Secrets of the Trade (Butcher)

sun wu

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
2,020
Reaction score
1,422
Wadau napenda kuja na wazo la ku-disect biashara fulani fulani ili tuweze kufahamu undani wa hiyo biashara (najua jungu kuu na humu ndani kuna wafanyabiashara tofauti)..

Mfano niliongea na muuza karanga akaniambia mara nyingi shilingi huzaa shilingi kwenye karanga zake.., au muuza soda, magazeti, bia au voucher anakula percent kiasi ya kila anachouza..

Sasa kwa kuanza na Butcher.., Wadau hivi kwenye hii biashara wenye butcher wengi huwa wananunua wanyama na kuwapeleka kuchinja (then ndio wanauza) au wananunua machinjioni na kuuza reja reja ?, na margin ni kiasi gani ukizingatia kwamba kuna kuharibika na mzigo kuoza ?

Na je unaweza kununua mfano Cuts unazotaka (mfano utumbo peke yake au mkuu au mbavu) ?

Natanguliza shukrani...

Sun Wu.... The Seeker of Knowledge
 
yeah. ng'ombe wanatoka shinyanga wanapelekwa machinjion ( according to order) wanachinja afu wenye mabucha wanaenda kununua kwa jumla.
kama una mabucha mengi ndo unaweza kuleta ng'ombe wako wakuchinjie.
 
Ukinunua kwa jumla margins zipo vipi ?, yaani kila kilo unakula buku ngapi ?

Na ununuaji wa jumla wanapima kilo za mchanganyiko, au unaweza ukaamua kununua nundu, utumbo , mguu au mbavu peke yake ?, yaani wanauza kulingana na cuts (prime cuts bei kubwa na nyingine tofauti)?, Mfano muuza mishikaji anaweza kwenda machinjioni akaomba akatiwe steak kwa bei poa, au yeye inabidi aifate butcher ?
 
hapo sijui chochote, ntakudanganya nikiendelea
 
Thi is very interesting...biashara za wanyama na mazao huwa tuna zipiga kikumbo kuliko kuangiza nguo na vitu toka Turkey, Thailand na China.
Lakini nchi kama Comoro, Mauritiu na Middle East biashara ya wanyama inalipa kweli kweli....
 
Kesho nikienda sokoni nitaongea na muuza nyama then nitakuletea jibu
 
Kesho nikienda sokoni nitaongea na muuza nyama then nitakuletea jibu

wengi huwa hawasemi siri ya urembo..., hapo tu atakwambia duh siku hizi nyama kazi kweli kweli yaani mimi hapa faida ni tshs 100 kwa kilo .., si unajua tena 🙂 (unless ni jamaa yako)

Lakini kipindi nilikuwa Arusha nilipita pale Arusha Meat waliniambia bei inalingana na cuts.., yaani ukitaka prime cuts nadhani hii huwa ni kwenye miguu na makalio hapo utatoa bei kubwa sana.., ingawa nilikuwa naongea na jamaa mmoja wa mikoani akaniambia kwamba kilo ni kilo hawajali ni kilo ya nini (issue ambayo kwangu haikumake sense.., kwanini mtu anunue sehemu yenye mifupa mingi wakati yenye nyama ndio ina faida)..

All in all ningependa kujua margins za hii biashara
 
swali zuri sana ........nilishawi muuliza mmiliki wa bucha juu ya hii margin akaniambia ni 1000 per kilo ...na inapanda sana kipindi cha siku kuu .........anasema akiuza kilo 100 anajua margin yako hapo 100,000( this was last year ) tusubiri mfanyabiashara atakuja tu humu na jibu la uhakika
 
Okay kwahio huenda vyote yaani utumbo, mchanganyiko, maini, steki n.k. anakula buku buku ?, basi kama ni hivyo ujanja ni kuhakikisha nyama hailali, by the way kwahio mtu akiwa na sikukuu anaweza kwenda machinjioni akachukua nyama kwa bei ya muuza butcher ?, yaani kilo mia moja za steki (kwa bei ya butcher minus 1000)
 
Nadhani ndio maana wanaita Secrets of the Trade..., Watu wanazificha..,
 
Hata Husninyo aliyeenda kununua nyama toka mwaka 2013 hajarudi kuleta mrejesho.....

Siri ys Biashara wanaifichua wafanyabiashara wenyewe kwa warithi wao tuu, mwingine atakupa asilimia 20 au 60 baasi.
 
Hata Husninyo aliyeenda kununua nyama toka mwaka 2013 hajarudi kuleta mrejesho.....

Siri ys Biashara wanaifichua wafanyabiashara wenyewe kwa warithi wao tuu, mwingine atakupa asilimia 20 au 60 baasi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nafkiri Bado anapewa Siri hiyo. So tuwe wapole akimaliza ataileta[emoji4]
 
Hata Husninyo aliyeenda kununua nyama toka mwaka 2013 hajarudi kuleta mrejesho.....

Siri ys Biashara wanaifichua wafanyabiashara wenyewe kwa warithi wao tuu, mwingine atakupa asilimia 20 au 60 baasi.
napenda kufahmu namna hii biashara ianvyoendeshwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…