FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,789
- 5,401
- Thread starter
-
- #41
Nadhani FL, hupaswi tu kumshangaa. Hebu tueleze baadaye wewe ulimsaidiaje? au utamsaidiaje au ndo unaendelea kumshangaaa!!
huyo ni mental case aisee, ni obsessive disorder
duh
Itamsaidia sana tu.Atafanikiwa kumtoa moyoni mwake hata kama kwa maumivu ili apishe nafasi kwa mwingine atakaempenda.Hata hivyo itabidi umkanseli kwanza kuwa kukataliwa sio mwisho wa maisha na kwamba Mungu ana Mpango maalumu kwa ajili ya maisha yake ikiwa ni pamoja na kumpa mwezi sahihi atakaempenda bila masharti.Mpendwa katika bwana itabidi unipe mbinu mbadala hivi akikataliwa si ndo atakufa huyu dada ..mapenzi gani haya ya kuuguzana .??
Kweli mie sijamsaidia lolote mpaka sasa ndo naona huu ushauri wa wadau najaribu kufikiria cha kufanya :A S 39:
FL Am standing to be corrected, kama ni secret admirer ina maana huyu kaka hajui kama huyo binti kampenda so anafanya mambo yake vile anavyofikiri kuwa ni sawa, kama kweli huyo dada yuko penzini kiasi hicho si asonge tu front akamueleze huyo secret admirer wake kuwa amevumilia ameshindwa so anatangaza nia!
...mwambie haikuwa rizki yake ndio maana akayaona hayo. Kilichomliza siku hiyo ingekuwa kilio chake cha kila siku. Akiacha alinacha zake, atawaona 'secret admirers' wanaotamani yeye awe la'aziz wao vile vile.
Hapo kwenye RED hawezi kuondoa hisia bila kuujua ukweli.....maana nnawezekana mkaka wa watu wala hana hili wala lile....We mwambie bana "Avunje Ukimya".... kama "mbwai mbwai tu bana".....hakuna kitu kizuri cha kua na amani kama kuujua Ukweli ingawa sometimes unauma....Thanks Mbu kwa hiyo hapa binti inabidi ajaribu kuondoa hisia zake juu ya kaka huyo na kusonga mbele na maisha
nadhani hii itakuwa njema kwake ..nitaongea naye yote na pia baada ya muda nitamwambia pitie hapa Ndani
sidhani kama amevuka kikomo...hapo ndio hisia zake zilipofikia mwisho....japo hata mimi namlaumu muda wote huo miaka miwili mbona mingi sana, alitakiwa ndani ya miezi sita awe anammiliki mkaka
Mi ninaye hapa naona tatizo ndo hilo hilo hebu nisaidieni wadau:A S confused:
Hapo kwenye RED hawezi kuondoa hisia bila kuujua ukweli.....maana nnawezekana mkaka wa watu wala hana hili wala lile....We mwambie bana "Avunje Ukimya".... kama "mbwai mbwai tu bana".....hakuna kitu kizuri cha kua na amani kama kuujua Ukweli ingawa sometimes unauma....
Mi ninaye hapa naona tatizo ndo hilo hilo hebu nisaidieni wadau:A S confused:
Msaidie wewe FL1 .nenda kamwambie huyo kaka kuhusu huyo dada anayempenda.Ili ajue moja kama Gender Sensistive
Kuna Binti hapa kaniacha hoi mie labda na nyie atawashangaza
Huu ni mwaka wa pili sasa yuko kwenye hiyo secret admirer na kaka mmoja ,
Kila siku binti anategeshea amuone huyu kaka ndo apande gari aliyopo,Lunch time anategea mida ya huyo kaka kwenda lunch ndiona yeye anaenda amekuwa kama mtumwa wa penzi na kusema hawezi.
Cha kushangaza jana tumeenda kwenye Party moja,,,,Binti akiwa anaenda Toilet kamkuta huyo secret admirer wake amekumbatiana na mdada mmoja wa haja wanakiss
Kaja kuniaga huku anabubujikwa chozi eti anaenda home hawezi kuendelea na partyl,leo hajafika kazini namuuliza kulikoni kanipa mkasa kamili...
Kumwambia amesema hawezi tena sasa anauguza majeraha ya mapenzi
Hii imekaaje wadau?:A S 39::A S 39:
Masikini, dada wa watu, pole yake kuna rafiki yangu mmoja yeye alishawahi kunisimulia kuhusu secret admirer wake, huyo shoga yangu ana - supermarket jamaa alikuwa mteja wake, sasa eti akihisi harufu ya perfume ya huyo secret admirer wake yeye hooooooooooooooooooooooooi, lakini hamwambii, ila kusema ukweli tulivyopata fursa ya kumuona tukiwa pamoja dada alinionyesha huyo kaka kwa kweli alikuwa yuko good looking sana tu. Mbaya zaidi dada alifanya jitihada za kumwonyesha kaka lakini naona mwenzake hakuelewa kabisa. Sasa ikatokea kukawa na harusi ya mdogo wake na rafiki yangu, dada akampa kadi ya mwaliko, kweli kaka akahudhuria sherehe na mchuchu wake, looooh dada karibia arudi nyumbani maana alibadilika ghafla, akawa mwekundu, uchangamfu wote ukamwisha, aliugulia maumivu, akapoteza mwelekeo, jamaa naye hakuwa na hiana wakati wa kuondoka akajakumuaga na kumtambulisha. Ila story ya huyu shosti wangu mwishowe walikuja kupendana lakini pia hawakudumu. Kwa sababu kumbe jamaa alikuwa ana mke mwingine zaidi ya yule aliyemtambulisha shotsti wetu. Haya sasa ku-admire vitu vya wenye navyo.