Masikini, dada wa watu, pole yake kuna rafiki yangu mmoja yeye alishawahi kunisimulia kuhusu secret admirer wake, huyo shoga yangu ana - supermarket jamaa alikuwa mteja wake, sasa eti akihisi harufu ya perfume ya huyo secret admirer wake yeye hooooooooooooooooooooooooi, lakini hamwambii, ila kusema ukweli tulivyopata fursa ya kumuona tukiwa pamoja dada alinionyesha huyo kaka kwa kweli alikuwa yuko good looking sana tu. Mbaya zaidi dada alifanya jitihada za kumwonyesha kaka lakini naona mwenzake hakuelewa kabisa. Sasa ikatokea kukawa na harusi ya mdogo wake na rafiki yangu, dada akampa kadi ya mwaliko, kweli kaka akahudhuria sherehe na mchuchu wake, looooh dada karibia arudi nyumbani maana alibadilika ghafla, akawa mwekundu, uchangamfu wote ukamwisha, aliugulia maumivu, akapoteza mwelekeo, jamaa naye hakuwa na hiana wakati wa kuondoka akajakumuaga na kumtambulisha. Ila story ya huyu shosti wangu mwishowe walikuja kupendana lakini pia hawakudumu. Kwa sababu kumbe jamaa alikuwa ana mke mwingine zaidi ya yule aliyemtambulisha shotsti wetu. Haya sasa ku-admire vitu vya wenye navyo.