Wanabodi,
Hili ni bandiko la security alert lenye hoja 54 kati ya hoja hizo, hoja 33 ni maswali ya kiusalama kuhusu taifa letu Tanzania.
Angalizo Kuhusu Security Conscious
Ulinzi wa taifa sio jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama pekee bali ni jukumu la kila Mtanzania Mzalendo wa taifa lake. Hakuna hujuma yoyote kama ugaidi, inaweza kupangwa na watu wa nje bila ushirikiano na watu wa ndani.
Security Conscious ni uwezo wa kuinusa hatari ya usalama wa taifa kwa mbali kabla haijatokea, hivyo hili ni bandiko la kizalendo la kutoa angalizo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, kuwa kuna kitu hawa mabeberu wa Marekani wanakipanga kuhusu Tanzania kwa siku zijazo, sasa ili kukihalalisha, wanapenyeza watu wao kwa makini kabisa na very strategically kutafuta local collaborators ili muda muafaka wa kufanya yao ukifika, hao local collaborators ndio watatumiwa na kuonekana ni Watanzania wenyewe.
Mpango wenyewe uko hivi:
- Kuna mambo ya jinsi rais Magufuli anavyoendesha nchi, Wamarekani hawapendi.
- Wamarekani wanalazimisha modal yao ya demokrasia iwe ndio standard democratic modal kwa nchi zote, bila kuzingatia Tanzania tuna modal yetu ya demokrasia ambayo ni part of African Democracy, ambayo inaruhusu nchi ya vyama vingi, kufanya uchaguzi wa vyama vingi na chama kimoja kupata ushindi wa 99.9% na uchaguzi ukawa ni wa kidemokrasia, huru na wa haki kama ilivyo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Wao mabeberu hawa wa Marekani hawataki kukubali hilo
- Kufuatia ushindi wa CCM wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, na sasa ndicho kinachokwenda kutokea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ili hili lisitokee, Marekani itatumia fedha nyingi sana kufund political dissidents ili kuonyeshea dunia jinsi rais Magufuli anavyopingwa.
- Baada ya ushindi wa kishindo cha asilimia 90+% kwa rais Magufuli na CCM, kwa uchaguzi wa mwaka huu, kuna watu watapangwa kuleta chokochoko na vitendo vya kigaidi, hivyo kupitia mkataba wa ugaidi na Marekani, Marekani inaweza kuingia nchi yoyote kwa kisingizio cha kusaka magaidi ila lengo lao sio kusaka magaidi bali ku fund dissidents kum distabilize Magufuli.
- Pia Marekani inataka kulazimisha human rights records zake kuwa ndio standards records kitendo cha kumzui Makonda kuingia Marekani, mlengwa sio Makonda, Makonda ni chambo tuu, lengo ni kuichafua taswira ya nchi yetu kimataifa tuonekane tuna bad human rights records, wakati kiukweli Marekani ina worse human rights records kuliko sisi!.
- Katika utekelezaji wa nia hii ovu, Marekani kwa kutumia taasisi zake, imeanza kusambaza taarifa za uongo na uchochezi kwa kudai kuwa serikali ya rais Magufuli inaendeshwa kwa mfumo Kistu hivyo ku fund Muslim extremist na fundamentalists kuwa magaidi na kufanya vitendo vya kigaidi.
- Tayari baadhi ya Taasisi za Kimarekani zimeanza kuandika utabiri wa kuibuka kwa ugaidi Tanzania baada ya rais Magufuli kushinda.
- Mtanzania Mzalendo mwenye security conscious akisoma mahali na kubaini kuna kitu ambacho sio kizuri kinapangwa dhidi ya nchi yake, jukumu lake ni kusema tuu alichokisoma na anacho kiona.
- Ni jukumu la vyombo vyetu vya usalama, sio kuzingatia kila kinachosemwa mitandaoni kuhusu usalama wa taifa letu lakini pia wakisikia kitu sio kuzipuuzia.
- Mimi kama Mzalendo nimetimiza wajibu wangu, sasa niwapeleke kwenye makala yenyewe ya bandiko hili ambayo imetokana na bandiko hili la mwana jf dada yetu al maaruf kwa jina la Faiza Foxy USA yaendelea kuichimba Tanzania
- Hoja hizi 54, zenye maswali 33 ni maswali ya msingi sana, japo kuna hoja za urongo humu sio za kuzizingatia, lakini pia kuna hoja za ukweli, sio za kuzipuuzia
Jumatatu njema
Paskali