Sehemu nzuri za mashamba/ viwanja bagamoyo

Sehemu nzuri za mashamba/ viwanja bagamoyo

Great thinkers, ni wapi naweza nikapata mashamba sehemu nzuri karibu na barabara au isiwe mbali sana na barabara bagamoyo ? Viwanja pia itakuwa vizuri.. Na gharama zake zina range kuanzia gani ? Thanks in advance
ViwanjaVilivyopimwa (Surveyed Plot) – Maeneo ya Bagamoyo. Ndugu, nakupongeza kwa fikara zako za kutaka kuwekeza kwenye viwanja au shamba pande za Bagamoyo. Kuna viwanja (SurveyedPlots) zinauzwa Tshs. 13,500.00 kwa meta moja ya mraba (TZS 13500.00 per square meter). Viwanja hivi vipo 6 km kabla ya kuingia Bagamoyo mjini ukitokea Dar esSalaam, upande wa kushoto. Eneo hilo linaitwa Mataya. Ramani ndogo pamoja na chati inayoonyesha viwanja hivyo pamoja na ukubwa wake imeambatanishwa.Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutumia namba +255 754 787 775 au +255 655 787 775. Email address – gck@ksonsfreight.co.tz au info@ksonsfreight.co.tz. Kuhusu Kutapeliwa. Katika kila mradi kuna element ya risk. Japo hatuwezi tukaacha kufanya kitu kwa kuogopa ku-risk. Cha msingi ni kujipanga na kuwa na tahadhari (Risk Management). Ni vizuri kuepuka watu wanaotaka kufanya mambo kwa uficho. Usikubali kuuziwa kiwanja au shamba bila ofisi ya kijiji kujua. Pia, japo ni ghari lakini unaweza ukawahusisha wanasheria ili kongeza kiasi cha risk management. Ukitaka maelezo zaidi basi tuwasiliane! Kwa nini ufikirie kununua kiwanja au eneo pande za Bagamoyo zaidi ya maeneo mengine? Bandari ya Bagamoyo (SEAPORT) na Export Processing Zone (EPZ) Bandari kubwa ya mizigo itaanza kujengwa hivi karibuni kule Bagamoyo. Kumekuwa na ongezeko endelevu la biashara ya Import na Export ndani ya Nchi na Nchi jirani, mbali ya duniani kote kwa ujumla. Bandari hiyo itakuwa busy sana. Karibu na bandari hiyo kumetengwa eneo kwa ajili ya viwanda vitakavyozalisha au kuboresha bidhaa kwa ajili ya soko la nje ya Nchi [Export Processing Zone (EPZ)]. Pilika pilika za kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi zimeshaanza (Soma attachment mojawapo hapo chini). Nini cha kutegemewa? Bandari na Viwanda nikati ya vitu vinavyochangia sana ukuaji wa miji (makazi ya watu) pamoja nashughuli za kimaendeleo! Bandari pamoja na EPZ zitahitaji wafanyakazi wengi sana na wa aina zote kuanzia wakati wa kujenga mpaka kuendesha miradi yenyewe. Mahitaji yataanzania kwenye Makazi, Maduka, Shule/Vyuo, Nyumba za kupanga/kulala wageni, Karakana/garage za aina zote n.k. Iwe ni bustani ya matunda au mboga, shamba la mihogo au viazi, nyumba za kupangisha au kulala wageni, maduka (supermarket),vyote hivyo vitakuwa biashara. Una kiwanja au eneo lakini umekosa kabisa namna ya kuwekeza, natumaini utapata muwekezaji wakuingia naye ubia au kupanga kwenye kiwanja au eneo lako. Na kadhalika, na kadhalika. Uki-google kwa mfano; http://regionomist.blogspot.com/2012/12/the-impact-of-odessa-sea-port-on.html na http://www.sobiad.org/eJOURNALS/journal_IJBM/arhieves/2011_Vol_3_n_2/30sibel_bayar.pdf unaweza kuelewa zaidi. Uzoefu kidogo nilioupata. Mwaka 2009, eneo fulani karibu na Msata liliuzwa ekari moja kwa Tshs 200,000.00. Miaka Miwili baadaye (2011) bei ya ekari moja ilipanda kutoka Tshs 200,000.00 na kufikia Tshs1,000,000.00. Ongezeko la 400% bila stress wala kuhangaika!! Sijui kwa leo hii 2014 bei inaweza kuwa imefika kiasi gani! Wageni wameanza kunyemelea na kunyakua maeneo hayo kwa kasi. Habari nilizozisikia kutoka kwa mchina mmojawapo ni kwamba Wachina wengi wananunua viwanja au maeneo pande za Bagamoyo wakivizia fursa zinazotarajiwa. Sina kinyongo na Wachina kuwekeza (kwenye kazi halali na stahiki) hapa nchini, lakini je, sisi tuendelee kubaki kuwa watazamaji tu? Au nasi tujitose kama ambavyo wengine wametangulia?? Kila la heri na samahani kwa kuwachosha na maneno mengi!
 

