Schmeichel kuhusu David De Gea na Dean Henderson

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Ni mapema sana kwa Manchester United kufikiria kumbadili kwenye jezi namba moja Davidi De Gea kwa ajili ya Golikipa wao aliye kwa mkopo katika klabu ya Sheffield United, Dean Henderson, kwa mujibu wa Peter Schmeichel.

Huku kiwango cha De Gea kikionekana kuyumba katika misimu miwili ya hivi karibu na Henderson akionesha kiwango kizuri kumekuwa na hoja za Muingereza huyo kuchukua nafasi ya Muhispania.

Peter Schmeichel hana hofu kuhusu uwezo wa Henderson lakini uhalisia wa kuwa namba moja wa Man United kuna vigezo vingine lazima viangaliwe.

“Kuna mtu yoyote anafikiria kutokuwa na David De Gea golini na nafasi yake achukue Dean Henderson sasa hivi ? Hakuna shaka kuhusu uwezo wa Henderson lakini amecheza msimu mmoja katika klabu ambayo imekuwa na msimu mzuri ndani ya Ligi ya Uingereza “.

“Henderson atahitaji kuonesha msimu mwingine kama huu ambao ameibuka, halafu na mwingine na mwingine tena , ili kumshawishi kila mtu kwamba ni kipa sahihi . “ .

“ Kuna utofauti mkubwa sana baina ya kuwa namba moja katika dimba la Bramall Lane na kuwa namba moja Old Trafford, tofauti kubwa sana. Hata kuwa mchezaji tu wa ndani kuna tofauti ya hivyo vilabu viwili “.

“ Nimeona watu wengi sana ambao wamekuja Old Trafford na rekodi zao , wafungaji magoli lakini wakashindwa kufanya kile walichoahidi kufanya kwa kuangalia viwango na vipaji vyao . Hiyo ni kwasababu presha ya Old Trafford ni tofauti , ni kubwa sana unajua “.

“ Kwa mfano kama Henderson akifanya kosa - naweza kukumbuka lile kosa dhidi ya Liverpool , itakuwa aaah sawa , bado mdogo na blah blah blah nyingi kwasababu anacheza Sheffield . Kama akifanya kosa Old Trafford akiwa na Manchester United basi itakuwa kichwa cha Habari hiyo , na itakuwa wiki nzima mpaka itakapokuja mechi nyingine , ambapo watu watakuwa wanahoji kuhusu uwezo wake.“

“ Kwahiyo swali, De Gea au Henderson? Kuna jibu moja tu hapa sasa hivi “

 
Edwin Van de Ser alitokea Fulham na akashine OT Kwa sasa Dean Henderson ni bora kumzidi De Gea msimu ukiisha arudi nyumbani OT ili De Gea apumzike.
 
Edwin Van de Ser alitokea Fulham na akashine OT Kwa sasa Dean Henderson ni bora kumzidi De Gea msimu ukiisha arudi nyumbani OT ili De Gea apumzike.
Unajua De gea alitokea Ajax, Juventus ndio Furaham. Huwez kumleta mbadala wa De gea kwasababu ame ng'aa klabu za vichochoroni.

Pale OT pana presha kubwa huwezi fanya jambo nyeti kama la kubadili kipa kirahisirahisi ni sawa na kucheza kamali.
Umetokea kwenye kiwanja kinachukua mashabiki 500 unakuja kwenye uwanja wenye mashabiki zaidi ya 70,000. Mwishoe yanakua ya Masiano Taibi Siku ya Man U na Chelsea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa hiyo unataka tuendelee na De Gea ambae ameshuka kiwango kuliko kumleta Dean?
 
Edwin Van de Ser alitokea Fulham na akashine OT Kwa sasa Dean Henderson ni bora kumzidi De Gea msimu ukiisha arudi nyumbani OT ili De Gea apumzike.
Kabla ya kwenda Fulham unafahamu kuwa alikuwa ameshapiga Champions League za kutosha!?
 
Sikuwahi kujua kama De Gea alitokea Fulham,Ajax na Juve,nnacho jua tulimnunua 2012 kutoka Club de Atletico ďe Madrid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kwenda Fulham unafahamu kuwa alikuwa ameshapiga Champions League za kutosha!?
Ina maana ili Dean Henderson awe bora unataka acheze UCL akiwa na Sheffield? Kwa sasa Dean Henderson ni bora kumzidi De Gea. Na De Gea kiwango chake kimeshuka Sana huu ni msimu wa pili hayupo kwenye kiwango kizuri.
RUDI NYUMBANI DEAN HENDERSON KARIBU.
 
Edwin Van de Ser alitokea Fulham na akashine OT Kwa sasa Dean Henderson ni bora kumzidi De Gea msimu ukiisha arudi nyumbani OT ili De Gea apumzike.
Kabla ya kuja Fulham alicheza Ajax anachukua kombe la uefa akahamia juve ndio akaja man u
 
Dean Henderson, ubora wake sio wa kubahatisha. Msimu uliopita akiwa Championship alikinukisha akiwa hapohapo Sheffield United. Amekuwa pale United kitambo sana ila amekuwa akitolewa kwa mkopo kuimarisha ubora wake. Kwa sasa sidhani kama yupo tayari kuwa kipa namba moja wa United. Msimu ukiisha mkataba wake unaisha Sheffield United ila nadhani msimu ujao tunapaswa kumrudiaha tena Sheffield United, hawa ndio wanatusaidia kulea kipaji chake vizuri kabisa.

David De Gea ni moja ya makipa bora kabisa EPL na misimu hii miwili hajawa vizuri ila bado anahitaji muda, Deano kuingizwa kikosi cha kwanza itakuwa ni jambo la taratibu, kumtoa De Gea akae Deano golini au kumtoa Romero bench akae Deano inahitaji maamuzi magumu sana.
 
Huyu dogo wa shelfield kumbe ni mchezaji wa Man u!!! daah, leo ndio nimejua kwanini yule jamaa yangu shabiki wa Man u alikuwa anamsifia sana huyu kipa.[emoji3][emoji3][emoji119]
 
Bwashehe umejicontradict hebu jisome tena.Halafu kwa Fulham umeandika Furaham

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…