Sebule yenye ukubwa wa futi 14 kwa 13 zinaingia tiles box ngapi na bajeti yake yote

Munch wa annabelletz47

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2019
Posts
1,885
Reaction score
3,227
Wakuu naomba kujua sebule yenye vipimo hivo inaingia tiles box ngapi? Na nahitaji tiles ambazo ni affordable kwa mlala hoi lakin imara urembo SIO kipaumbele, vilevile gharama za ujenzi zote pamoja na mafundi

Karibuni kwa mchango wenu wadau
 
Mkuu ingependeza kama ukampata fundi sahihi na mwenye uzoefu kazini ili akupatie idadi sahihi na sio kutegemea mafundi kutoka humu jamii forum hutopata kitu zaidi ya kejeli na dhihaka tu.
 
Mkuu ingependeza kama ukampata fundi sahihi na mwenye uzoefu kazini ili akupatie idadi sahihi na sio kutegemea mafundi kutoka humu jamii forum hutopata kitu zaidi ya kejeli na dhihaka tu.
Mkuu JF wenye akili timamu bado wapo wengi sema ndo hawajiheshimu tu
 
Wakuu naomba kujua sebule yenye vipimo hivo inaingia tiles box ngapi? Na nahitaji tiles ambazo ni affordable kwa mlala hoi lakin imara urembo SIO kipaumbele, vilevile gharama za ujenzi zote pamoja na mafundi

Karibuni kwa mchango wenu wadau
Mwambie fundi akwambie Kila kitu Sisi tunakupanga tiles nzuri na bei Tu
 
Piga hivi hesabu

Tiles nyingi size yake ipo kwenye cm/m

Futi 14 x futi 13 = 4.27m x 3.93m = 16.78sqm

Weka 10% ya uharibifu = 16.78sqm * 1.1 = 18.46sqm

Angalia box moja lina piece ngapi zenye size gani

Mfano 50cm x 50cm halafu ziko 8 maana yake box moja lina 0.5m x 0.5m x 8 = 2sqm

Kama ni 120cm * 60cm halafu ziko 4 itakuwa 1.2m x 0.6m x 4 = 2.88sqm

Gawanya size 16.78 kwa size ya box moja mfano 2sqm unapata box 8.39 = box 9
Gawanya size 16.78 kwa size ya box moja mfano 2.88sqm unapata box 5.8 = box 6

Box moja shilingi ngapi, kazi kwako
 
Tiles 40×40 box 9=tsh. 270000 wastani, grout kg 1=tsh.3000, tiles za scatting box 1=tsh.35000, mchanga ndoo kubwa fanya 15=tsh.__sijui uko wapi, maji pipa 1=tsh.__sijui kama unanunua au vipi, Cement 3=tsh.__sijui uko wapi, fundi haizidi tsh. 80,000/-. KARIBU.
 
C
Location chalinze
 
Mbona nimeshakupa au haujaona reply

Au umeleewa???

Futa 13 ni sawa na mita 3.93
Futa 14 ni 4.24

Unachukua 4.24 x 3.93 =16.7

Unachukua tile za 40cm

0.4 x 0.4 = 0.16cm

16.7 ÷ 0.16 =
Mkuu hesabu zako kuelewa inabd uwe na akili zaid ya eistein
 
Wakuu naomba kujua sebule yenye vipimo hivo inaingia tiles box ngapi? Na nahitaji tiles ambazo ni affordable kwa mlala hoi lakin imara urembo SIO kipaumbele, vilevile gharama za ujenzi zote pamoja na mafundi

Karibuni kwa mchango wenu wadau
Sebule yako ina
16.38sqm
Ukitumia tiles 40*40
Box moja ni 1.92sqm
16.38/1.92
Utatumia box 8.5.
Huwezi kupata nusu box hivyo utahitaji box 9.
 
Umenisaidia mpaka Mimi idumu jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…