Sehemu ya kuanikia nguo huwa inasahaulika katika ramani na ujenzi wa nyumba

Sehemu ya kuanikia nguo huwa inasahaulika katika ramani na ujenzi wa nyumba

Ukiwa na eneo kubwa ni rahisi kutenga eneo kwa kazi hiyo
 
Ulaya nguo hazianikwi nje ila kuna mashine za kufua na kukamua😅 zikitoka hapo zinakula pasi! Huwez kuta watu wameanika nguo nje ila kwa sisi wazee wa mapokeo tumeiga ramani zile zile bila kujua tunahitaji mazingira yakuanika nguo
Wapo wanaoanika hasa majira ya summer
 
Ata sehemu ya kuhifadhi/kutupa taka, kuna ndugu yangu kaweka bonge la garden kuzunguka nyumba ila taka zinamtesa
Ukiwa na kiwanja kikubwa unaweza kuchimba shimo refu kama la choo, unazungusha mabati na kuweka mlango ili watoto wasilifikie. Likijaa unafukia.
 
Usafi wa nguo hufanyika kila mara na hii inategemea ukubwa wa familia au wingi wa wakazi. Kuna wanaofua kila siku, kila baada ya siku au mara moja kwa wiki. Wengine Hufua kwa mashine na kukausha kwa dryer, hawa siwaongelei hapa kwani ni wachache sana.

Nguo kuanikwa hovyo hovyo kunapoteza uzuri wa nyumba. Unakuta ni nyumba nzuri barazani kuna nguo zimeanikwa. Zile za community ndiyo balaa, nguo kuonekana kambani ni sehemu ya maisha.

Kusema ukweli kutegemea nishati ya jua kukaushia nguo ni rahisi na unaokoa pesa pia mazingira. Kutumia umeme kukaushia nguo ni wakati tuna jua la ziada ni matumizi mabaya ya nishati.

Kama unajenga nyumba ni mihimu kufahamu idadi ya watu watakaoishi humo pia huduma zao kama kuanika nguo zitakuaje. Ni nyumba chache za community unakuta kuna makaro ya kufulia na miti na kamba za kuanikia nguo hasa nyuma ya nyumba. Pia unaweza kuvuta bati hasa lile transparent uweke eneo la kuanikia nguo siku za mvua.

Huwa ninakereka kuona maghorofa mazuri mjini lakini barazani nguo zimeanikwa. Uzuri wa nyumba unapotea ghafla.
Mimi nimezingatia hilo dada.. Takutumia picha uone
 
Nilibahatika kusoma shule ya RC, ilikua ni wasichana watupu hivyo pichu tulianika kwenye kamba lakini walijenga laundry room, ilikua na makaro na meza za kupigia pasi. Kusema ukweli utaratibu ulikua mzuri sana, pasi zilikua za kutosha na kama hutaki vurugu weekend unawahi mapema laundry.

Like the school nilisoma
 
Mleta tunaomba picha ya Laundry, na hizo sehemu za kunyooshea na kufulia...
 
Back
Top Bottom