Sehemu ya Kazi inapogeuka sehemu ya stress na migogoro

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,753
Umeishawahi kukutana na changamoto zipi sehemu unayofanya kazi mpaka ukatamani kuacha, Kisa; kuna jamaa yangu anafanya kazi mwaka wa6 sasa kampuni flani ila hafurahii kazi, kwa muda wote huo anafanya nafasi hiyohiyo hapandi daraja, haongezwi mshahara na anafanya kazi sana (multitask), boss wake ni wa kike, mara nyingi recommendation zikitoka jamaa apewe nafasi flan yeye ndio huweka Uzibe, hiyo imekuwa kwa wakti wote, mpaka jamaa anajiuliza amekosea wapi.

Ilishatokea wakati nafasi anatakiwa azine yy sababu mzoefu ila akaletewa mtu mpya amfundishe ndio amuongoze, jamaa akapiga moyo konde maisha yakaendelea, boss wake amekuwa akimstress sana jamaa, imefikia mpk akiomba kaz sehemu zingine boss akijua anaenda kuziba (direct and indirect) hapa mnanielewa nkisema Indirect, na jamaa na boss wala hawajawahi kuzinguana, kutongozana,kumtaka, na boss humchekea jamaa, ila ndio michezo yake kuziba hata kwa wengine.

Pia jamaa ashafanya usaili sehemu nyingi ila anakosa last time alifanya usaili sehemu flani, wakamuuliza uko tayari kuanza lini na kiasi gani tukupe cha ajabu majibu yakaja kapigwa chini, sasa hapo alipo alishapachoka kwa kuwa kakaa muda mrefu sana watu wanakuja wanamkuta wanamuacha na wengine hupata offer nono sehemu zingine, kashaomba kazi sehemu zingine mpaka kachoka, usaili hufanya ila anakosa, stress ndio zinazidi, kuna muda anaona home ni sehemu salama kuliko kazini japo muda wote yy huwa humble.

Nyinyi mnaokutana na situation hizi huwa mnawezaje kukabiliana nazo?
 
Hiyo hali huwa inapunguza morali na kuharibu utendaji kazi wa mtu. Ni hali mbaya sana hiyo. Dawa ndio hiyo kutoka na kutafuta kazi sehemu nyingine.

Ila unashangaza kidogo kwa hii story yako. Huyo boss wake anamzuia vipi kupata kazi sehemu nyingine? Kamuweka kama referee kwenye CV ama vipi? Mwambie atulize akili na atafute kazi kimya kimya..sio kupigiwa tu simu ya usaili anaanza kutangaza.
 
Hata mimi amenishangaza hapo anaposema akiomba kazi sehemu nyingine Boss wake anaenda kuharibu,ina maana huyo Boss wake ana mamlaka au anajuana na makampuni yote ya Tanzania?

Kingine pia tunapoomba kazi na kuitwa kwenye interview huwa hatutangazi tunafanya kimya kimya haya ni mambo serious.
 
Tuanze ni kazi katika taasisi za serikali au private entities...kama ni serikalini hachomoki bila Boss wake kupitisha maombi yake ila kama ni private hana nguvu serikalini hasa Utumishi
 
Inategemea na industry gani yupo. Kuna fani wanajuana vibaya sana, na wanakuwa hata na informers kwenye kampuni nyingine. Nimewahi kushudia jamaa amefanya interview, kila kitu kimekwisha imebaki kupewa offer.

Mara zoezi likasitishwa, baadae kuja kufuatilia ma CEO wake aliongea na mwenzake wa hiyo kampuni mpya. Long story short, jamaa hakwenda kule, alikuwa frustrated akaamua kuondoka kabisa.

Hizi mambo zipo sana, kuna makampuni mpaka yana anti-poaching agreements, usichukue wangu na mimi sichukui wa kwako.
 
Huu mchezo tunaujua sisi.
Ishu ni kwamba anaweka namba zake kwenye CV. Zile namba zikipigwa anapokea boss anaharibu.

Afute hizo namba. Aweke za kiongoz mwingine hapo kazini
 
Si kwamba kamuweka kama referee hapana, jamaa hata anapoomba emergence leave ili akafanye usaili boss hunusa harufu flani ya jamaa kusepa, na hutumia ile Indirect way ya kuzuia jamaa kusepa, all in all ni kama hufanya kumkomoa jamaa na kumuonesha yy ni nani
 
Hata mimi amenishangaza hapo anaposema akiomba kazi sehemu nyingine Boss wake anaenda kuharibu,ina maana huyo Boss wake ana mamlaka au anajuana na makampuni yote ya Tanzania?

