Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
UTANGULIZI
Tunaishi hapa duniani, kuna siri nyingi zipo na wale wanaoweza kuzifahamu wanapata kujua mambo ya spirituality. Ni ukweli usiopingika kuwa pamoja na Sayansi kuleta mabadiliko makubwa lakini vilevile Imani zinaleta mabadiliko makubwa zaidi. Msimamo wangu ni Imani ipo na nafasi kubwa sana katika maisha yetu, vilevile sayansi nayo ipo na nafasi katika maisha yetuLeo ninapenda nitoe siri ambayo inawafanya watu waweze kujiunganisha na ulimwengu wa roho. Moja ya siri hizo ni DAMU.
DAMU NI NINI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
Katika ulimwengu wa Roho, damu huwa inazungumza. Damu inaweza kukunenea na kukufanya uweze kutakasika. Damu inafungua milango ambayo imefungwa.NItajikita sana kuongelea mambo yaliyomo kwenye Biblia maana ndio msingi wangu na nikitabu changu cha kwanza kuanza kujifunza mambo ya kiroho.
Damu ni Uhai Mambo ya Walawi 17:11
Kwa kuwa uhai wa mwili uko katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.
Damu inatumika kuidhinisha maagano kati ya Mungu na wanadamu. Mwanzo 15:9-21, Kutoka 24:8
Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.
Damu ni Upatanisho Mambo ya Walawi 16:15-16
15 Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya vile vile kama alivyofanya kwa damu ya ng'ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema,
16 naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao.
Watu wameacha misingi hii muhimu sana ya kujiunganisha la ulimwengu wa roho. Wengine wanasema kuwa Damu ya Yesu inatosha. Lakini ukweli ni kwamba kama unataka kujiungamananisha na ulimwengu wa roho ni muhimu sana kuanza kujifunza kutoa sadaka ya kuchinja
JE NANI ANATAKIWA KUCHINJA?
Je umewahi kujiuliza, kwanini hapa Tanzania ni watu wa dini fulani tu wanatakiwa kuchinja? Watu wengi hawajui maana yake na imekuwa kama utamaduni ambao msingi wake ni mambo ya kiroho.Unapo chinja mnyama unaneno maneno. Maneno hayo yanapelekwa moja kwa moja katika ulimwengu wa roho kwa niamba yako. Watu wanachukulia kawaida tu.
KUNA JAMII WANAKUWA NA SHEREHE YA KUJICHA NA KUGAWA NYAMA BURE
Kama hujajua siri hii utaendelea kutawaliwa na wenzako watakuwa wakifanya biashara kubwa. Wewe unaendelea kusema damu ya Yesu yatosha huku ukienda kwa Mwamposa kila Siku. Lakini Mambo ya msingi utaendelea kuyasikia kwa wenzako.
Ukija kuangalia kuna baadhi ya tamaduni wanafanya hivyo. Mfano wapo kila mwisho wa mwaka wanaenda nyumbani kwao na kuchinja wanyama kisha wanakula na jamii yao kwa pamoja. Wengine wanaikinga hiyo damu na kuioga. Lakini wengine wakula na kuita kisusio.
NGOJA NITAENDELEA...