Attachments

ViwanjaVilivyopimwa (Surveyed Plot) – Maeneo ya Bagamoyo.Ndugu,nakupongeza kwa fikara zako za kutaka kuwekeza kwenye viwanja au shamba pande zaBagamoyo.Kuna viwanja (SurveyedPlots) zinauzwa Tshs. 13,500.00 kwa meta moja ya mraba (TZS 13500.00 per squaremeter). Viwanja hivi vipo 6 km kabla ya kuingia Bagamoyo mjini ukitokea Dar esSalaam, upande wa kushoto. Eneo hilo linaitwa Mataya. Ramani ndogo pamoja nachati inayoonyesha viwanja hivyo pamoja na ukubwa wake imeambatanishwa.Kwa mawasiliano zaidiunaweza kutumia namba +255 754 787 775 au +255 655 787 775. Email address – gck@ksonsfreight.co.tz au info@ksonsfreight.co.tz.Kuhusu Kutapeliwa.Katika kila mradi kunaelement ya risk. Japo hatuwezi tukaacha kufanya kitu kwa kuogopa ku-risk. Chamsingi ni kujipanga na kuwa na tahadhari (Risk Management). Ni vizuri kuepukawatu wanaotaka kufanya mambo kwa uficho. Usikubali kuuziwa kiwanja au shambabila ofisi ya kijiji kujua. Pia, japo ni ghari lakini unaweza ukawahusishawanasheria ili kongeza kiasi cha risk management.Ukitaka maelezo zaidibasi tuwasiliane!Kwa nini ufikiriekununua kiwanja au eneo pande za Bagamoyo zaidi ya maeneo mengine?Bandari ya Bagamoyo(SEAPORT) na Export Processing Zone (EPZ)Bandari kubwa ya mizigoitaanza kujengwa hivi karibuni kule Bagamoyo. Kumekuwa na ongezeko endelevu la biasharaya Import na Export ndani ya Nchi na Nchi jirani, mbali ya duniani kote kwaujumla. Bandari hiyo itakuwa busy sana.Karibu na bandari hiyokumetengwa eneo kwa ajili ya viwanda vitakavyozalisha au kuboresha bidhaa kwaajili ya soko la nje ya Nchi [Export Processing Zone (EPZ)]. Pilika pilika zakuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi zimeshaanza (Soma attachmentmojawapo hapo chini).Nini cha kutegemewa?Bandari na Viwanda nikati ya vitu vinavyochangia sana ukuaji wa miji (makazi ya watu) pamoja nashughuli za kimaendeleo!Bandari pamoja na EPZzitahitaji wafanyakazi wengi sana na wa aina zote kuanzia wakati wa kujengampaka kuendesha miradi yenyewe.Mahitaji yataanzaniakwenye Makazi, Maduka, Shule/Vyuo, Nyumba za kupanga/kulala wageni,Karakana/garage za aina zote n.k. Iwe ni bustani ya matunda au mboga, shamba lamihogo au viazi, nyumba za kupangisha au kulala wageni, maduka (supermarket),vyote hivyo vitakuwa biashara.Una kiwanja au eneolakini umekosa kabisa namna ya kuwekeza, natumaini utapata muwekezaji wakuingia naye ubia au kupanga kwenye kiwanja au eneo lako. Na kadhalika, nakadhalika.Uki-google kwa mfano; http://regionomist.blogspot.com/2012/12/the-impact-of-odessa-sea-port-on.htmlna http://www.sobiad.org/eJOURNALS/journal_IJBM/arhieves/2011_Vol_3_n_2/30sibel_bayar.pdf unaweza kuelewa zaidi. Uzoefu kidogonilioupata.Mwaka 2009, eneo fulanikaribu na Msata liliuzwa ekari moja kwa Tshs 200,000.00. Miaka Miwili baadaye(2011) bei ya ekari moja ilipanda kutoka Tshs 200,000.00 na kufikia Tshs1,000,000.00.Ongezeko la 400% bilastress wala kuhangaika!! Sijui kwa leo hii 2014 bei inaweza kuwa imefika kiasigani!Wageni wameanzakunyemelea na kunyakua maeneo hayo kwa kasi.Habari nilizozisikiakutoka kwa mchina mmojawapo ni kwamba Wachina wengi wananunua viwanja au maeneopande za Bagamoyo wakivizia fursa zinazotarajiwa.Sina kinyongo na Wachinakuwekeza (kwenye kazi halali na stahiki) hapa nchini, lakini je, sisi tuendeleekubaki kuwa watazamaji tu? Au nasi tujitose kama ambavyo wengine wametangulia??Kila la heri na samahanikwa kuwachosha na maneno mengi!

Hongera sana kwa useful info, swali la chap chap. Bandari inajengwa sehemu gani exactly huko bagamoyo ? Ili tujue ni wapi tununue hayo mashamba au viwanja. Natanguliza shukrani.
 