Kingine pia tunapoomba kazi na kuitwa kwenye interview huwa hatutangazi tunafanya kimya kimya haya ni mambo serious.
Si kwamba anajuana na makampuni yote wala sio referee wake, kwa lugha nyepesi boss yuko pale issue nyingi humtegemea jamaa amchezeshe, yaani jina la boss linang'aa kupitia jamaa, sasa hofu ni jamaa akisepa au kupanda nani atamfanyia kazi zake, maseke huanzia hapo mpk mizizi inatumika
 
Tuanze ni kazi katika taasisi za serikali au private entities...kama ni serikalini hachomoki bila Boss wake kupitisha maombi yake ila kama ni private hana nguvu serikalini hasa Utumishi
Ni Private
 
Si kwamba anajuana na makampuni yote wala sio referee wake, kwa lugha nyepesi boss yuko pale issue nyingi humtegemea jamaa amchezeshe, yaani jina la boss linang'aa kupitia jamaa, sasa hofu ni jamaa akisepa au kupanda nani atamfanyia kazi zake, maseke huanzia hapo mpk mizizi inatumika
Eh na mizizi tena
 
Inategemea na industry gani yupo. Kuna fani wanajuana vibaya sana, na wanakuwa hata na informers kwenye kampuni nyingine. Nimewahi kushudia jamaa amefanya interview, kila kitu kimekwisha imebaki kupewa offer.

Mara zoezi likasitishwa, baadae kuja kufuatilia ma CEO wake aliongea na mwenzake wa hiyo kampuni mpya. Long story short, jamaa hakwenda kule, alikuwa frustrated akaamua kuondoka kabisa.

Hizi mambo zipo sana, kuna makampuni mpaka yana anti-poaching agreements, usichukue wangu na mimi sichukui wa kwako.
Pia kampuni ambayo yupo inalipa vizuri sana kwa nafasi za juu ila level alippo jamaa malipo ni ya kawaida, usaili mwingi humshangaa why anataka asepe hiyo sehemu wakati kuna watu wanapahitaji, hupelekea kumchunguza labda kaharibu, hata wakipeleleza kupitia watu wengine hufikisha taarifa kwa boss wake kuwa kijana wako naona anataka akukimbie, hapo boss nae hutumia njia zake kuhakikisha jamaa hatoboi
 
Eh na mizizi tena
Mambo sio madogo, kuna maboss wako sehemu ila hamna kitu, na huwatumia vijana wadogo kutengeneza majina, wakibaki wao kama wao mambo huharibika
 
Rafiki yqako ni melancholic mwambie ajibu asikae kimya kwa chochote atapata Amani ya moyo.
 
Si kwamba anajuana na makampuni yote wala sio referee wake, kwa lugha nyepesi boss yuko pale issue nyingi humtegemea jamaa amchezeshe, yaani jina la boss linang'aa kupitia jamaa, sasa hofu ni jamaa akisepa au kupanda nani atamfanyia kazi zake, maseke huanzia hapo mpk mizizi inatumika
Huyo jamaa yako naye ni mzito kujiongeza.
Wewe kama ni Boss wangu huwezi kunichezesha hivyo kama mtoto wako.

Nishafanya kazi kampuni 5 tofauti na kwenye interview zote nilizoenda hakuna mtu alijua hadi nafanya resignation ya kazi watu wanakuja kujua niko na kampuni gani ni baada ya mwaka tena huwa naamua kuwasimulia rafiki zangu.

Kwa hyo bado hujanishawishi kwamba ukiamua eti Boss wako anaweza kuzuia ndoto zako.
 
Huu mchezo tunaujua sisi.
Ishu ni kwamba anaweka namba zake kwenye CV. Zile namba zikipigwa anapokea boss anaharibu.

Afute hizo namba. Aweke za kiongoz mwingine hapo kazini
yeah ,mareferee wake nao wanaeza kua source awachunguze ,unakuta umepata kazi akipigiwa referee anatoa recommendations mbaya juu yako
 
Huyo jamaa yako naye ni mzito kujiongeza.
Wewe kama ni Boss wangu huwezi kunichezesha hivyo kama mtoto wako.
Nishafanya kazi kampuni 5 tofauti na kwenye interview zote nilizoenda hakuna mtu alijua hadi nafanya resignation ya kazi watu wanakuja kujua niko na kampuni gani ni baada ya mwaka tena huwa naamua kuwasimulia rafiki zangu.
Kwa hyo bado hujanishawishi kwamba ukiamua eti Boss wako anaweza kuzuia ndoto zako.
Ntamfungua macho aache kuzubaa
 
Back
Top Bottom