Sean “Diddy” Combs, amepatikana na hatia katika mashtaka mawili kati ya mashtaka matano yaliyokuwa yakimkabili

Sean “Diddy” Combs, amepatikana na hatia katika mashtaka mawili kati ya mashtaka matano yaliyokuwa yakimkabili

Fufua Tumaini Jipya

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2024
Posts
223
Reaction score
469
MWANAMUZIKI Mkongwe duniani Sean “Diddy” Combs, amepatikana na hatia katika mashtaka mawili kati ya mashtaka matano yaliyokuwa yakimkabili.
FB_IMG_17514755210575094.jpg

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mahakama ya New York Nchini Marekani, Rapa huyo amepatikana na hatia katika tuhuma za kufanya usafirishaji unaohusiana na biashara ya ukahaba huku akifutiwa mashtaka mazito zaidi yaliyokuwa yakimkabili katika kesi hiyo ambayo yanahusiana na kuwalazimisha Wanawake kufanya ngono na Wanaume wengine.

Diddy (55) alishtakiwa kwa makosa matano ambapo shtaka mojawapo ni la kula njama na makosa mawili kila moja ni ya biashara ya ngono na kushiriki katika usafirishaji unaohusiana na biashara ya ukahaba ambapo hata hivyo hakupatikana na hatia yoyote ya kula njama na kushiriki katika biashara ya ngono.

Jaji amesema Diddy hajapatikana na hatia katika kosa la njama za ulaghai, pia hajapatikana na hatia katika mashtaka ya ‘ulanguzi’ wa ngono wa Mpenzi wake wa zamani aitwae Cassie Ventura.

Vyombo vya Habari Nchini Marekani vimeripoti kuwa Diddy anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 kutokana na makosa hayo.

#KitengeUpdates
 
Back
Top Bottom