Sehemu tano za kushangaza duniani

Sehemu tano za kushangaza duniani

plan z

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2019
Posts
1,394
Reaction score
1,434
Dunia ina maajabu yake. Basi leo tuangalie baadhi tu ya maeneo ambayo hukufikiria kama yanaweza kuwepo duniani na utastaajabia maajabu ya Mungu katika uumbaji wake.

1. Gates of Hell
Eneo hili lipo Russia, ni kama shimo kubwa linalowaka moto ambao hauzimiki ndani yake. Eneo hili lilikuwa kawaida hapo zamani, ikagundulika kuna gas, katika harakati za uchimbaji wa gasi hiyo ndipo walipokutana na moto, walifikiri utazimika lakini mpaka leo bado unawaka. Basi pakaitwa Gates of Hell, yaani malango ya kuzimu.

2.Reflective Salt Flats

Eneo hili lipo Bolivia, ukienda ni kama kioo unajitazama kwa chini na ni eneo kubwa lenye heka za kutosha, eneo lote lipo kama kioo unajiona chini kama vile umekanyaga kioo.

3. Shimmering Shores of Vaadhoo Maldives

Hii ni Beach ambayo maji yake ni ya kawaida lakini ukiyagusa au yakapigwa na upepo yanakuwa na rangi kama ya shoti ya umeme. Hata ukitizama mawimbi yake ni ya hivyohivyo.

4.Pink Lake Hillier

Eneo hili lipo Australia. Tumezoea kuona maji ya ziwa au bahari yakiwa na mwonekano wa rangi ya blue, japokuwa maji kama maji huwa hayana rangi. Eneo hili maajabu yake hili ziwa mwonekano wake ni wa rangi ya pink kitu ambacho sio cha kawaida.

5. Volcanic Lightning in Iceland

Ukienda eneo hili volcano yake ni ya tofauti kabisa na maeneo mengine kwani eneo hili volcano yake ni hatari zaidi, inatoka na radi pamoja na umeme, tofauti na maeneo mengine.

Kwenye hii video nilijaribu kuonyesha real clip za maeneo hayo niliyoyataja hapo juu. Bahati mbaya kipande cha kwanza cha Gates of Hell kikawa na restriction ikabidi nikikate. Kwahyo nitaweka picha tu ila maeneo mengine, namba 2 hadi 5 yapo yanaonekana real clip zake.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gates Of Hell
IMG_20200321_170925_815.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom