hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 13,628
- 20,992
Ni mapema sana kwa Manchester United kufikiria kumbadili kwenye jezi namba moja Davidi De Gea kwa ajili ya Golikipa wao aliye kwa mkopo katika klabu ya Sheffield United, Dean Henderson, kwa mujibu wa Peter Schmeichel.
Huku kiwango cha De Gea kikionekana kuyumba katika misimu miwili ya hivi karibu na Henderson akionesha kiwango kizuri kumekuwa na hoja za Muingereza huyo kuchukua nafasi ya Muhispania.
Peter Schmeichel hana hofu kuhusu uwezo wa Henderson lakini uhalisia wa kuwa namba moja wa Man United kuna vigezo vingine lazima viangaliwe.
“Kuna mtu yoyote anafikiria kutokuwa na David De Gea golini na nafasi yake achukue Dean Henderson sasa hivi ? Hakuna shaka kuhusu uwezo wa Henderson lakini amecheza msimu mmoja katika klabu ambayo imekuwa na msimu mzuri ndani ya Ligi ya Uingereza “.
“Henderson atahitaji kuonesha msimu mwingine kama huu ambao ameibuka, halafu na mwingine na mwingine tena , ili kumshawishi kila mtu kwamba ni kipa sahihi . “ .
“ Kuna utofauti mkubwa sana baina ya kuwa namba moja katika dimba la Bramall Lane na kuwa namba moja Old Trafford, tofauti kubwa sana. Hata kuwa mchezaji tu wa ndani kuna tofauti ya hivyo vilabu viwili “.
“ Nimeona watu wengi sana ambao wamekuja Old Trafford na rekodi zao , wafungaji magoli lakini wakashindwa kufanya kile walichoahidi kufanya kwa kuangalia viwango na vipaji vyao . Hiyo ni kwasababu presha ya Old Trafford ni tofauti , ni kubwa sana unajua “.
“ Kwa mfano kama Henderson akifanya kosa - naweza kukumbuka lile kosa dhidi ya Liverpool , itakuwa aaah sawa , bado mdogo na blah blah blah nyingi kwasababu anacheza Sheffield . Kama akifanya kosa Old Trafford akiwa na Manchester United basi itakuwa kichwa cha Habari hiyo , na itakuwa wiki nzima mpaka itakapokuja mechi nyingine , ambapo watu watakuwa wanahoji kuhusu uwezo wake.“
“ Kwahiyo swali, De Gea au Henderson? Kuna jibu moja tu hapa sasa hivi “