SEASONAL CARDS

ipogolo

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2011
Posts
6,280
Reaction score
5,979
Wapendwa hongera kwa juma la pasaka.
Kweli dunia inabadilika kwa kasi kubwa.
Miaka 10 iliyo pita tulizoea kutumiana kadi za Eid, Easter, Xmas no.
Tulinunua kadi kwenye stationary na kutuma kwa Posta kwenda kwa wapendwa wetu.
Pamoja na maneno yaliyochapishwa kwenye kadi,tuliweza pia kuongeza vimaneno viwili vitatu kuchagiza.
Mpokeaji akipata kadi kupitia SLB( Posta) alipata furaha na kuona" BARUA NI NUSU YA KUONANA"
Siku hizi tunatuma kupitia Simu zetu na zikijaa unadelete na kupotezea.
Nyingi maneno yake yanafanana ( fowadedi). Kupoteza mvuto na hisia.
AMA Kweli dunia inakimbia kama super Sonic speed Concord.
PASAKA NJEMA.
 
Na ww pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…