu wameshindwa. Pia naumia sana sababu sauti inaniambia mambo mengi ambayo mengine hayapaswi hata kutambulika kwa binaadamu anaendelea kushi hapa duniani!
Asanteni natumaini mtanisaidia!