DUH!! mbona naskia huko fukayosi ni bei chee. millioni sita mbona parefu hivo. khaaaaaaaaa!!

Hizi ni bei za Fukayosi barabarani, ukiingia nyuma kule clouds unapata kwa laki nne mpaka tano. Ila angalia sana Fukayosi ina vitapeli vingi. Mimi nimekimbilia Msata.

Kuna maeneo hata laki mbili unapata, tatizo wengi wanataka majina. Nilipoona Fukayosi maji marefu nimekwenda Madesa kwenye bei za kilala hoi.
 
Hizi ni bei za Fukayosi
barabarani, ukiingia nyuma kule clouds unapata kwa laki nne mpaka tano.
Ila angalia sana Fukayosi ina vitapeli vingi. Mimi nimekimbilia Msata.
Kuna maeneo hata laki mbili unapata, tatizo wengi wanataka majina.
Nilipoona Fukayosi maji marefu nimekwenda Madesa kwenye bei za kilala
hoi.


MKUU naomba na mm nikufuate huko MSATA, la sivo watoto wetu watakosa vya kurithi!
 
Hongera sana kwa useful info, swali la chap chap. Bandari inajengwa sehemu gani exactly huko bagamoyo ? Ili tujue ni wapi tununue hayo mashamba au viwanja. Natanguliza shukrani.
EPZ inachukua eneo kuanzia unapovuka Mto Mkuza ukiwa barabara ya Bagamoyo na usawa huo huo mpaka baharini na eneo lina extend kupita Zinga na kuendelea mpaka Kaole, Kiromo na Kitopeni. Lakini eneo la Bandari liko upande wa baharini likiwa imezungukwa (engulfed) na EPZ. Inasemekana (sina uhakika sana kwa hili) kutakuwa na uwanja wa ndege pia upande wa Kushoto. Nina kiramani kinachoonyesha eneo la EPZ lakini nikikubwa kidogo na hakiwezi ku-fit kwenye scanner ili ni-attach. Ninachoweza kusema ni kwamba maeneo hayo ya Bagamoyo mpaka Msata yatakuwa mali tu japokuwa kwa sasa maeneo jirani na Bagamoyo ni potential zaidi. But be very very careful kama unanunua shamba maeneo hayo kwani unaweza ukajikuta umenunua eneo lililo ndani ya EPZ, Bandari (au hiyo Airport). Kama ni viwanja (shamba) vilivyopimwa basi siyo shida kwani vitakuwa viko ndani ya mipango miji tayari. All the best.
 
Hizi ni bei za Fukayosi barabarani, ukiingia nyuma kule clouds unapata kwa laki nne mpaka tano. Ila angalia sana Fukayosi ina vitapeli vingi. Mimi nimekimbilia Msata.

Kuna maeneo hata laki mbili unapata, tatizo wengi wanataka majina. Nilipoona Fukayosi maji marefu nimekwenda Madesa kwenye bei za kilala hoi.
huko msata bei zake zipo vipi Malila? kuna friends zangu hapa walikuwa wanaplan kwenda fukayosi kisa wameskia maeneo bei rahisi, nimestuka ulivyosema umeambiwa 6m.
 
Last edited by a moderator:
Duh, sasa tukanunue
wapi hayo mashamba na viwanja ? Nimekimbia kigamboni kwa kuogopa
kutapeliwa yakiwemo na maeneo mengi dar. Hivi kuna sehemu isiyokuwa na
migogoro ya ardhi hapa nchini kwetu ?
Maana hivi vijisenti vyangu nisije nikachezea vibaya nikaja kujilaumu
baadae...pls jamani nisaidieni bandugu
nichek kwa namba hiyo kama unauhakika kwa ajili ya bagamoyo na kigamboni
 
Duh, sasa tukanunue
wapi hayo mashamba na viwanja ? Nimekimbia kigamboni kwa kuogopa
kutapeliwa yakiwemo na maeneo mengi dar. Hivi kuna sehemu isiyokuwa na
migogoro ya ardhi hapa nchini kwetu ?
Maana hivi vijisenti vyangu nisije nikachezea vibaya nikaja kujilaumu
baadae...pls jamani nisaidieni bandugu
nichek kwa namba 0789249110 hiyo kama unauhakika kwa ajili ya bagamoyo na kigamboni
 
huko msata bei zake zipo vipi Malila? kuna friends zangu hapa walikuwa wanaplan kwenda fukayosi kisa wameskia maeneo bei rahisi, nimestuka ulivyosema umeambiwa 6m.

Fukayosi ni kubwa, tatizo wote mnataka Fukayosi ya barabarani, ukiingia kule nyuma bei ni ndogo, tatizo miundombinu kama umeme, unaweza pata umeme mwaka 2070!!!!!!!.
 
Back
Top Bottom