KERO Secretariati ya Ajira kupeleka usaili wa mahojiano Dodoma wakati written zilifanyika mikoani si sawa!

KERO Secretariati ya Ajira kupeleka usaili wa mahojiano Dodoma wakati written zilifanyika mikoani si sawa!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kuwasilisha malalamiko yangu:

Ni kwanini hawa PSRS wanapeleka oral interviews Dodoma ilihali written zinafanyka mikoani jambo hili linawagusa graduates wengi wa kada tofauti na ualimu na afya wao kila kitu wanafanya mikoa walipo lakini kwa kada nyingne ni lazima uende Dodoma?

Kiufupi, vijana tunaumia nauli na maradhi yako juu Dodoma na hao watendaji sielewi walielewaje maagizo ya Serikali maana iliagizwa usaili watu wafanye mikoa walipo kupunguza gharama za nauli na accomodations.

Kundi linaloumia ni fani za uhasibu, sheria, wahandisi, n.k ,

Ombi langu: Kama waliagizwa saili zifanyike mikoani watekeleze maagizo ya Serikali waache kusumbua watu kwenda Dodoma isipokua kwa walioko huko sawa wafanye huko.

Ahsante!
 
Ila Nyerere alitengeneza kizazi cha hovyo sana. Yaani hata kutoa ushauri mzuri tu kama huu inabidi kuwa Anomyious. Sikulaumu mleta mada, nalaumu mifumo
 
..shukuru Mungu hata hio Oral umeitwa... kuna wenzako wana 10 plus hawajawahi kuitwa popote for interview, licha ya kufanya maombi kichele.....
Mpumbavu
 
Hizo kada wanasoma watu wanaojiweza kiuchumi, wana haki ya kuitwa Dodoma.
 
Back
Top Bottom