tucker carlson
Senior Member
- Oct 5, 2025
- 182
- 759
Wakuu,
Nasikitishwa sana na hiki nilichokiona hapa kwenye hii barabara ndogo ya Segesela Street hapa Sinza, ni kamtaa fulani kanaanzia hapa Mlimani City kuelekea Kitambaa Cheupe.
Hii barabara ni mpya na ilikuwa inajengwa na Wachina, imejengwa kwa zege, of course ni kitu kizuri lakini baada ya kujenga kwanini mmeacha uchafu kama mifuko na mabomba baada ya ujenzi?
Barabara ni mpya, lakini tayari imeanza kuonekana chafu kutokana na kujaa mifuko ya plastiki kila sehemu. Kipindi hiki cha mvua, mifuko hiyo huingia kwenye mifumo ya majitaka na mitaro ya kupitisha maji, jambo linalosababisha kuziba kwa njia hizo. Matokeo yake maji yanashindwa kupita kwa urahisi na kusababisha maji kutuama.
Kama mliweza kutujengea barabara basi mnaweza kuondoa hii mifuko. Mamlaka zinazohusika, zifanye kweli.