Ndugu D5,
Umesemaa amepata admission social sciences halafu baadae ukasema Msc. Naona kama kunaweza kuwa kuna confusion hapo. Social sciences hupelekea kupata MA (unless kuna kitu sijui ktk hili). Anyway, sio ishu sana.
Wapo wafadhili wengi sana anaoweza kuwapata hasa kama ameshapata admission tayari. Tatizo ni kuwa hujasema amepata admission ya kusoma nini. Social sciences bado ni too general. Ninachojua mimi wanaotoa scholarship wengi wanapenda usome ktk local universities-inakuwa rahisi sana (zaidi) kupata kuliko ya kwenda nje. Sasa basi balozi hizi hutoa scholarship sana kwa watu wanaojua kuzifuatilia.
(1) Ujerumani (Chini ya mwavuli wa wizara yao ya mambo ya nje kwa kupitia Deutsher Akademischer Austausch Dienst, DAAD)
(2) Ubalozi wa Ireland
(3) Ubalozi wa China
(4) Balozi za nchi za Scandinavia-Norway, Sweden, Denmark na Finland
(n.k)
NB. Mara nyingi scholarship zao zinalenga maeneo ambayo yatakuwa na manufaa directly kwa jamii. Mostly mazingira, education, sciences kwa ujumla. Sheria NO etc.
Ajaribu kucheki hizo. Afuatilie asisubiri kuunganishiwa. Anaweza kugoogle akaona kama balozi zao wana scholarsship kwa Tz this yr.
Asante. namtakia kila la kheri.